Tuesday 20 December 2016

Gabo: Mtindo wa Maisha Yangu ni Tofauti na Wenzangu

Msanii Gabo Zigamba ameweka wazi kuwa hana tofauti na wasanii wenzake kama ambavyo imekuwa ikilalamikiwa na wengi kuwa msanii huyo haelewani na wenzake.

Akizungumza na East Africa Television, Gabo amesema kinachomfanya aonekane ana tofauti na wasanii wenzake ni utoafuti wa mtindo wa maisha alionao, lakini hana tatizo nao na anawapenda kwa dhati.
“Hakuna msanii ambaye sielewani naye, sema lifestyle yangu mimi ndiyo haifanani na wao, lakini naelewana na wasanii wote nawapenda wananipenda, mimi nawapenda kwa dhati ya moyo, sijui wao kama wananipenda kwa nafsi ya uso, ila sina kikwaruzo, sina ugomvi, ila utofauti unapoonekana unaweza mtu ukakunja kwa sababu ndiyo tatizo la watanzania, ila mimi niko sawa nao labda wao wasiwe sawa na mimi”, alisema Gabo.
Gabo aliendelea kusema kwamba tofauti kubwa iliyopo kwake na wasanii wenzake ni matarajio yake ya kufanya utofauti kwenye tasnia ya filamu hapa nchini.
“Unajua kila mmoja ana nafasi yake kwa mashabiki wake, siwezi nikasema najiona tofauti na wao, ila naweza kusema natarajia kufanya vitu tofauti na wao walivyovifanya”, alisema Gabo.

KUMBE MIMBA YA NISHA ILIKUWA KIKI TU

 Wiki kadhaa zimepita tangu muigizaji  Salma Jabu nisha kuweka picha mtandaoni akiwa mja mzito na kusema ujauzito huo umetokana na kubakwa na aliyekua mpenzi wake ambae ata hivyo hajamuweka wazi
 Akifunguka kiafrika bila hofu yoyote kwa kua Tanzania ni nchi huru amesema yeye sio mjamzito ila amesema hivyo ili kuona mtu mwenye ujauzito uliotokana na kubakwa jamii inampokeaje anapoweka wazi swala lake
 "mimi sina ujauzito ata ile picha yangu ya kwanza kuweka mtandaoni na kujitangaza ni mimi,sikua mimi ile ni picha ya mdada wa Nigeria nimeitumia tu"
Amesema kwa yupo kwenye maandalizi ya filamu yake mpya amabayo imelenga mambo ya mimba za utotoni na ataifanya vizuri kwakua ameshapitia kipindi cha ujauzito wa mtu aliyebakwa na kutelekezwa


kwa sasa Nisha anatamba na filamu ya Kiboko kabisa akiwa na mkongwe wa tasnia hii King Majuto,inasongezwa mtaani na kampuni ya steps entertainment.

Tuesday 13 December 2016

FILAMU YA SIRI YA MOYO SASA INAPATIKANA KWENYE AFROBOX

 Filamu kutoka kwa muigizaji anaekuja juu kwa kasi nchini Man Fizo imeanza kuoneshwa kwenye application ya Afrobox inayopatikana kwenye play store kwa wale wenye simu za android na app store kwa wenye simu za apple
 Wasanii wengine ambao wameonesha uwezo mkubwa kwenye filamu hiyo ni pamoja na Mwanaher,Kupa pamoja na Mzee majuto wakiwa sambamba na msanii chipukizi kabisa kwenye tasnia Careen Jonas
Mbali na kuoneshwa kwenye Afrobox filam hiyo inasambazwa na kampuni ya steps entertainment kwa mfumo wa DvD nchi nzima,usikose nakala yako halisi

Saturday 3 December 2016

UZINDUZI WA SIRI YA MOYO WATIKISA DAR ES SALAAM

wasanii wa filamu ya siri ya moyo wakiwa na waandaji wa uzinduzi wa filamu hiyo



Mcheza filamu Rammy Galis


Msanii fizo



Uzinduzi wa filamu ya Siri ya moyo umefanyika kwenye ukumbi wa sinema Suncrest ulipo ndani ya jumba la biashara,Quality centre na kuudhuriwa na mamia ya mashabiki wa filamu nchini

Akifunguka kiafrika bila hofu yoyote muandaaji na muhusika mkuu wa filamu hiyo Salum Salehe(man fizo) amesema filamu hiyo ameitengeneza visiwani Zanzibar na imeghalimu dora 13799.45 sawa na zaidi ya milioni 30 kwa madafu ya kibongo

Aidha amesema wahusika wote wameonesha uwezo mkubwa kwenye nafasi zao jambo lilifanyanya muongozaji asipate shida sana kuwaongoaza

"kwenye filamu hii wahusika ni mimi mwenyewe,Mwanaheri,Careen,Deus,Kupa pamoja na Mzee Majuto,ni hadithi ambayo kila mtu ataipenda itakapo kuwa madukani msikose"

Filamu ya siri ya moyo inatarajia kuingia sokoni tarehe 12 mwezi wa 12 mwaka 2016 na inasambazwa na kampuni ya Steps entertainment.