Wednesday 28 September 2016


Leo tarehe 28 mwezi wa 9 mcheza filamu grade 1 kutoka bongo movie Wastara Juma amesaini mkataba wa miaka miwili kwenye kampuni ya simu KZG,kupitia ukurasa wake wa
 instagramamesemanimesain rasmi mkataba wa kuwa balozi wa company ya uuzaji wa sim ya china KZG

kuanzia leo mim wastara juma issa nimeanza rasmi kazi ya ubalozi wa KZG itakayoningizia milion 400 kwa mwake

kikubwa ni kunisupot kwa kila hatu naimani ndani ya mafanikio yangu nyuma yake kuna watanzania wenzangu wengi watakao nufaika na kujipatia vibarua kupitia wastara
asanteni kwa ushirikiano kwa wale woootw walihudhuria tukio hili.....

Wednesday 21 September 2016

KALAMBATI LOBO YA JB KUONESHWA SIBUKA MAISHA IJUMAA KABLA YA KUINGIA SOKONI

 Mcheza filamu maarufu Jacob stephen (JB) amefanya mkutano na waandishi wa habari kwa lengo la kutambulisha mfumo mpya wa kuonesha filamu kupitia media ya Sibuka Maisha channel 111 kwenye startimes kabla ya kuingia madukani.
Amesema filamu hiyo inaoneshwa kwa mara ya kwanza Ijumaa tarehe 23 mwezi huu saa 3 usiku na kurudiwa Jumamosi na Jumapili ili kuwapa muda mashabiki zake waweze kuona filamu hiyo
Aidha ameishukuru kampuni ya Steps entertainment kwa kuanzisha mfumo huu mpyaa wa kuonesha filamu kabla hazijaingia sokoni
Filamu hii inatarajia kuingia sokoni Jumatatu 26 mwezi wa 9 nchi nzima,kwa sasa hivi Jb anatamba sokoni na filamu ya chungu cha tatu akiwa na Wema Sepetu na wasanii wengine wengi.

FILAMU YA NANI ZAIDI IMEINGIA SOKONI

FILAMU YA NANI ZAIDI IMEINGIA SOKONI

KAMA UMEPITWA NA KIPINDI CHA STARS AND FANS KIKO HAPA







Mcheza filamu za kitanzania Sonnatah Nduka akiwa kwenye kipindi cha stars and fans kinachorushwa sibuka maisha channel 111 kila ijumaa saa 1 usiku

Friday 2 September 2016

SIBUKA MAISHA WAICHUKUA KESHO YANGU

Filamu ya Kesho yangu leo saa tatu usiku inaingia kwenye histori ya kuwa filamu ya kwanza kutoka kampuni ya usambazaji steps entertainment kuonekana kwenye Sibuka Maisha channel 111 ndani ya startimes kabla ya kuingia sokoni

Filamu hiyo iliyochezwa na waigizaji wenye uwezo mkubwa kutoka Dodoma Sonnatah Nduka,Gosbert Mvungi na wengine wengi itaingia sokoni jumatatu ya wiki ijayo