Monday 12 October 2015

LUCY KOMA AMERUDI NA "TANZANIA TO DENMARK AKIWA NA SLIM OMARY

 Muigizaji mkongwe kwenye tasnia ya filamu Lucy Komba amabae anapiga mziko nchini Denmark amerudi na filamu ya 'From Tanzania to Denmark akiwa na Slim Omary  na wenginie wengi kutoka nchini humo


Filamu hiyo inayomuhusu binti ambae alikenda Denmark na kukutana na misuko suko mingi kabla ajakutana na mpenzi wake na kuanza kuishi pamoja inasambazwa na kampuni ya steps entertainment pata nakala yako sasa

AUNT EKIEL:NAFANYA CHOCHOTE KUKIDHI MAITAJI YANGU,NITAWAFURAISHA

 Filamu ya Mwajuma nipe ya Aunt Ezekiel imeingia mtaani leo ikisambazwa na steps entertainment,filamu hiyo ambayo amewashirikisha Mzee majuto,Stanley Nsungu na wengine wengi inaelezea jinsi msichana Mwajuma anavyoweza kujutolea chochote alicho nacho kukidhi mahitaji yake

Aint Ezekiel anasema 'Nafanya chochote ili  kukidhi mahitaji yangu,ni mazoea ya jamii yetu kudharau na kutowathamin wanawake,lakin si mimi Mwajuma nipe ni zaidi ya mwanamke chungu na tamu naifahamu lazima nitawafuraaisha kwa gharama yoyote ile"




Saturday 10 October 2015

Ester Kiama avamiwa, apewa kichapo ajeruhiwa!

Staa wa Filamu za Kibongo, Ester Kiama juzikati alijikuta kwenye wakati mgumu baada ya kuvamiwa na vibaka na kuchezea kichapo kisha kuibiwa pesa na simu mbili.

Sosi aliye karibu na staa huyo aliyeomba hifadhi ya jina lake alidai kuwa, siku ya tukio Ester alitoka viwanja na wenzake, walipofika Kijitonyama jijini Dar yeye akiwa anaendesha gari, aliwashusha wenzake lakini wakati anarudi kwenye gari ili aondoke, wakatokea vijana wawili na pikipiki wakamfanyizia.


Ijumaa lilipopata taarifa hizo lilitinga nyumbani kwa Ester na kumkuta akiwa hoi sambamba na majeraha, alipotakiwa kueleza kilichompata alikiri kufanyiwa unyama huo ambapo alisema anajuta kutembea usiku bila kuwa na mwanaume.


Monday 5 October 2015

IVONY BIRINGWA STAA WA FILAMU YA HEART ATTACK AKIWA KWENYE UBORA WAKE




ESTER KIAMA:MUHANGA INA MAFUNZO MAKUBWA KWENYE NDOA

Staa wa filamu za kibongo nchini Ester Kiama amesema filamu ya Muhanga ina mafunzo makubwa kwenye ndoa,kwa kua stori yake inalenga maisha halisi ya matatizo wanayokutana nayo wanandoa,wengi wanaotafuta mtoto
 Ester amesema filamu hiyo inahusu wanandoa waliokaa mda mrefu bila kupata mtoto,mpaka mama mkwe akawa anamsumbua mtoto wake wa kiume jambo lililopelekea mtoto huyo kujitoa Muhanga

Anasema kwenye filamu hiyo ambayo ameshiriki na Issa Mussa cloud,Suleiman Barafu,pamoja na Luckness Mokiwa yeye amacheza kama mwanamke ambae ameamua kuzaa na mume wa mtu kwa makubaliano maalum ili kuioka ndoa ya mwanaume huyo
"kwenye filamu hiyo mm ndio mwanamke ambae Cloud alinifata nimzalie mtoto baada ya mkewe kuonekana hawezi kuzaa kabisa,hivyo akajitoa muhanga kuja kwangu kwa makubaliano maalum zaid nunu filamu hii ujifunze mambo mengi "

filamu hiyo ipo madukani kote Tanzania inasmbazwa ns steps entertainment

Friday 2 October 2015

THE SCAR YA MKUTANISHA RIYAMA NA RADO

Filamu ya the scar imetoka leo ikiwa imechezwa na mastaa kama Rado na Riyama,na wengine wengi,filamu hii inasmbazwa na steps entertainment sio ya kukosa,pata nakala yako sasa