Tuesday 21 March 2017

CLOUD 112 AWAVUTA WASTARA NA BARAFU SWEDEN KUFANYA MOVIE YA USIJISAHAU

 Wasanii wenye majina makubwa bongo movie Wastara Juma na Suleiman Barafu wapo nchini Sweden wakifanya stage play kwa watanzania wanaoishi nchini humo,kwa lengo la kuwaelimisha mambo mbalimbali ya kimaisha kupitia sanaa za jukwaani
 Aidha Wastara na Barafu wako nchini humo pia kwa maandalizi ya filamu ya Usijisahau inayoandaliwa na mcheza filamu mkongwe nchini Cloud 112
 Filamu hiyo yenye maudhui ya kislamu inaenga kuwafumbua macho watu,waishi kwa kumtegemea mungu wasijisahu wafanye ibada


Wednesday 15 March 2017

LUTWAZA KUZIBA PENGO LA KANUMBA KWENYE FILAMU


Mcheza filamu anaefanya vizuri kwenye tasnia Philemon Lutwaza ametajwa kuwa ndio mwenye jukumu la kuziba pengo la marehemu Steven Kanumba kutokana na kufanana kwa muonekano na uigizaji wake

Wakifunguka kiafrika bila hofu yoyote baadhi ya mashabiki wamesema Lutwaza anaweza kuziba pengo kwani anajituma sana kwenye kazi na hajatofautiana sana na marehemu Kanumba

"Unajua huyu Lutwaza anacheza vizuri sana na nina vutiwa na uigizaji wake anajua yani nikimuangalia namuona Kanumba kabisa"
Lutwaza anaonekana kwenye filamu ya Yai viza ambayo imeandaliwa na muongozaji wa filamu nchini Sulesh Mala

UJIO MPYA WA VINCENT KIGOSI # GATE KEEPER







Filamu ya Gatekeeper kutoka kwa mcheza filamu Vicent Kigosi (Ray) imeingia sokoni wiki iliyopita na kufanya mapinduzi ya filamu nchini



mashabiki wa filamu wametoa maoni yao kuhusiana na filamu hiyo jinsi ilivyochezwa kwamba ni tofauti na filamu zake zote zilizopita



filamu hiyo imewausisha wachezaji wakongwe kwenye tasnia akiwemo Single Mtambalike (richi) Hidaya Njaidi na Mr masinde uku ikibeba chipukizi wengi kwenye game ya filamu nchini

Monday 6 March 2017

GATEKEEPER YA RAY YAINGIA SOKONI LEO

Filamu ya Gatekeeper kutoka kwa mcheza filamu mwenye jina kubwa nchini Ray imeingia sokoni leo

Filamu hiyo iliyojaa mastaa kama vile Kajala na Richi imetajwa kuwa filamu bora kuwai kutokea tangu kifo cha marehemu Kanumba

Filamu hiyo imezinduliwa wikendi iliyopita imeonekana kuteka hisia za watu wengi kutokana na mtililiko wa stori yake

ipo madukani nchi nzima itafute uone utofauti na uwezo mkubwa wa kuigiza uliofanywa na wasanii nguli kwenye tasnia ya filamu nchini

Ray Ashindwa Kuishi na Chuchu

 DAR ES SALAAM: Pamoja na kumzalia mtoto wa kiume aitwaye Jaden, staa wa sinema za Kibongo, Vincent Kigosi ‘Ray’ anadaiwa kushindwa kuishi na mwandani wake, Chuchu Hans ambaye naye ni mkali wa Bongo Muvi, kisa kikielezwa kuwa ni mama wa jamaa huyo ambaye hataki mwanaye aishi mbali naye.
 Habari za kuaminika zilieleza kuwa, Chuchu amekuwa akitangaza kwamba, amefunga ndoa na Ray lakini jamaa huyo amekuwa akikanusha hivyo mwanamama huyo kuwa kwenye wakati mgumu.
Hata hivyo, habari za ndani zilieleza kuwa, Ray ambaye amempangishia nyumba Chuchu maeneo ya SinzaDarajani, Dar amekuwa akienda nyumbani hapo kwa mzazi mwenzake lakini kila inapofika usiku wa manane huwa anamkimbia na kurudi kulala nyumbani kwa mama yake, Sinza-Mori, Dar. “Yaani hakuna kitu kinachomuumiza Chuchu kama hicho.
Lakini kibaya zaidi Ray amekuwa na msimamo mkali kwamba hawezi kumwacha mama yake na kwenda kuishi na Chuchu. Mbali na hilo pia Ray hawezi kuishi na Chuchu pale kwa mama yake kwa sababu kuna mambo hayajakaa vizuri kati ya Chuchu na mamamkwe wake,” kilisema chanzo chetu na kuongeza:
“Ray anapaswa kumaliza tatizo hilo ili mtoto wao apate malezi ya baba na mama kwa saa ishirini na nne.”
Wikienda lilipomtafuta Ray alikiri kushindwa kuishi au kukaa na Chuchu kwa muda wote kutokana na ukweli kwamba, mama yake hapendi ahame nyumbani na kwenda kupangisha kwani yeye ni kama ‘mume’ wa mama yake kwani ni mtoto wa mwisho hivyo anamuangalia mama yake.
“Ni kweli ninaishi nyumbani kwetu, siyo kama sina nyumba na kuishi nyumbani siyo dhambi. Uwezo wa kupanga ninao lakini mama yangu hapendi nihame nyumbani kwetu.
“Ni kweli mama mtoto wangu (Chuchu) anaishi kwake na mimi ninaishi nyumbani kwetu. Mama yangu alishaniambia hata nikihama atakuja kuishi na mimi nyumbani kwangu.
“Chuchu Hans anajua kuhusu hilo ndiyo maana hata nyumba anayoishi nimempangia mimi,” alisema Ray aliyelelewa na mama yake pekee tangu baba yake alipofariki dunia wakati staa huyo akiwa na umri wa miaka nane.
Wikiendi iliyopita Ray alizindua sinema yake mpya ya Gate Keeper ambayo alieleza kwamba imelenga kuvunja ukimya wake wa muda mrefu tangu alipofariki dunia, mshindani wake kwenye soko la sinema za Kibongo, Steven Kanumba mwaka 2012.

CHEKI KILICHOJIRI KWENYE UZINDUZI WA FILAMU YA GATEKEEPER KUTOKA KWA RAY