Tuesday 26 May 2015

SALMA JABU NISHA KUJA NA MTAA KWA MTAA MWISHO WA NWEZI HUU

 Mcheza filamu anejizolea umaarufu kwenye uchekeshaji Salma Nisha nakuja na filamu ya mtaa kwa mtaa mwisho wa mwezi huu
Kwenye filamu hiyo wamo pia Hemedy,Tausi,Diana Kimaro pamoja na Asha Boko na wengine wengi
 Filamu hiyo anazungumzia  maisha ya traffick feki ambae anatumia nguo za jeshi la polisi vibaya na mwisho wa siku anajikuta kwenye matatizo makubwa
 Filamu hiyo inasambazwa na steps entertainment limited itaingia mtaani mwisho wa mwezi huu


ODAMA KUJA NA BIG SUPRISE MWEZI UJAO

 Mcheza filamu anaesumbua sana bongo kwa hivi sasa Jennifer Kyaka jina la kumuingizia kipato Odama anakuja na filamu ya Big suprise akiwa na na Salim Ahmed jina maarufu Gabo pamoja na mastaa wengine wengi
 Filamu hiyo inayosambazwa na kampuni ya steps entertainment imewashirikisha pia wasanii wengine kama vile Kupa,Pastor Miyamba,Jengua pamoja na Mutrah itakuwa sokoni mwezi ujao
 Filamu hiyo inaelezea kisa cha mwanamke aliekuwa kwenye ndoa lakini akawa anachepuka na vijana wadogo mwisho wa siku mume wake anamfumania na kuamua kumpa adhabu inayompa wakati mgumu sana
Mutraha na Odama


Gabo

Odama na Gabo

Kupa na Gabo

Odama

Friday 8 May 2015

MUTRAN:WOLPER AMENIPA TABU SANA KWENYE HUBA

 Mcheza filamu Mutrah Tamimu ambae anasumbua huvi sasa na filamu yake ya HUBA inayosambazwa na kampuni namba moja ya usambazaji Tanzania Steps Entertainment amesema Wolper amempa wakati mgumu walipokua wanaandaa filamu hiyo kutokana na mvuto wake.
 Akifunguka kiafrika bila hofu yoyote kwakua Tanzania ni nchi huru,amesema kuwa ilikua ngumu sana kucheza vipande vya kimapenzi na Wolper kutokana na urembo wake ila anashukuru kuwa ameweza na ameitendea haki filamu hiyo
 Kwenye filamu hiyo wamo pia Mzee Majuto pamoja na Neema ambao wameitendea haki sana,uku ikipigwa picha na Kabuti Onyango na kuongozwa na Leah Mwendamseke ambae pia ndio muandishi wa filamu hiyo
kwa mahitaji ya jumala na reja reja wasiliana kwa namba 0716 788 805 na 0713 570581 sio ya kukosa

Tuesday 5 May 2015

BAADA YA HAKUNA MATATA SASA NISHA ANAKUJA NA MTAA KWA MTAA

FILAMU YA KIMENUKA YA MAFUFU YAIBIWA


Kupitia ukurasa wake wa instagram Jimmy Mafufu amendika 

Ndugu zangu mashabiki na wadau wa film zangu nasikitika kuwaambia kuwa Film yangu mpya iko jirani sana kutoka lakini Mtu mmoja mjinga asiyependa mafanikio yangu kana kwamba alihusika kunitoa baada ya kujua ninatoa film niliyowaahidi hivi karibuni na yeye amechukua jina la film yangu huku akijua nimelitumia jina hilo na film nimeshauza Steps na iko mbioni kutoka nilimsihi kabla hajatoa

 akakaidi na kuruhusu kifilm chake kibovu kitoke nimehuzunika sana maana nimekula hasara na kubwa niliwalipa wasanii wakubwa wa bongofreva wakafanya sound track na vitu vingi vimekula pesa lakini mjinga huyu ameona yote hayo ni upuuzi kubwa zaidi muandaaji wa film hiyo ndiye aliyeweka sauti (voice over) katika film Yangu na amekiri kuwa amemuuzia huyo aliyenitenda hayo na film yake iliitwa 

(SIKU MOJA)anasema baada ya kuuza film.hiyo mnunuzi alishawishi iitwe KIMENUKA jina ambalo ni la kwangu na film tayari lakini Muhafidhina huyo aligoma na kudai mafufu ni Mtu mdogo akatumia nguvu kujitwalia jina la film yangu kwa hiyo film nitaitoa na kuanzia sasa Sintatumia jina la KIMENUKA ukiiona film yenye jina hilo sio langu na film hiyo siyo yangu jina nitalitangaza hivi karibuni yaliyotokea 
nimemwachia Mungu na kama walidhani wameniwin wamechemsha na kikazi nimejipanga Pumbavu sana.