Monday 28 September 2015

FILAMU YA MAMA LISHE YAINGIA MTAANI LEO

Filamu ya Mama Lishe imeingia mtaani leo ikisambazwa na steps entertainment,filamu hiyo imechezwa na Halima Yahaya maarufu kama Davina akiwa na Issa Mussa Clouds,Swebe na wasanii wengine wengi.

Akifunguka kiafrika bila hofu yoyote kwakua Tanzania ni nchi huru Davina amesema filamu hiyo inamafundisho makubwa sana kwenye ndoa ikiwa ni pamoja na kutomuamini rafiki yako wa karibu na madhara ya kufanya ngono zembe yanavyoalibu kizazi cha sasa na familia kwa ujumla

Davina anasema kwenye filamu hii amecheza kama mama lishe mwenye familia,nakuonesha changamoto wanazopata kina mama lishe kwa waume zao

filamu hii ipo madukani kuanzia sasa pata nakala yako halisi sasa

No comments:

Post a Comment