Monday 23 November 2015

KAJALA MASANJA"NAPENDA SANA KUCHEZA FILAMU,NDIO MAISHA YANGU

 Mcheza filamu mwenye jina kubwa Tanzania kwa uwezo wake wa kuigiza Kajala Masanja amesema anapenda sana kucheza filamu kwani ni moja ya vitu anavyovipenda sana kwenye maisha yake,

amesema tangu akiwa na umri mdogo amekua akipenda nakutamani kucheza filamu mara nyingi sana jambo ambalo akilifanya anajisikia faraja zaidi.
 "mimi napenda sana kucheza filamu yani sana natamani ata kwa mwaka nicheze filamu tano,yani filamu ni sehemu ya maisha yangu"
 Kajala Masanja amecheza filamu nyingi za zimependwa na watu wa lika zote,na kwa sasa anatamba sokoni na filamu ya hii ni laana aliyocheza na Gabo Zigamba
Mbali na filamu hiyo pia Kajala amecheza filamu kama vile Pishu na wake up ambazo pia zinafanya vizuri sokoni

JB NA WEMA WAKUTANA TENA KWENYE FILAMU YA CHUNGU CHA TATU

Mcheza filamu mwenye jina kubwa Tanzania Wema Sepetu anatarajia kukutana tena na mkongwe wa fani hiyo Jacob Steven kwenye filamu ya chungu cha tatu

Filamu hiyo ambayo ina husu mwanadada Doreen (wema sepetu) an aingia kwenye mahusiano na wanaume wa tatu tofauti kwa kile anachoamini kuwa atapata mtoto na badala yake kupambana na visa na mikasa ya kusisimua

Kwenye filamu hiyo inayotoka mwezi ujao wamo pia Patcho,Mwamba,Mau na wengine wengi inatarajiwa kuasmbazwa na steps entertainment kwa jumla na reja reja wasiliana nao kwa namba 0713 570 581 au 0716 788 805

FILAMU YA FIGISU FIGISU INATOKA MWISHONI MWA MWEZI HUU

KUTANA NA MUANDISHI ALIETEKWA NA KUTOROKA NDANI YA WHO"S BACK