Saturday 22 November 2014

HII NDIO FILAMU YA MZEE WA SWAGA YA JB CHEKI NAYO

HUU NDIO WIMBO MPYA WA DIAMOND UCHEKI HAPA

BATULI KUOLEWA SOON

GOOD news kwa mtoto mzuri Bongo Movies, Yobnesh Yusuf ‘Batuli’ ni kwamba anatarajia kuolewa hivi karibuni baada ya kuishi maisha ya upweke kwa muda mrefu, Risasi Jumamosi linakujuza.

Batuli ambaye ni mama wa watoto wawili, amesema kuwa kwa umri alionao, amejifunza vitu vingi katika maisha hivyo kwa kuwa ameshampata mtu sahihi kwake, ameona bora aolewe.
Amesema katika safari ya maisha, vikwazo ni vingi ikiwemo masuala ya skendo za wasanii lakini ameshavuka vikwazo hivyo na hahitaji tena kuyumbishwa na mtu kwani anaingia kwenye ndoa akiwa ameshajifunza mengi.
“Ndoa siyo kitu cha mchezo tena kwa sisi wasanii mambo ni mengi. Kazi yetu tunakutana katika mazingira mbalimbali hatarishi na wadau tofauti, vikwazo ni vingi na mtu akivuka salama basi ni jambo la kumshukuru Mungu,”  

RAY: CHUCHU SASA NDO’ KILA KITU KWANGU

LEGENDARY kwenye anga la sanaa Bongo, Vincent Kigosi ‘Ray’ kwa mara ya kwanza amefunguka kuwa mpenzi wake wa sasa, Chuchu Hans ndiye kila kitu na kilichobaki ni ndoa tu.

Rayamesema licha ya kupitia katika changamoto nyingi za mapenzi lakini kwa Chuchu amefika na haoni tabu kujinadi kwa mtu yeyote juu ya penzi lake hilo.
“Chuchu ndiye kila kitu kwangu, tunaendana kwa kila kitu hivyo nitakaowaudhi kwa kumpenda yeye, wanisamehe,” alisema Ray.Ray kabla ya kuwa na Chuchu, kwa nyakati tofauti alikuwa akitajwa kushea penzi la mwigizaji Ruth Suka ‘Mainda’ na Blandina Chagula ‘Johari’.
Ray kwa hivi sasa anasumbua sokoni na filamu ya V.l.P aliyomshirika Jackline Wolper,Amisa Mobeto pamoja na Gabo

Thursday 20 November 2014

MAJONZI UPYA NDANI YA FILAMU YA LIKWATA,MUONE MAREHEMU ADAMU KUAMBIANA KWA MARA YA MWISHO

FILAMU YA JENEZA LA FEDHA INATOKA WIKI IJAYO SIO YA KUKOSA

SHAMSA STAA ANAEKIMBIZA KWENYE FILAMU YA CHAUSIKU AMESEMA: NITAZAA MPAKA NIAMBIWE BASI

Staa wa Filamu za Kibongo, Shamsa Ford amesema kuwa kutokana na kupenda watoto anaona hawezi kutosheka kuzaa watoto wawili au watatu ila atakachofanya ni kuzaa tu mpaka atakapoambiwa hospitali inatosha.

 Shamsa amesema kuwa tangu alipoanza uhusiano na mchumba wake aitwaye Dick kisha kuzaa naye, walikuwa wamepanga wazae angalau watoto saba ila wapishane kidogo ili waweze kuwalea vizuri.

“Siwezi kutosheka kuzaa watoto wawili au watatu, nitakachofanya nitazaa mpaka basi. Sijali kwamba eti nikizaa nitachuja na kuharibu umbo langu kwani naamini kuwa hata kama nisipozaa bado umri utazidi kwenda na nitakapofikia kuzeeka nitazeeka bila kuwa na watoto,”

Shamsa kwa sasa anasumbua kwenye tasnia ya filamu kwa muvi ya Chausiku ambayo imempa sifa kubwa sana nchini kutokana na kuitendea haki,filamu hiyo inasambazwa na kampuni ya steps entertainment


Saturday 15 November 2014

FILAMU YAVOCHA YA RAMY GALIS IMEVUNJA REKODI YA KANUMBA KWENYE BODI YA FILAMU




Filamu mpya na ya kipee kutoka kwa mcheza filamu Ramy Galis imevunja rekodi kwenye bodi ya filamu Tanzania kwa kupata daraja A

Kupitia ukurasa wake wa facebook Galis ameandika

 Vocha ni Filamu ambayo imepata daraja ya 'A' Kutoka kwenye board ya wakaguzi wa FILAMU Tanzania , Record hio ikiwa ilishikiliwa na Marehm ST.C.Kanumba Nashkuru Mungu na Wewe Pia!

Filamu ya Vocha imechezwa na wasanii kama vile Hemedy,Hamisa Mobeto,Rammy Galis na wasanii wengine wengi inatoka jumatatu usikose nakala yako kwani inasambazwa na kampuni kubwa ya steps entertainment

Friday 14 November 2014

HII NDIO SCENE AMBAYO INAWAPA WAKATI MGUMU MASTAA WETU KUITENDEA HAKI



AUNT, ODAMA WATIMULIWA BONGO MOVIE

UPEPO mbaya unaendelea kuvuma ndani ya Klabu ya Bongo Movie Unity! Safari hii umewakumba mastaa wakubwa klabuni hapo, Devotha Mbaga, Aunt Ezekiel na Jennifer Kyaka ‘Odama’ ambao wanadaiwa kutimuliwa kundini kwa sababu ya kujiweka karibu na mwenyekiti wa klabu hiyo aliyejiuzulu, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’.
 uongozi ambao ulibaki madarakani kundini baada ya Steve kujiuzulu, ulifanya tathmini upya ya memba waliobaki kisha kuwachuja hadi kubaki na wasanii 20 pekee wenye sifa

“Wamewaengua baadhi ya wasanii ambao wameona hawana sifa ya kubaki kundini, miongoni mwao ni Devotha, Aunt na Odama. Wamesema wanahitaji mastaa wenye msimamo siyo kujipendekeza upande wa Steve, siku si nyingi watayaanika majina ya wenye sifa za kubaki kundini,”  

Baada ya habari hiyo walivyotafutwa MASTAA wanadaiwa kutimuliwa  haya ndio wameyasema 

Odama: Hakuna kitu kama hicho, wanaoenguliwa ni viongozi siyo wanachama, watanienguaje bila kunipa taarifa? Kwanza ndiyo nasikia sijui chochote ndiyo napata taarifa kutoka kwako.
Kwa upande wa Aunt Ezekiel, simu yake iliita bila kupokelewa.

HIKI NDIO AMEKISEMA JACK DUSTAN BAADA YA PICHA ZAKE AKIOGA KUVUJA



'Cha ajabu kipi hapo, nilikuwa naoga kwa raha zangu nikamuita mtu akanifotoa, tatizo liko wapi?”

Thursday 13 November 2014

SIRI YA USIA YA WAKUTANISHA ESHABUHETI NA FROLA MVUNGI

 Filamu yenye mvuto wa kusisimua iliyowakutanisha mastaa wenye majina makubwa nchini Esha Buheti na Frola Mvungi wamekutana kwenye filamu ya Siri ya Usia amabyo imetoka leo .

Filamu hiyo inayohusu kijana mwenye tamaa ya mali za urithi ambazo hajui siri ya mali hizo na mwisho anajikuta katika wakati mgumu tamaa nyingi mbele giza

Filamu hii inasambazwa nchi nzima na steps entertainnment pata nakala yako

Tuesday 11 November 2014

KAMA WE NI SHABIKI WA WASTARA JUMA USIKOSE KUTAZAMA INTERVIEW ALIYOFANYA CTN KESHO SAA TATU USIKU







Wastara Juma anashikilia tuzo mbili nazo ni msanii bora wa kike kwa mwaka huu pia anatuzo ya superwoman aliyopata siku ya birthday yake ambapo team wastara walimpa

FILAMU YA SIRI YA USIA KUTOKA ALHAMIS HII

KUWA WAKWANZA KUANGALIA FILAMU MPYA YA RAMY GALIS INAYOITWA VOCHA

RAMY GALIS;MASIKINI HANA THAMANI KWENYE ULIMWENGU WA KIFALME

 Mcheza filamu Ramy Galis anaekuja juu kwa hivi sasa hapa nchini anatarajia kuachia filamu yake mpya ya Vocha mapema jumatatu ijayo,kwenye filamu hiyo amecheza na Hemedy Suleimani pamoja na Hamisa Mobeto na wasanii wengine wengi wenye uwezo mkubwa
Akipiga stori na blog hii Ramy amesema filamu hiyo ni tofauti na filamu zote zinazoandaliwa na wacheza filamu waliowengi kwani mpangilio wa matukio upo tofauti sana

'mimi nimepanga matukio tofauti sana ukiangalia sehemu ya kwanza ya filamu hii na sehemu ya pili kunautofauti sana japo stori ni moja'

Filamu ya Vocha inatarajia kuingia sokoni tarehe 17 mwezi huu na inasambazwa na kampuni kubwa kabisa ya filamu Tanzania Steps Entertainment.

WEMA NA PENNY WAPATANA

WEMA, PENNY WAPATANA
HATIMAYE mastaa wawili wakubwa Bongo, Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu na Mtangazaji wa Redio EFM, Peniel Mungilwa ‘Penny’ wamepatana baada ya kuwa katika bifu kwa kipindi kirefu, chanzo kikiwa ni penzi la Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’.

Habari za ndani zinaeleza kuwa wawili hao walipatanishwa na mdau mkubwa wa burudani, Jennifer Pemba kwenye sherehe ya siku yake ya kuzaliwa iliyofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita katika Ukumbi wa East 24 Bar and Grill uliopo ndani ya Hoteli ya Sea Cliff, Masaki jijini Dar es Salaam ambapo wawili hao walialikwa.

Monday 10 November 2014

ESHE AWANANGA MASTAA BONGO MOVIE

Staa wa filamu za Kibongo,  Eshe Buheti ameibuka na kuwananga mastaa wa kike waliobaki kwenye Kundi la Bongo Movie Unity kuwa hawajielewi na kazi yao ni majungu tu 

Eshe amesema  kuwa imefikia hatua baadhi ya wasanii hao hawasalimiani wanapokutana misibani kisa ni yeye kujitoa kwenye kundi, kituambacho haoni kama kina tija.

“Nawashangaa wasichana wenzangu naona hawajielewi tu ni kama vipofu kwani kwa ilipofikia mwisho tutapigana kwa sababu hata tukikutana misibani wananuna hiki ni kichekesho, mbona wakina Monalisa hawana kundi akina Riyama na wanafanya kazi kama kawaida? Badilikeni”, alisema Eshe pasipo kuwataja majina akidai wanajijua.

FILAMU YA ITIKADI YAIGIA SOKONI LEO

Filamu iliyowashirikisha mastaa wa kubwa kwenye filamu kama vile Tino na Gabo inayokwenda kwa jina la Itikadi imeingia sokoni leo ikisambazwa na kampuni kubwa ya usambazaji Afrika Mashariki Steps entertainment,
Filamu hiyo inahusu Baba mmoja ambae anamlazimisha kijana wake kumuoa msichana asiyempenda,anapokataa anatumia nguvu za giza kutimiza matakwa yake.
 Je nini kinatokea usikose nakala yako halisi kuanzia leo wai madukani 

Friday 7 November 2014

TIKO WA BONGO MOVIE ABONDWA

 STAA wa filamu za Kibongo, Tiko Hassan, hivi karibuni alionja joto ya jiwe baada ya kushushiwa kipigo kizito na hawara wake aliyetajwa kwa jina moja la Ally.
Kwa mujibu wa chanzo makini, siku ya tukio Tiko alikuwa na Ally nyumbani kwake, Mwananyamala ndipo ghafla hali ya hewa ikachafuka baada ya pedeshee mmoja kumpigia simu mwigizaji huyo.
“Mzozo ulianzia kwenye simu na huwezi amini amemvunjia simu yake kwani alimpiga kwa sababu alikuwa akiongea na mwanaume mmoja kimahaba na hapo ndipo timbwili lilipoanza,” kilidai chanzo hicho.
Kikazidi kumwaga ubuyu kwamba, wakati kipigo cha ngumi kikiendelea, mwanaume huyo alimrushia chupa Tiko ambayo ilimpasua usoni na kumuacha na jeraha kubwa lakini hakwenda kumshtaki polisi kwa kuwa anampenda sana.

Thursday 6 November 2014

SOMA ALICHOKIANDIKA WEMA SEPETU INSTAGRAM BAADA YA KUPOSTI PICHA YA MBWA

'Okay... Lets get things straight here.... See dat doggie up there... Y'all see her....? Dat is my bebi.... since i dont have a bebi... Huyo ndo mtoto wng... Basi sasa nitapopost afu nisikie kuzaa nakublock fasta... Mshaniona sizai basi ndo mjue sizai... Akha...!! Zaa zaa... If u have a child im happy for u... Nd wish u da best... I dont... Ndo mungu alivyonipangia... So please hey.... Watakaozaa all da best... Walio na mipango ya kuzaa hongereni... Mimi sina ... Im'

AUNT EZEKIEL;HAKUNA AWEZAYE KUFUMBUA MACHO NA KUTAMBUA MASAA MACHACHE YAJAYO ISIPOKUWA MUNGU PEKEE



 Filamu ya Utamu wangu inayowashirikisha wasanii wenye majina makubwa nchini akiwemo Luckey Luckamo,Neema Ndepanya na Aunt Ezekiel imetoka leo,inasambazwa nchi nzima na kampuni ya steps entertainment
Filamu hiyo iyoongozwa na Luckey Luckamo ni ya kimapenzi inayohusu thamani ya mtu inatakiwa kudhihirishwa bila kungoja kesho kwani binadaamu tumepewa dhamana ya kuijua leo,Hakuna awezaye kufumba macho na kutambua masaa machache yajayo isipokuwa mungu pekee

Wednesday 5 November 2014

MSANII AFA AKITAJA JINA MAINDA

 MSANII aliyefariki dunia hivi karibuni mjini Morogoro, Sherry Magali, anadaiwa kuwa alikuwa akilitaja jina la Ruth Suka ‘Mainda’ kila mara hadi alipofikwa na umauti.
Chanzo chetu makini kilichokuwa karibu na msanii huyo wa filamu, kinasema Sherry alianza kugoma kula akidai hadi amuone msanii mwenzake huyo ambaye alikuwa jijini Dar es Salaam anakoishi.

Mpashaji huyo alisema hata siku aliyofariki pia alilitaja jina hilo, kitendo kilichowaumiza sana baadhi ya ndugu na marafiki. Mainda ambaye alikuwa ni rafiki wa marehemu, alikiri kusikia jambo hilo na anasikitika kwamba siku aliyopanga kwenda, ndiyo ambayo mwenzake alifariki.

RAMMY GALIS MATATANI KUFIKISHWA MAHAKAMANI NOVEMBER 17

Mcheza filamu za kitanzania Rammy Galis ambaye amejizolea umaarufu mkubwa kwenye filamu kama vile Snitch na chausiku anadaiwa kukamatwa uko Arusha na uenda akafikishwa mahakamani november 17 mwaka huu

Akiongea na blog hii mmoja kati ya watu walioshuudia timbwili zima wamesema mcheza filamu huyo amekubwa na soo hilo maeneo ya Njiro mjini humo

Mpaka sasa bado tuanendelea kufatilia sakata hilo na hivi punde tutawajulisha kinachoendelea,

Rammy Galis anatarajia kuachia filamu yake mpya inayokwenda kwa jina la Vocha akiwa na msanii Hemedi na wengine wengi na inasambazwa na steps entertainment usikose nakala yako

HII NDIO HUKUMU YA NDOA YA JB

Tuesday 4 November 2014

HII NDIO CHUNGU KIMOJA YA KING MAJUTO

KAMA UMEPITWA NA JB AKIONGELEA FILAMU YAKE YA MIKONO SALAMA HII HAPA CHEKI

NIVA AMEANZA KUFATA NYAYO ZA MAREHEMU KANUMBA KWENYE FILAMU

 Mcheza filamu za kitanzania Niva Zubery ameonesha kuwavutia mashabiki wake kwa kile anachofanya kwenye filamu zake kwa kuwatumia wasanii wenzake wa kikundi cha Jumba la Dhahabu na kupelekea mashabiki kuvutiwa na kazi zake na kumtabili uenda akariziba pengo la marehemu Kanumba kwani ameonesha nia ya kufata nyayo zake

 Kanumba mara kwa mara kwenye filamu zake alikua anatumia wasanii wenzake kutoka kikundi cha Kaole kitu amabacho anakifanya Niva kwa hivi sasa kwenye filamu zake.

Pia Niva amekua akibadilika kila mara kama alivyokua anafanya Kanumba kwa kucheza uhusika wa sehemu yoyote jambo ambalo linamfanya ajiongezee mashabiki wengi

Ukiangalia filamu yake ambayo inasumbua kwa hivi sasa nchini ya Najuta Mie ambayo amecheza na  Nikita na Mam tei ambao ni zao la tamthilia ya Jumba la Dhahabu utagundua msanii huyu ni miongoni mwa wasanii watakaofika mbali sana endapo akizidi kujituma zaidi na kuwa na heshima kwa mashabiki

Filamu ya Najuta Mie ip madukani Tanzania nzima itafute uone utofauti na uwezo mkubwa alionao mcheza filamu Niva Zubery

Monday 3 November 2014

DIAMOND PLATINUM AMESAPOTI RAY KWENYE FILAMU MPYA YA V.I.P

 Msanii ambae napeperusha vizuri bendera ya taifa letu kwa hivi sasa kupitia mziki wake  Diamond Platinum  ameonesha mapenzi na tasnia ya filamu nchini baada ya hivi karibuni kumsapoti mcheza filamu mwenye jina kubwa nchini Vicent Kigosi (Ray) kwa kuwaomba mashabiki wake kununua filamu  yake mpya ya V.I.P amabayo imetoka mwishoni mwa mwezi ulipita
kupia ukurasa wake kwenye mitandao ya kijamii Diamond ameweka picha ya cover la filamu hiyo na kuandika hivi

'jus another one from #RjCompany , Je Umeshapata Nakala yako....???..Have you got your Copy???... #VIP'

Filamu hiyo inasambazawa na kampuni kubwa ya usambazaji filamu zenye ubora ya steps entertainment inapatikana kwenye maduka na bongo shop zote hapa Tanzania pata nakala yako

FILAMU YA UAMINIFU DHAIFU YAMTESA WASTARA JUMA

 Ikiwa ni siku chache tangu filamu mpya ya Uaminifu Dhaifu kuingia sokoni,imeonekana kumtesa sana mcheza filamu Wastara Juma kwa kua imekua ikimvurugia ratiba zake sana kwani amekua kiirudia kuiangalia kila wakati jambo ambalo linamtesa sana
 Akifunguka kiafrika bila hofu yoyote kwakua Tanzania ni nchi huru amesema filamu hiyo imekua ikimtesa sana kwani amekua akipoteza muda mwingi kuiangalia na hii yote ni kutokana na ubora wa story iliyomo kwenye filamu hiyo

'yani kwenye filamu hii kwanza nimecheza scene ambazo sijawai kuzicheza kwenye maisha yangu ya sanaa na nina shukuru mungu nimeitendea haki sana hivyo inanitesa kila mara kuiangalia yani kuna muda navunja ratiba zangu na kaa naangalia tu nilivyocheza'
 Filamu hiyo amabayo inasambazwa na kampuni yenye jina kubwa Tanzania steps entertainment imewashirikisha wasanii wakubwa akiwemo Bambo,Matumaini,Nsungu,Wastara na bond bi sinnan