Monday 18 July 2016

KAMA UMEPITWA NA PREMIERE YA SIKITU PICHA ZIKO HAPA















SIKITU YA KAJALA IMETOKA LEO

Filamu ya Sikitu kutoka kwa muigizaji mkubwa Tanzania Kajala Masanja imetoka leo,inasambazwa na kampuni ya Steps Entertainment

Kwenye filamu hiyo iliyoandikwa na kuongozwa na Leah Richard imechezwa pia na wasanii kama vile Asha Boko,Tausi,Hemedi na wengine wengi


Monday 4 July 2016

Iyobo amtaka Aunt ajichore kama Shilole

DAR ES SALAAM: Dansa kutoka Wasafi Classic Baby (WCB), Moses Iyobo ‘Moze’ ambaye ni mzazi mwenza wa staa wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel Grayson, amemwambia mpenzi wake huyo kuwa na yeye ajichore ‘tatuu’ ya jina lake kama ilivyokuwa kwa msanii Zuwena Mohammed ‘Shilole’ kwa Naftal Mlawa ‘Nuh Mziwanda’ kabla ya kumwagana.
Moze alimwambia hayo Aunt baada ya mwanadada huyo kujichora mkononi kwa kalamu maneno yaliyosomeka; ‘Aunt wa Mose Iyobo’ ambapo jamaa huyo alimsisitizia kuwa kama kweli anamaanisha hivyo, basi ajichore kama Shilole alivyofanya kwa Nuh.
“Kama mama Cookie (mtoto wao) anataka kujilipua, ajichore kama Shilole alivyofanya kwa Nuh maana alivyojichora kwa kalamu, hata akioga, inatoka,” alifunguka Moses.

Saturday 2 July 2016

MWANAHER YA MWANAHER KUINGIA SOKONI JUMATATU IJAYO

Filamu ya Mwanaheri inaingia sokoni jumatatu ijayo ikisambazwa na kampuni ya steps entertainment,filamu hiyo iliyochezwa na Riyama Ally,Mzee majuto,Frola Mvungi na Mwanaher mwenyewe ina kisa cha kusisimua ambacho kime "base" kwenye maisha halisi ya kitanzania

Akiongea na blog hii Mwanaheri amesema filamu hii ina mafundisho makubwa sana kwa watu walioingia kwenye ndoa na wanaume watu wazima

"filamu hii ina fundisha jinsi sisi watoto wa kike tunavyopata mitihani mingi baada ya kuolewa na watu wanaotuzidi miaka mingi"

Mbali na filamu hii Mwanaheri anatamba sokoni na filamu mbili Makusaro Pumu

SIKITU KUZINDULIWA SUNCREST QUALITY CINEMA QUALITY CENTRE

Filamu ya Sikitu kutoka kwa Kajala Masanja inatarajiwa kufanyiwa uzinduzi mwishoni mwa wiki ijayo kabla ya kuingia sokoni

Filamu hiyo iliyochezwa na wasanii wengi wenye uwezo mkubwa akiwemo Taiya,Mutrah,Jada,Asha boko na wengine wengi,ina story nzuri ya kugusa itakayo kufanya usichoke kuiangalia imeandikwa na kuongozwa na Leah Richard Mwendamseke

Uzinduzi wa filamu hii upo chini ya kampuni kubwa kabisa ya usambazaji nchini steps entertainment