Tuesday 21 April 2015

SABBY ANGEL:SIO RIZIKI ILIMTAKA MAJUTO

 Mcheza filamu za kitanzania Sabby Angel amesema filamu yake ya Sio Riziki imechukua baadhi ya matukio ambayo yamewai kumtokea kwenye maisha yake

Amesema wakati anajiandaa kufanya filamu hiyo alimtafuta muigizaji Kulwa Kikumba(Dude)na kumuelezea jinsi anavyotaka kufanya filamu hiyo ndio akamuandikia muongozo na kwenda nchini Kenya kwa ajili ya kuandaa filamu hiyo
"Sio Riziki ni filamu ambayo inazungumzia mapenzi kwa ujumla inamzungumzia msichana amabe yeye aliondoka nyumbani kwao na kwenda kutafuta maisha yake mwenyewe,wakati yupo kwenye pulukushani hizo anakutana na wanaume kadhaa ambao anawapenda lakini hawadumu nae kwenye mahusioano na kuona kwamba sio bahati yake ayani sio Riziki"

Stori ya filamu hii ilimtaka Mzee hivyo tukaona sio vibaya kumchukua Mzee Majuto kwenye hii filamu na kiukweli amefanya kitu kikubwa mbali na majutoto yupo pia Tino,Dude na wengine wengi filamu hii inapatikana Tanzania nzima jipatie nakala ayako halisi au wasiliana kwanamba 0716 788 805

Friday 17 April 2015

NIVA"MAPENZI YA KIKUSHINDA ONDOKA"

Wacheza filamu wenye majina makubwa nchini Niva na Chekbud wamektana kwenye filamu ya Hila Haijengi ambayo imeandaliwa na Sulesh Marah kutoka mkoani Dodoma.

Akifunguka kiafrika bila hofu yotote Niva amesema filamu hiyo inaelezea kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi au ndoa utakiwi kuwa na hila kwa mkeo maana haijengi na mapenzi ya kikushinda ondoka

Filamu hiyo inasambazwa na kampuni ya steps intertainment ipo madukani pata nakala yako kuazia sasa

Monday 13 April 2015

KAJALA MASANJA NA HEMED WAKUTANA KWENYE FILAMU YA LOVE AND PAIN

 Kwa mara nyingine tena wasanii wenye uwezo mkubwa wa kuzitendea haki filamu Kajala na Hemed wamekutana kwenye filamu ya Love and pain iliyotoka ijumaa iliyopita kupitia kampuni ya steps entertainment
Filamu hiyo yenye kisa cha mapenzi ieandaliwa na Ivory Bilingwa ambaye ndani ya filamu hiyo ameonesha pia uwezo wake mkubwa wa kucheza na script,jipatie nakala yako halisi sasa kwa jumla na reja reja piga simu namba 0713 57 05 81