Wednesday 25 March 2015

RAY KUWAPA ZAWADI YA PASAKA MASHABIKI WAKE

.Mcheza filamu anaemiliki kampuni ya RJ COMPANY Vicent Kigosi (Ray) anatarajia kuachia filamu yake ya Kichwa cha Kuku tarehe 01.04.2015 kama zawadi ya pasaka kwa mashabiki wake

Ray amesema kwenye filamu hiyo amecheza na waigizaji wengi nyota akiwemo Skyner Ally na Rayuu na filamu hiyo inamafundisho makubwa sana kwa wanawake wanaoishi kwenye ndoa zao akifafanua filmu hiyo anasema "Unajua katika maisha siku zote mwanamke anatakiwa kujiamini na anachokokifanya usidhani kama unafanya ushujaa bali unaonyesha udhaifu ,inawezekanaje ukamuachia mtu aendelee kufaidi raha za mumeo"

Filamu hii inasmbazawa na kampuni ya steps entertainment hivyo naomba mashabiki wangu wanunue DVD original ili kukuza kipato cha wasanii wao watanzania

SKYNER

RAYUU

Tuesday 24 March 2015

HUYU NDIO SABBY ANGEL WASIO RIZIKI




Mcheza  filamu na muombaji wa nyimbo za kizazi kipya Sabby Angel amesema filamu yake yasio riziki ni historia ya kweli kalibu filamu nzima maisha ameyapitia

Amesema muongozaji wa filamu hiyo na alieandika muswaada ni Kulwa kikumba maarufu kama Dude na filamu imechezewa nchini Kenya

Mbali ya Dude pia yumo Tino na Mzee Majuto,hii filamu sio ya kukosa inasmbazwa na steps entertainment kuipata kwa jumla na reja reja wasiliana kwa namba 0713 57 05 81

Monday 23 March 2015

Baba Haji: Kanumba Ameondoka Na Sanaa ya Bongo

Staa wa Bongo Movies, Haji Adamu Rajabu ‘Baba Haji’ amefunguka kuwa, soko la filamu  Bongo kwa sasa linashuka siku hadi siku  na sababu kubwa ni  wasanii kutopenda kwenda shule kujiendeleza kielimu na kujua ni jinsi gani filamu inatakiwa kutengenezwa.
 Baba Haji amesema anakubaliana na kila mtu anayesema soko limeshuka kwa sababu wasanii wanapenda kukopi,  pia hawapendi kuandika miswada ya filamu na kupendelea kuingiza mambo ya kizungu, ingawa wengi wanamtaja msanii Steven  Kanumba kuwa ameondoka na soko hilo.

Baba haji anafunguka kama hivi…
Mwandishi: Vipi, mbona kimya kingi? Soko la filamu limekwenda na Kanumba au unalionaje?
Baba Haji: Tunaweza kusema hivyo, kwa sababu yeye alikuwa anajitoa kwa hali na mali, anatoa pesa zake kwa ajili ya filamu, ni tofauti na wasanii wengine ingawa pia alikuwa akitumia sana ‘media’ kueleza kila anachokifanya.
Mwandishii: Unadhani ni kwa nini wasanii wengi wanapenda kufanya kazi na Wanaigeria?
Baba Haji: Kwa sababu wao wanalipwa tu ila nchi nyingine wana sheria kali, kufanya kwao filamu ni mpaka uwe na digrii ya sanaa.
Mwandishi:  Wewe umejipanga vipi kwa hilo?
Baba Haji: Mimi nimejipanga vizuri kwa sababu nilikwenda Shule Bagamoyo (Pwani) kwa muda wa miaka mitatu na nilifanikiwa kupata diploma ya sanaa, wakati nakwenda shule nakumbuka Kanumba aliniambia napoteza muda kwani soko ndiyo lilikuwa limechanganya ila namshukuru Mungu hata niliporudi sijapotea sana kwa mashabiki.
Swala hili sio mara ya kwanza kusema wasanii na mashabiki kulisema, kwako wewe mdau, unadhani kuna ukweli wowote hapa? mbona alivyokuwepo watu hawakusema kuwa yeye ndio amebeba soko?...

Saturday 14 March 2015

Rammy Kuja na Zakayo Akiwa na Shamsa Ford


Staa wa Bongo Movies, Rammy Galis baada ya kufanya vizuri kupitia filamu yake ya Vocha  anakuja na filamu yake ya Zakayo inayotoka hivi karibuni.
Kwenye filamu hiyo amemshirikisha nyota mwingine wa bongo movie Shamsa Ford,na wengine wengi,filamu hii inauhusu usaliti kwenye mapenzi, hii ni mara ya pili kwa Shamsa Ford na Rammy kufanya kazi pamoja kama utakumbuka wamewai kucheza kwenye filamu ya Chausiku inayosumbua mpaka sasa sokoni.
Wadau na mashabiki kaeni mkao wa kula.

RAY: “VIP haijaigwa popote duniani” Ni baada ya Kashfa iliyompata JB kwenye ‘Mzeee wa Swagga’.

MWIGIZAJI na Muongozaji mahiri wa filamu tokea bongo movie  Vincent Kigosi AKA ‘Ray’ ametangaza dau nono kwa mtu yoyote anayethibitisha kuwa filamu yake ya V.I.P kuwa imeigwa kutoka katika filamu yoyote kutoka nje ya nchi au ndani ya nchi and thet person atayefanya hivyo atampatia milioni moja taslimu.

Ameamua kufanyahivyo baada ya mdau mmoja kuwashutumu wasanii wakubwa kuwa wamekuwa (VILAZA) mabingwa wa kuiga filamu kutoka nje yaani (Copy and paste) wakati wakijadili filamu ya Mzee wa Swaga ya JB iliyoigwa kutoka katika moja ya filamu ya kihindi na kuzua mjadala.

“Hakuna wazo jipya mtu unaweza kufanya na likawa la kipekee, hadithi zinaweza kufanana lakini si hadi dialogue, kuna mtu anadai filamu yangu ya V.I.P nimeiga kutoka sinema ya Ghana, sasa mimi nasema mtu ambaye ana filamu niliyoiga aje nayo ofisini nitampatia milioni moja,”anasema Ray.

Wednesday 11 March 2015

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI KAMPUNI YA STEPS ENTERTAINMENT

Kampuni ya steps entertainment inatangaza nafasi za kazi kwa vijana wa kitanzania umri kuanzia miaka 18 hadi 30.

SIFA ZA MUOBAJI

1.Miaka 18-30
2.Asiwe na historia yoyote ya wizi
3.Awe tayari kufanya kazi muda wowote
4.Elimu kuanzia darasa la Saba

Usaili utafanyika kiwandani maeneo ya kipawa siku ya jumamosi tarehe 14.03.2015 saa mbili asubuhi 

kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kwa simu namba 255 786 351 432 au 0652202316

Monday 9 March 2015

Riyama na Keisha Mzigoni Kupinga Mauaji ya Albino!!

Takribani kwa wiki mzima sasa Staa wa Bongo Movies, Riyama amekuwa akitoa ujumbe mzito akiitaka  jamii kuacha na kupinga mauaji huku akisisitiza upendo kwa ndugu zetu mwenye ulemavu wa ngozi  (Albinos)  kupitia ukurasa wake kwenye mtandao wa Instagram.
Siku ya jana  Riyama alibandika picha hiyo hapo juu akiwa na mwanamziki Keisha ambae ni mlemavu wa ngozi na kuandika kuwa wapo kazini, kitu ambacho mashabiki wake wengi  walijiongeza kuwa Riyama  na Keisha watakuwa Lokeshani wakitengeneza filamu ambayo bila shaka itakuwa ikihusiana na maswala ya kupinga mauaji ya ndungu zetu Albino.
Riyama aliandika
“Kazini Mungu bariki kazi ya mikono yetu...... ..Sambazaupendo tunawazaa sisi ni watoto wetu mamazetu baba zetu rafiki zetu Wao ni kama sisi tuwakumbatie tusiwabague ndugu zetu watanzania wenzetu ….”
Kama ni kweli watakuwa wanatengeneza filamu itakuwa imekaa poa sana. Kwa upande wa Keisha hii itakuwa  sio mara yake ya kwanza kucheza filamu yenye maudhui ya kupinga mauaji ya Albino, kwani hapo nyuma alishawahi kucheza filamu ya aina hiyo.

Friday 6 March 2015

KUWA STAR SIO MPAKA UKAE UCHI KAMA UWEZO HUNA AUNA TU JIPANGE

 Mwanzoni mwa miaka ya tisini ilikua kila nyumba kuna msanii wa kuimba,vipaji vilikua vingi ila kwa sasa waliofata mkumbo wanaonekana na wenye uwezo ndio wanamafanikio kwasasa,kuna baadhi ya watu waliacha shule wakiamini muziki utawalipa lakini zimebaki kuwa stori tu za mjini,sasa na kwenye tasnia ya filamu wamejazana sasa hivi kila nyumba kuna muigizaji kitu ambacho sio kweli kabisa bali wanafata mkumbo wakiamini ipo siku watafanikiwa.
 Dada zetu wengi wanauchu wakutoka na kuwa mastaa wakubwa nchini lakini wengi wao wanaishia kudhalilishwa na kutumiwa kingono bila faida yoyote wanayopata,mfano mzuri ni hizi picha nimekutana nazo facebook zimewekwa na moja ya wataarishaji wa filamu nchini akimnadi huyu dada kuwa ni msanii mzuri sasa hofu yangu ni je huyu mtaarishaji amesomea wapi?na kwanini anatuma picha hizi kwenye mitandao ya kijamii mi binafsi naona ni udahlilishaji na kutojitambua.
 Mwana muziki wa bongo fleva Nay wa mitego amewai kusema kwenye moja ya nyimbo zake kuwa "makahaba wenye viwango wapo bongo movie,bongo movie kama danguro poleni Ray na JB kuonesha ulijali nanyie mnawapitia" wasanii wengi walilalamikia kauli hii lakini je iki cha kupiga picha za uchi na alichokisema Nay kunatofauti gani?Je mastaa wakubwa ndio wanawapotosha chipukizi wanaokuja au chipukizi wanajipotosha wenyewe kwa kuamini kukaa uchi kutawafanya watambulike kwa halaka na kupata mashabiki wengi? ebu soma ujumbe huu wa Madebe Lidai na picha alizoweka kwenye mitandao ya kijamii


Ongea chochote juu ya msanii huyu....!
 — with Warda Salum.
 Tasnia itakufa kwa kudhalilishwa na wachache waliovamia fani kuja kuchafua wenzao,na kuwadhalilisha waonekane hawana maana kabisa kwenye kazi zao za sanaa kumbe ni ujinga wawa chache wasiojielewa ndio wanaalibu
Ushauri wangu kwa dada zangu mnaoingia kwenye filamu,msijidhalilishe kwakupiga picha za uchi ili mjulikane kujulikana sio lazima kupiga picha za uchi ni uwezo wako binafsi pamoja na kujituma tu na sio vinginevyo9

Thursday 5 March 2015

IRENE PAUL:NILIAMINI NIKIZAA NA MUME WA RAFIKI YANGU NITAOKOA NDOA YAKE KUMBE SIVYO NILIVYOFIKILIA MIMI

 Irene Paul ameingiza mtaania filamu yake ya F.R.I.E.N.D.Z  akiwa na wasanii wenzake Mlela na Chuchu Hansi,filamu hiyo inayosambazwa na kampuni kubwa ya steps entertainment inausu familia mbili zilizoshibana sana lakini baadae zinakuja kugombana baada ya usaliti wa mapenzi kuingia kati kati na kuvuruga ndoa zao


Irene Paul amesema kuwa filamu hiyo inamafundisho makubawa kwa mabinti wanaotoa mimba wakiwa mashuleni,kama unaitaka filamu hii wasiliana na 073 570581 sasa

Wednesday 4 March 2015

BAADA YA SERENGETI BOY KUSEMA KAFAIDI PENZI LA WOLPER,HAYA NDIO MAJIBU YA WOLPER KUPITIA INSTAGRAM


wolperstylishEmbu Tusaidiane Waungwana humu insta hapa nashtaki Gazeti au Namshtak huyu mdogo wangu Ambae ata mdogo wangu alienifwata Mimi ni mkubwa kwake na nimrefu pia kwke nisaidieni tuu#maana kwanza ata Famly yangu na Mwanaume wangu akiona ili gazet ni Fedhea na 

Aibu kubwa#sikatai mapenzi Akuna ukubwa wala utoto lkn Mimi binafsi sijapenda kilichoandikwa ktk hili gazet .jamani ungwana uko wapi hapa?? je kijana ulieandikwa hapa naomba uthibitishe ni lini 

umenivua nguo kwamaandishi namatamshi Maana hili stolifumbia Macho nitakufunga nautoamin katika Maisha yako.kikubwa nataka kujua nikwel umeenda kwenye gazet nakuongea nilichokisoma au laah#naningekua najua pakupata namba yako ningekupgia nautamke kwakinywa chako lkn ata hyo 

nguvu yakutafuta namba yako nimekosa#narudia tena nilini umenivua nguo yangu nakujamiana na Mimi jacqueline wolper Massawe mwenye sura hyo hapo labda majina tunafanana naata sura je tunafanana?? ni lini Tumefanya hcho kitendo Bingwa???

Monday 2 March 2015

Wastara Awashukuru Wazee wa Chekecha Cheketua!!

Mrembo na mwigizaji wa filamu, Wastara Juma ambae amefungua biashara ya kuuza  pamba amewashukuru  wanamuziki Ally Kiba na Abdul Kiba kwaku tembelea duka lake na kumuunga mkono. “Yeeeeeeeeah au sijui yioooooo hhhhha kulitaja hili neno linahitaji kipaji mwenye kulitamka ni mwenye kulibuni couz linatokea kooni kwa ubora wa hali ya juu hhhha mwenye kuliweza ni king kebekebe linanikoshaje asante  Ally Kiba na Abdul Kiba kwa kunisaport kwa kununua bidhaa zangu mzee wa chekecha na pita mbele kama umewahi kupenda na kunitendwa asanteni sana- Wastara aliandika. Imekaa poa sana hii, hongera sana Wastara kwa kuwa mjasiliamali .

HEMEDI:Sio kila mwenye macho basi anaona na sio kila mwenye masikio basi anasikia

Kampuni kubwa ya kusambaza filamu ncchini steps entertainment imeingiza filamu ya Hisia potofu sokoni leo baada ya mashabiki kuisubiyo ambayo wamecheza mastaa kama vile Hemed,Jengua na Jack Pantzel inahusu mtu amabae amekua akimuhisi mke wake ana mauhusiano na kijana amabae anamatatizo ya hakili na mwisho wa siku amegundua sivyo alivyokua akidhania ni Hisia potofu tu Kampuni ya steps inatoa filamu nane kwa mwezi na kwa mwezi huu hii ndio filamu yao ya kwanza kwa mawasiliano zaidi wasiliana nao kwa simu namba 0713 570581