Friday 31 October 2014

DAVINA: BONGO MOVIE HAIJANIPA MUME

MSANII wa filamu Bongo, Halima Yahya ‘Davina’ amesema wanaomsimanga kuwa amepata mume kwa sababu yao hawana hoja kwa sababu Bongo Movie Unity haina ubavu huo.

“Mimi sijatafutiwa mume na Bongo Movie, alinitafuta mwenyewe baada ya kuniona kwenye muvi yangu ya Tone la Damu akiwa Italia, sasa nashangaa na ninaumia ninaposikia eti Bongo Movie walinitafutia.
“Ukweli naombeni mniache kwa sababu hakuna aliyehusika kwa kitu chochote kunikutanisha na mume wangu, hivyo acheni kunisengenya na mimi siringi kwa chochote kama ni kutoka huko kwenye kundi ni maamuzi yangu maana sikuwa naona faida yoyote,” alisema Davina.

ROSE NDAUKA: SIFAGILII WANAUME TENA

STAA wa filamu Bongo, Rose Ndauka amesema kuwa kwa sasa yupo bize na malezi ya mwanaye hivyo hana mpango wa kuwa na mwanaume yeyote hata awe pedeshee mwenye uwezo wa fedha kiasi gani kwani mwenyewe anajitosheleza.

kipindi hiki hafagilii kabisa mambo ya mabwana na wala hahitaji mapedeshee kwa kuwa yeye mwenyewe ana uwezo wa kujitosheleza kifedha. “Mimi sina bwana kwa sasa na wala sihitaji hao mapedeshee, watanisaidia nini wakati nafanya kazi zangu zinazoweza kuniingizia fedha, nina akili timamu, nina miguu na nina macho sasa kwa nini nitegemee pesa ya mtu?” alihoji Rose.
Kwa mara ya kwanza...

ODAMA: NIKO KWENYE UHUSIANO MAKINI

MWANADADA mwenye mvuto wa kipekee ndani ya tasnia ya filamu Bongo, Jennifer Kyaka ‘Odama’ amefunguka kwamba kwa sasa yupo kwenye uhusiano makini (serious) na muda si mrefu ataolewa.

Odama alisema: “Ukweli kwa sasa niko kwenye uhusiano siriasi na tuko kwenye mipango ya ndoa japokuwa siwezi kutaja mwezi au tarehe ila mashabiki watambue kwamba nitaolewa soon.”
Alipotakiwa kutaja angalau jina la mwanaume wake huyo, msanii huyo aliweka ngumu na kudai haina umuhimu kwa sasa hali inayoashiria huenda ni mume wa mtu na kwamba akimuanika atakinukisha.

Thursday 30 October 2014

MUIGIZAJI MZEE MANENTO AMEFARIKI DUNIA

Habari zilizotufukia hivi punde zinasema kuwa muigizaji Mzee Manento amefariki dunia hapo jana. Bado tunafuatilia kwa karibu habari hizi nz chanzo ch kifo cha mzee wetu huyu.
Mzee Mnento atakumbukwa hasa kwa filamu alizocheza kiumakin na marehemu Kanumba. Hero of the church, Dar to lagos,fake pastor n.k pumzika kwa Amani
Mungu ailaze Roho ya maerehemu mahali pema peponi amina. 

FILAMU MPYA YA RAY AKIWA NA GABO,AMISA MABETO NA WOLPER YAINGIA SOKONI LEO INAITWA V.I.P

 Filamu mpya ya Ray inayoitwa V.I.P (The president's Daughter imeingia sokoni leo ikisambazwa na kampuni kubwa ya steps entertainment
RAY NA WOLPER
 Filamu hiyo inayomuhusu binti ambae ni mtoto wa Raisi imechezwa na mastaa kadhaa akiwemo Gabo,Wolper,Amisa Mabeto na Ray mwenyewe inategemewa kupokelewa vizuru kutokana na aina ya story hiliyopo ndani yake
GABO NA WOLPER



Akielezea kwa kifupi filamu hiyo Ray amesema hivi..........

''Tangu nimezaliwa paka kufika leo, nimekuwa naishi maisha feki, hayakuwa maisha yangu, tangu nimezaliwa nimekuwa naelekezwa kila kitu cha kufanya, mda wa kuamka,mda wa kulala,namna ya kula ili nionekane mstaarabu,nani aina ya rafiki ninayetakiwa kuwa naye na ni nani nisiwe nae,na kuwa hivyo

 ndivyo ustaarabu. Mtu asiye na sifa izo nikimuona sio msataarabu au nikamita majina mbalimbali ka, a mswahili na mengineyo lakini yote hayo nimegundu kuwa ni mawazo ya watu wengine,maisha yangu yote hayo naishi maisha yatakayokuwa na mawazo ya watu wengine,sijapata fursa ya kujua ninachotaka hasa... hii leo ninafurahi kwasababu ninaanza kujijua mimi ni nani na kwa siku izi ninataka niishi mimi Sharon,Sio mtoto wa Rais..''

Tuesday 28 October 2014

KABUTI ONYANGO;WASTARA,NISHA NA SHAMSA FORD NDIO WASANII WAKIKE WANAOLETA CHANGAMOTO KWENYE TASNIA YA FILAMU

 Camera man mwenye jina kubwa kwenye tasnia ya filamu kwa hivi sasa Kabuti Onyango ameshindwa kuficha hisia zake na kuamua kutoa yamoyoni kuhusiana na wacheza filamu wakike wanaosumbua kwenye soko la filamu kwa hivi sasa hapa nchini
 Akifunguka kiafrika bila hofu yoyote amesema kwa hivi sasa kwenye tasnia ya filamu hakuna kama Wastara,Nisha na Shamsha ford na kwamba hao ndio vinala wake.
Amesema Wastara ni msanii anaebadilika kuendana na jamii yake na ukiangalia kwenye filamu ya Gumzo aliyocheza na Nisha ni tofauti kabisa na filamu ya Uaminifu Dhaifu inayosumbua kwa hivi sasa sokoni kwani ameonesha uwezo mkubwa sana
Kabuti pia amesema Salma Nisha ni msanii ambae amaejinyakulia tuzo ya uchekeshaji bora kuoitia tuzo za action and cut na kwamba filamu zake za Gumzo,Tikisa na zena na betina zimemuweka kwenye orodha ya wacheza filamu wakike wanaokubalika kwa hivi sasa hapa bongo.

Kwa upande wa Shamsa Ford yeye ajawai kushuka tangu alipocheza filamu ya Saturday morning ya marehemu Kanumba na nyota yake inazidi kuwa juu siku adi siku,na amekua kivutio kikubwa kwa watu mara baada ya kucheza filamu mpya ya chausiku amabayo amevaa uhusika wa tofauti sanaa

filamu zote hizo zinazowaweka juu wasanii hawa zinasambazwa na kampuni kubwa ya usambazaji nchini stepsentertainment ambayo kwa kiasi kikbwa inasaidia sanaa ya Tanzania kwenda mbali zaidi

CHEKI PROMO YA FILAMU MPYA YA RAY INAYOTOKA ALHAMISI HII

CHEKI PICHA ZA MKALI WA FILAMU YA CHUNGU KIMOJA AUNT EZEKIEL ALIPSHEREKEA BIRTHDAY YAKE







ROSE NDAUKA AMERUDI TENA CHEKI HII INEVITABLE LOVE

HII NDIO 'HARD PRICE' YA RAY CHEKI MWENYEWE HAPA

KAMA ULIPITWA NA INTERVIEW YA NIVA AKIONGELEA FILAMU YAKE NAJUTA MIE HII HAPA

Monday 27 October 2014

ROSE NDAUKA HAKAMATIKI


Acha kabisa! Baada ya kuachana na aliyekuwa mchumba’ke, Malick Bandawe kisha kurudi kwao, Kigogo jijini Dar, staa grade one wa Bongo Movies, Rose Donatus Ndauka anadaiwa hivi sasa hakamatiki hivyo hakauki viwanja.
Rose unaonesha kwamba tangu ametengana na mwanaume huyo amekuwa huru kupita maelezo huku akionesha jeuri ya fedha kama ilivyokuwa kwa mastaa wenzake, Wema Isaac Sepetu na Kajala Masanja.

mara tu baada ya kutoka ‘kifungoni’, Rose aliangusha bonge la sherehe ya ‘bethidei’ yake ndani ya Ukumbi wa Hoteli ya Collosseum, iliyopo Kariakoo jijini Dar na ndiko alikoanza kuonesha jeuri ya fedha.
Rose Ndauka anatarajia kuonekana kwenye filamu mpya ya Inevitable Love mapema mwezi ujao akiwa na wasanii kadhaa wenye majina nchini

KAMA ULIPITWA NA PICHA ZA WASTARA ALIPOTEMBELEA HOSPITAL YA AMANA HIZI HAPA




Mcheza filamu mwenye sifa ya kucheza filamu za kuuzunisha Wastara Juma ametembelea hospital ya Amana na kuwapa msaada wa mama wajawazito

Wastara kwa hivi sasa ametikisa soko la filamu kwa filamu mpya ya Uaminifu Dhaifu ambayo amecheza na Bond Bin Sinnan

HAPPY BIRTHDAY AUNT EZEKIEL MKALI WA FILAMU YA CHUNGU KIMOJA

Mcheza filamu mwenye jina kubwa nchini Aunt Ezekiel anasherekea siku yake ya kuzaliwa leo,kupitia ukurasa wake wa facebook mcheza filamu Batuli ameandika

"Happy Birthday Aunt Ezekiel "Watu Wangu" Tumtakie siku njema super star wetu" #Uzalendo#Kwanza"

Ezekiel kwa sasa anatamba sokoni na filamu mpya ya Mzee Majuto inaitwa Chungu Kimioja ambayo inasambazwa na steps entertainment


RAY NA GABO WAVUJISHANA JASHO KWENYE FILAMU MPYA YA V.I.P

 Wacheza filamu wenye majina makubwa kwa hivi sasa hapa nchini Ray na Gabo wamekutana tena kwenye filamu mpyaa ya Ray inayoitwa V.I.P

Filamu hiyo inayosambazwa na kampuni kubwa ya usambazaji Tanzania Steps entertainment inatoka mwishoni mwa mwezi huu.
.
Filamu hiyo ambayo inamuhusu mtoto wa raisi jinsi alivyokua anaendesha maisha yake tangu amezaliwa yumo pia staa mwingine Jackline Wolper

Gabo na Ray wamewai kucheza filamu nyingine ya Hard Price ambayo bado inafanya vizuri sokoni

SAD MOMENT YA ISIKE SAMWEL IMETOKA LEO

Filamu ya Sad Moment ya mcheza filamu Isike Samweli imetoka leo ikisambazwa na steps entertainment filamu hiyo ambayo amewashilikisha wasanii wenye majina makubwa nchini kama vile Slim Omary inatarajiawa kupokelewa vizuri kutokana na aina ya story iliyomo ndani

"Si kama tu tunajifunza mazuri kupitia mazuri yawengine, bali hata mabaya yawengine yaweza kuwa darasa tosha kwetu SAD MOMENT"Isike amesema

Saturday 25 October 2014

SOMA ALICHOANDIKA NISHA KWENYE UKURASA WAKE WA FACEBOOK

Mcheza filamu za kitanzania Salma Jabu Nisha ambae kwa sasa anashikilia tuzo ya uchekeshaji bora kupitia tuzo za action and cut ameandika hivi kupitia ukurasa wake wa facebook kama njia ya kuaambia mashabiki wa ke malengo yake ya baadae

"Saa nyingine huwa nafikiri,Angeline Jolie huyu hapa,na wakati mwengine nawaza Genevieve Nnaji au Mercy Johnson huyu hapa,ila inshaallah M'Mungu atanifungulia kwa kila ndoto niiotayo leo,na ndio maana kufanya kazi kwa bidii na kuwa mbunifu na kutokuchoka na kuridhika ndo wamekuwa marafiki zangu wakubwa.. "I dont wanna be only a star,I wanna be a succeful woman"

Nisha kwa sasa anasumbua sokoni na filamu yake ya Zena na Betina ambayo inasambazwa na kampuni kubwa ya usambazaji Tanzania steps entertainment

Friday 24 October 2014

WASTARA:FILAMU YA UAMINIFU DHAIFU IMEMRUDISHA MATUMAINI

Mcheza filamu mwenye sifa ya kutendea haki kila kipengele anachocheza Wastara Juma amesema filamu ya Uaminifu Dhaifu ambayo ipo mtaani kwa sasa imemrudisha Matumini kwenye sanaa maana alikuwa kimya mda mrefu.
 Akifunguka kiafika bila hofu yoyote kwa kua Tanzania ni nchi huru Wastara amesema matumaini amecheza kwenye filamu hiyo kama mfanyakazi wandani mwenye vituko sana na ameonesha uwezo mkubwa sana pamoja ya kuwa alikua kimya mda mrefu na watanzania wampokee maana ameitendea haki nafasi yake


Kwenye filamu hiyo ambayo inasukumwa mtaani na kampuni ya stepsentertainment pia yumo mchekeshaji Bambo,mtangazaji na mcheza filamu Bond bin sinna na nsungu,pamija nawengine wengi,

sio ya kukosa kwani inasiku kama mbili tu mtaani kuwa mjanja kwa kupata nakala halisi kutoka stepsentertainment

MSHITUKO VIFO VYA WASANII

Misiba kila kona! Achilia mbali watu wasiokuwa na majina hasa vijana wadogo, ndani ya saa 24 wamefariki dunia wasanii wanne wa kutoka kwenye tasnia za Bongo Movies na Bongo Fleva, Amani lina habari yenye kuumiza moyo.

OKUMU
 HAWA HAPA
Matukio hayo yalitokea kati ya Jumatatu jioni na Jumanne asubuhi ambapo kutoka kwenye tasnia ya filamu waliotangulia mbele ya haki ni pamoja na Sherry Salum ‘Sheri Magali’, Arafa na Benson Okumu Otieno.
Kwa upande wa Bongo Fleva, Yessaya Ambikile ‘YP’, naye alitangulia mbele ya haki ikiwa ni siku chache tu alionekana kwenye kumbi mbalimbali jijini Dar. 
ALIANZA MDOGO TYSON
Jumanne jioni, gazeti hili lilipokea kwa masikitiko kifo cha mdogo wa marehemu George Okumu Otieno ‘Tyson’ aitwaye Benson Okumu Otieno ‘Benii’ ambaye alifariki dunia baada ya kupata homa kali na kuchanganyikiwa.
SHERY MAGARI
 Babari za ndani zilieleza kwamba Benii alianza kuumwa mkono kawaida ambapo alitumia dawa lakini baada ya siku chache mkono huo ulianza kuvimba na kupata homa kali iliyosababisha kwenda hospitali.
Ilielezwa kwamba Benii alikwenda Hospitali ya Lugalo, Dar ambapo homa ile ilipanda kichwani na kumfanya achanganyikiwe, mwisho akaaga dunia.
Baada ya msiba huo kutokea, taratibu za kuusafirisha mwili kwenda kijijini kwao Kisumu nchini Kenya zilifanywa nyumbani kwa mdogo wake wa kike maeneo ya Sinza-White Inn jijini Dar.
Habari zilieleza kwamba Benii alikuwa akifanya kazi za uongozaji wa filamu (director) ambapo alifanikiwa kufanya filamu na wasanii mbalimbali.
Benii alianza kazi hiyo alipofika jijini Dar akiwa anaishi na kaka yake, George Tyson aliyefariki dunia Mei 30, mwaka huu kwa ajali ya gari iliyotokea maeneo ya Gairo mkoani Morogoro.
ARAFA
 “Jamani tatizo ni nini? Hata maumivu ya kifo cha kaka yake hajaisha, jamani na Benii naye? Tumuombe sana Mungu atuepushe na balaa hili la vifo,” alisema mwigizaji mkubwa Bongo, William Mtitu.
ARAFA WA BONGO MUVI AFIA INDIA!
Huku na huku, wakati watu wakitafakari kifo cha Benii na taratibu za kuusafirisha mwili wake, ghafla ziliibuka habari nyingine mbaya kuwa chipukizi wa Bongo Movies aliyetajwa kwa jina moja la Arafa naye aliaga dunia jioni hiyo ya Jumatatu.
Habari zilieleza kwamba Arafa, mtoto mzuri mwenye mvuto huku akiwa na umri chini ya miaka 20, anadaiwa kupelekwa nchini India na mama mmoja kwa shughuli binafsi.Ilielezwa kwamba, akiwa nchini humo aliumwa ghafla (ugonjwa haukutajwa) ndipo akapoteza uhai hivyo taratibu za kuurejesha mwili wake Bongo zinaendelea.
YP
YP NAYE AAGA DUNIA
Msanii YP kutoka Kundi la TMK Wanaume Family, naye aliaga dunia usiku wa kuamkia Jumanne wiki hii.
Habari kutoka kwa familia yake zilieleza kwamba YP alianza kusumbuliwa na kifua tangu mwezi Machi, mwaka huu ambapo alitibiwa na kuanza dozi.
Kwa mujibu wa mkewe, Sakina Robert na dada yake Hawa Ambikile, YP alimaliza dozi mwezi Septemba, mwaka huu ambapo hivi karibuni hali ilibadilika na kuwa mbaya zaidi.Mkewe alisema alikimbizwa katika Hospitali ya Temeke, Dar ambako alipatiwa matibabu hadi umauti.
Meneja wa TMK Wanaume Family, Said Fela alisema msiba wa msanii huyo uliwekwa Keko, Dar nyumbani kwa baba yake na alitarajiwa kuzikwa jana saa 10:00 jioni kwenye Makaburi ya Chang’ombe jijini Dar.
Fela alisema kuwa YP alifanya vizuri kimuziki wakati na msanii mwingine Y Dash ambapo alisikika kwenye ngoma kibao kama Ulipenda Pesa na Pumzika.
MASKINI! ALIPANGA KUACHIA NGOMA MPYA
Ngoma nyingine nyingi alifanya na TMK Wanaume Family kama Twende Zetu ya Chegge Chigunda, Dar Mpaka Moro, Kichwa Kinauma na Tufurahi na tayari alikuwa amerekodi wimbo wake mpya akiwashirikisha Tip Top Connection unaokwenda kwa jina la Wazee wa Jiji aliopanga kuuachia mwezi ujao.
YP ameacha mke na mtoto mmoja wa kike mwenye umri wa miaka saba.
BURIANI SHERRY MAGALI!
Wakati pigo la TMK Wanaume Family likiumiza, majira ya saa 6:00 mchana, siku ya Jumanne iliyopita, ghafla kuliibuka habari nyingine mbaya kwenye Bongo Movies baada ya kuondokewa na mwigizaji ambaye ni mchekeshaji, Sherry Magali.
Sherry Magali aliaga dunia wakati akipatiwa matibabu kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro baada ya kusumbuliwa na maradhi ya kifua na moyo kwa muda mrefu.

NISHA: SIJAFULIA JAMANI

BAADA ya saluni yake iliyopo Sinza jijini Dar kufungwa huku uvumi wa kudaiwa kufulia ukimuandama, msanii wa filamu, Salma Jabu ‘Nisha’ amefunguka kuwa uvumi huo hauna ukweli.

Nisha alisema biashara yake ya saluni ipo kama kawaida ila ameihamishia maeneo ya Chuo Kikuu - Mlimani kwa kuwa eneo la awali halikuwa na nafasi kubwa.
“Sijafulia hata kidogo hayo ni maneno tu yanayozagaa, saluni yangu nimeihamishia Mlimani jamani, nashangaa kweli kwa wanaosema nimefulia,”

Nisha kwasasa anashikilia tuzo ya action and cut kama mchekeshaji bora wa kike uku filamu zake kama tikisa na gumzo zikizidi kufanya vizuri sokoni chini ya kampuni bora kabisa ya usambaziji stepsentertainment

CATHY, KUBADILI JINA KISA LINA MKOSI

MKONGWE wa filamu kitambo, Sabrina Rupia ‘Cathy’ amesema kuwa jina analotumia katika sanaa lina mkosi hivyo yuko kwenye mkakati wa kulibadilisha na kujipa jina lingine labda linaweza kumkaa vizuri.


Cathy amesema anaona jina hilo lina mkosi kwa sababu linazungumzwa vibaya na baadhi ya wasanii wenzake hata kama kuna kitu ambacho hakijui ni lazima lihusishwe jina lake kitu ambacho anakiona kama jina hilo lina nuksi.
“Unajua naona jina hili lina mkosi kwa sababu kitu kifanyika labda mimi nimepita tu basi litatajwa jina langu kitu ambacho mimi sikipendi na kuona labda lina matatizo jamani, haliko sawa kuendelea kuwa nalo,” alisema Cathy huku akidai yuko katika mikakati ya kutafuta jina lingine zuri ambalo anaona linamfaa.

Staa huyo mkongwe ameonesha uwezo mkubwa kwenye filamu kama Big Daddy ya marehemu kanumba na Chausiku ya JB inayofanya vizuri sokoni ikisambazwa na kampuni kubwa ya filamu nchini stepsentertainment

Thursday 23 October 2014

FILAMU YA UAMINIFU DHAIFU YAINGIA MTAANI LEO




Filamu ya Uminifu Dhaifu ya Bond bin sinnan akiwa na Wastara Juma imeingia mtaani leo ikisambazwa na kampuni ya stepsentertainment

Filamu hiyo ambayo imekua ikisubiliwa kwa hamu kubwa kutokana na picha zake wakati wa uandaaji kuvutia wengi imechezwa pia na mchekeshaji Bambo na Matumaini sio yakukosa

‘UKAWA’ YAZALIWA BONGO MOVIE

WASANII wa filamu ambao hivi karibuni waliripotiwa kujitoa katika kundi la Bongo Movie Unity wamedaiwa kuunda la kwao linalojulikana kama Ukawa ambalo litakuwa chini ya uongozi wa Mwenyekiti aliyetimuliwa, Steven Mengere maarufu kama Steve Nyerere.

Baadhi ya wasanii wanaotajwa kuunda kundi hilo kwa mujibu wa chanzo chetu makini ni pamoja na Devotha Mbaga, Salama Salmin ‘Sandra’, Halima Yahya ‘Davina’ na wengineo.
“Yaani sasa hivi haya makundi mawili kuna vita kali sana, kila moja linataka lionekane kwamba lina nguvu kuliko lingine, hata jina la Bongo Movie Unity limebadilishwa sasa hivi linaitwa Bongo Movie Stars

Mussa Issa ‘Cloud’ alikiri kubadilishwa jina kwa Bongo Movie Unity na pia amesikia habari za kuwepo kwa kundi la Ukawa wakati Steve Nyerere alisisitiza kuwa bado ni mwanachama wa Bongo Movie Unity na kwamba mtu anayetaka kuwagombanisha wasanii anajulikana.