Monday 30 May 2016

KAJALA:NIMEJIFUNZA MENGI WAKATAI NASAMBAZA FILAMU YA PISHU

Mcheza filamu mwenye jina kubwa Kajala Masanja amesema amejifunza mambo mengi wakati anasambaza filamu ya Pishu kupitia kampuni yake ya Kajala entertainment

Amesema kikubwa kinachowashinda wengi wanaosambaza kazi zao ni kukulurupuka bila kulijua kiundani soko,linaitaji nini na jinsi ya kufikisha kazi kwa walaji wa mwisho bado imekua tatizo kubwa

"Ugumu unakuja mtu ujui soko linataka nini na jinsi ya kuwafikia wateja kwa wakati hii inatokana na mfumbo mbovu wa usambazaji uliopo ata msanii akitaka kusambaza kazi zake ajui atumie njia gani

Filamu ya Pishu iliyoongozwa na Lamata bado ipo madukani pata nakala yako halisi sasa

ROSE NDAUKA ATEMBELEA KITUO CHA WATOTO YATIMA KUPATA BARAKA ZA FILAMU YAKE YA ANGELA

Rose Ndauka na watoto yatima
 Mcheza filamu mwenye jina kubwa Bongo Rose Ndauka mwishoni mwa wiki hii ametembelea kituo cha kulelea watoto yatima kilichopo Kigogo Dar es salaam na kuwapa zawadi ili apate baraka kwenye filamu yake ya Angela inayotoka leo
Rose Ndauka,Sharoasla na mlezi wa kituo

Rose Ndauka na team yake

Gomesa na Beatrice

Tuesday 17 May 2016

RACHEL BITULO AMEFANYA MAKUBWA KWENYE NIMEKOSEA WAPI

Mcheza filamu za kitanzania Rachel Bitulo ameonesha uwezo mkubwa kwenye filamu ya Nimekosea wapi amabyo imetoka mwanzoni mwa wiki hii

kwnye filamu hiyo amevaa uhusika wa watu wawili kwa wakati tofauti jambo ambalo limewashangaza wengi kwa jinsi alivyomudu kucheza nafasi hizo mbili bila kuionesha mapungufu yoyote
Mbali na Rachel filamu inayosambazwa na kampuni ya steps entertainment wamo Gabo zigamba na Man fizo uku wakipewa sapoti na wasanii wengine wengi pata nakala yako sasa ipo madukani

FILAMU YA MWISHO YA MAREHEMU KINYAMBE HII HAPA

STEPS ENTERTAINMENT BONGO MOVIE PREMIER QUALITY CENTRE.

Friday 6 May 2016

NIMEKOSEA WAPI? KURUKA SUNCREST QUALITY CENTRE KATIKA BIG SCREEN!

FILAMU kubwa ya kitanzania ya Nimekosea wapi? ya mtayarishaji na mwigizaji mahiri Swahilihood Salum Saleh ‘Fizo’ itakuwa ni filamu ya kwanza kufungua njia kuonyeshwa katika jumba la sinema la Suncrest Cineplex Cinema lilopo Quality Centre wiki ijayo.


 Fizo amesema kwake ni bahati kubwa sana kupata nafasi hiyo kwa filamu yake kuwa ya kwanza kutoka kampuni ya Steps Entertainment kuanza kuonyeshwa katika Jumba la sinema katika Big Screen na kuingia katika hatua nyingine ya biashara.
“Namshukru sana Mwenyezimungu kwa kupata bahati hii nimetengeneza filamu kubwa na inaonyeshwa katika ukumbi wa filamu kwa hadhi kubwa, nipo na wasanii wakubwa Gabo zigamba na wengine,”anasema Man Fizo.
Filamu ya Nimekosea wapi? inatarajia kuonyeshwa tarehe 11.May.2016 kwenye Bongo Movie Premiere kuanzia saa 1:00 ambapo wasanii watapita katika Red Carpet na kuingia ukumbi kwa ajili ya kuona sinema yenye ubora mkubwa.
Tarehe 12.may.2016 hadi tarehe 15. May. 2016 saa 2:00 kamili usiku kila siku sinema ya Nimekosea Wapi? itaonyeshwa katika ukumbi wa Suncrest Cineplex Cinemas na wapenzi wa filamu kujionea hatua kubwa kutoka kwa wasanii wa kitanzania wakifanya mambo makubwa.
Na tarehe 16. May. 2016 filamu ya Nimekosea wapi itaingia mtaani kwa maana hatua ya Dvd.