Monday 28 September 2015

FILAMU YA MAMA LISHE YAINGIA MTAANI LEO

Filamu ya Mama Lishe imeingia mtaani leo ikisambazwa na steps entertainment,filamu hiyo imechezwa na Halima Yahaya maarufu kama Davina akiwa na Issa Mussa Clouds,Swebe na wasanii wengine wengi.

Akifunguka kiafrika bila hofu yoyote kwakua Tanzania ni nchi huru Davina amesema filamu hiyo inamafundisho makubwa sana kwenye ndoa ikiwa ni pamoja na kutomuamini rafiki yako wa karibu na madhara ya kufanya ngono zembe yanavyoalibu kizazi cha sasa na familia kwa ujumla

Davina anasema kwenye filamu hii amecheza kama mama lishe mwenye familia,nakuonesha changamoto wanazopata kina mama lishe kwa waume zao

filamu hii ipo madukani kuanzia sasa pata nakala yako halisi sasa

Wednesday 23 September 2015

HEMED AMPOKEA WASTARA KWA MIKONO MIWILI

Mcheza filamu wenye jina kubwa nchini Hemed Suleiman  ameonesha uhodari wa ali ya juu kwa kumpokea muigizaji mwenzie Wastara Juma kwa mikono miwili

Hemed ameya fanya hayo kwenye filamu ya Mama na Mwana baada ya kuamua kubeba shida zote za Wastara na mtoto wake na kumuacha Yusuph Mlela akiwa njia panda asijue pakwenda

Filamu ya Mama na mwana iliyoandikwa na kuongozwa na Leah Mwenda Mseke inatoa mafunzo kwenye ndoa jinsi ya kuishi na mtoto mlemavu,na kuonesha yeye ana haki

Akiongea na muandishi wa habari hii Wastara amesema kumekua na kawaida ya familia kuwatenga watoto wenye ulemavu na kuona kwamba hawana thamani ya kuishi kitu ambacho sio sawa,ndio maana alipambiwa acheze filamu hiyo hakusita

"niliongea na Lmata akaniambai kuna story anacheza Mlela,lakini stoey hiyo inakutaka wewe hivyo naomba ushiriki kwenye kucheza tutao kitu kizuri sana"

filamu hiyo ipo mtaani na inasambazwa na kampuni ya steps entertainment kwa mawsiliano zaidi jinsi ya kupata filamu hii na filamu zote za steps wasiliana nao kwa namba 0764 547 381,0713 570 581 au 0716 78 88 05

Tuesday 22 September 2015

CLOUD 112 AMERUDI NA MUHANGA

Baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu atimae mcheza filamu mkongwe Tanzania Issa Mussa maarufu kama Cloud 112 amerudi kwa kasi na filamu ya Muhanga akiwa na Barafu pamoja na Luckess Mokiwa

Filamu hiyo inayosukumwa mtaani na kampuni ya Steps entertainment inamuelezea mwanamke ambae ameolewa lakini ndoa yake inaingia dosari baada ya kukaa muda mrefu bila kubeba ujauzito

Atimae anashauriana na rafiki yake watafute mwanamke ambae ata beba ujauzito na mwisho wa siku mtoto akizaliwa amchukue kisili bila mama yake kujua