Tuesday 25 August 2015

TAIYA ODERA:FILAMU YA KICHECHE NI HISTORIA MPYA

 Mcheza filamu za kitanzania anaekuja juu kwa kasi Taiya Odera amesema filamu ya kicheche ni historia mpya kwake kwani ajawai kucheza filamu ya aina hii tangu ameanza kuigiza
 Akiongea na mwandishi wa habari hii amesema filamu hii imempa jina la kicheche kwakua inazungumzia mwanamke ambaye ameolewa,alafu anaishi na shemeji zake lakini mwisho wa siku anatembea na shemeji zake wote wawili,bila kujijua mpaka badae ambapo inakuja kugundulika
 "kicheche ni filamu ambayo nimecheza kama binti ambae sijatulia kwenye ndoa yangu,nilikua nafanya ukicheche,badae mpaka nikaingia kwa wadogo wa mume wangu nikatembea nao wote kwa kuwadanganya vitu kila mmoja kwa nafasi yake bila kujijua na mwisho yanatokea madhala makubwa kwenye familia"
 fFilamu ya kicheche imechezwa na wasanii wengine kama vile Mlela,Isike,Luckey na wengine wengi,imeandikwa na kuongozwa na Leah Mwenda Mseke na inasambazwa na steps intertainment jinsi ya kuipata filamu hii wasiliana kwa namba  0713 570 581 na 0716 788805






Monday 17 August 2015

KAJALA:HII NI LAANA NILIANDIKA GEREZANI


Mcheza filamu mwenye jina kubwa Tanzania Kajala Masanja amesema story ya hii ni Laana ameiandika akiwa Gerezani na alipotoka akaona asichelewe kuwapa mashabiki wake utamu wa filamu hiyo ya kusisimua

Amesema mambo yaliyomo kwenye filamu hiyo ni mambo ambayo vijana wengi wamekua wakitamani kuwa nayo,tena kwa njia ambazo hazimpendezi mwenyezi mungu

"Hii na Laana ni story amabayo nimeandika nikiwa Gerezani na inahusu kijana mmoja ambae alimaliza chuo,na akubahatika kupata kazi,akawa na maisha ya chini sana,lakini alikua anasaidiwa na mpenzi wake,mwisho wa siku anakuja kukutana na rafiki yake waliosoma nae lakini yeye ana maisha mazuri

Ndio anaamua kufata njia alizopita rafiki yake kupata utajili,anaenda kwa mganga na mganga anampa masharti ya kutembea na mama yake,sasa kilichoendelea hapo itafute ikitoka 20.08.2014 ujue zaidi

Kwenye filamu hii Kajala amecheza na Gabo zigamba pamoja na pasta miyamba na wengine wengi inasmbazwa na stepsentertainment