Tuesday 11 October 2016

HII NDIO MUNGU NISTILI YA AISHA BUI

 Diva wa filamu nchini Aisha Bui anatarajia kuachia filamu yake ya Mungu Nistili mapema mwezi ujao,filamu hiyo ambayo amewesharikisha wasanii mbali mbali akiwemo Hemed na wasanii wengine wengi,

Hizi ni picha za nyuma ya camera wakati wanaandaa filamu hiyo ya Mungu Nistili






KAJALA MASANJA: UKIWA NA SIFA HIZI NJOO TUZAE

 Malkia wa muziki wa kizazi kipya Kajala Masanja, amesema kwa sasa yupo tayari kuzaa na kuongeza mtoto wa pili wa kiume endapo mwanaume atakuwa na sifa


Mwigizaji huyo ambaye ana mtoto mmoja wa kike aitwaye Paula aliyezaa na prodyuza maarufu Bongo, Paul Matthysse ‘P Funk’, amesema anahitaji Paula apate kaka yake.

“Najua mtoto ni mtoto lakini kwa sasa natamani kuwa na mtoto wa kiume ili Paula naye ajivunie kuwa na kaka. Siku zote nilitamani nipate watoto wenye jinsia tofauti na sasa tayari ninaye wa kike ni zamu ya kumpata mwingine wa kiume,” Kajala aliliambia gazeti la Mtanzania.
Aliongeza, “Natamani kuzaa na mwanaume yeyote aliye tayari na anayejitambua na kuwa tayari kuitwa baba na kugharamia matumizi ya watoto wangu na kuipa familia matunzo bora.”

Kwa upande mwingine, Kajala ameweka wazi kuwa anatamani kuvuka nje ya nchi kimafanikio, jambo ambalo tayari kwa sasa limeanza kuonesha dalili kwa kiasi kikubwa.

Friday 7 October 2016

SIBUKA MAISHA KUIONESHA FILAMU YA KOVU LEO USIKU KABLA YA KUINGIA SOKONI

Filamu ya Kovu inayotarajia kuoneshwa leo saa 3 usiku kupitia Sibuka Maisha channel 111 kwenye king'amuzi cha startimes kabla ya kuingia sokoni

Filamu hiyo inayoingia sokoni mwanzoni mwa wiki ijayo kupitia kampuni ya Steps entertainment imechezwa na wasanii wenye uwezo mkubwa  akiwemo Mzee Majuto na Almasi itaptikana nchi nzima