Saturday 28 February 2015

Chozi La Riziki: Shamsa Ford Ndani, Chini ya Jerusalem Film Company


"Kutokana na upendo wake kwangu alithubutu kuniambia kuwa alitamani nizaliwe tumbo moja na yeye ili asiweze kunipoteza katika maisha yake coz tukiishia wapenzi itafika muda tutagombana na tutaachana..But yote yalikuwa ni maneno tu ambayo kila mwanadamu anaweza kutaamka..Siamini kama leo hii nimekua ADUI yake mkubwa.....coming soon hayo maneno utayasikia kwenye bonge la movie CHOZI LA RIZIKI".
Shamsa aliandika maneno hayo mtandaoni akiwa ‘lokesheni’ na kuwashukuru Jerusalem Filim Campany ambayo amekuwa akifanya kazi nayo.
“All in All thank u so much JERUSALEM FILIM COMPANY without u nisingekuwa hapa nilipo...I LOVE MY JOB pls God stand by me”

Thursday 26 February 2015

Zamaradi amchokonoa tena msanii mkubwa wa filamu nchini "JB"



Msanii anayefanya vizuri kunako bongo movie, Jacob Steven maarufu kama JB, hivi karibuni amekwaa scandal mpya ambayo imemshushia HESHIMA kama sio kumpunguzia credit ndani ya tasnia hiyo.

Msanii huyo maarufu amekumbwa na scandal hiyo baada ya muvi yake mpya kutoka inayofahamika kwa jina la MZEE WA SWAGA.

Muvi hiyo inayofanya vizuri sokoni inasadikiwa kukopiwa na ku paste kama ilivyo na moja ya movie maarufu kutoka bollywood inayofahamika kwa jina la "Ladies VS Ricky Bahl".

Akizungumza kupitia kipindi cha take one, Zamaradi Mketema amethibitisha usanii huo uliofanyika na kampuni maarufu ya JERUSALEM inayomilikiwa na JB, Kuwa karibia scene zote zilizochezwa na Filamu ya "mzee wa swaga" imeiga kama ilivyo kuanzia story hadi idadi ya waigizaji wakuu kutoka kwenye filamu hiyo ya kihindi iliyotoka mwaka 2011.

Mtangazaji huyo amelaani vikali utapeli huo uliofanyika na kampuni ya JB huku akijifanya yeye ndiye mtunzi na mwandishi wa story hiyo wakati ukweli anaujua mwenyewe.

Monday 23 February 2015

ODAMA,WASTARA NA HEMED WAKUTANA KWENYE FILAMU YA JADA



Wastaa watatu kutoka bongo movie Wastara,Hemed na Odama wamekutana kwenye filamu ya Jada ambayo inasumbua kwa sasa sokoni

Filamu hiyo ambayo inasambazwa na kampuni ya steps entertainment imeandaliwa na kampuni ya JAY 4LIFE inayomilikiwa na Odama sio ya kukosa pata nakala yako sasa

Wednesday 18 February 2015

NISHA KUWAPA ELIMU YA MAISHA MASHABIKI

 MWIGIZAJI wa filamu nchini, Salma Jabu ‘Nisha’, amesema anatarajia kuachia kazi yake mpya aliyoipa jina la ‘Shida’, ambayo itatoa mafunzo kwa mashabiki kukabiliana na hali yoyote ya maisha.
Akizungumzia filamu hiyo hapo jana, Nisha alisema filamu hiyo inatarajia kuingia sokoni mwishoni mwa mwezi huu, ambapo ameweza kumshirikisha nguli mwingine, Gabo.
"Napenda sana kusikiliza maoni ya mashabiki zangu na kuyafanyia kazi,kwenye filamu ya SHIDA nimewakumbusha Matilda kwa wale walioniomba nitoe serious movie pia sio comedy peke yake.. mimi mwenyewe nililia Ukweli kwa matukio yake, ingawa pia SHIDA itakuburudisha,kukuelelimisha na kukupa ladha halisi ya maisha ya mtanzania ungana nasi Gabo,Nisha,Tunu na wasanii kibao kutoka Zanzibar house of talent,chini uongozi na wapiga picha mashuhuri Tanzania CLEAR PICTURES" .
Amesema mashabiki wategemee mambo mengi mazuri zaidi kutoka kwake, kwani mara nyingi amekuwa akifanya kazi kwa mpangilio ili kuhakikisha anatoa vitu vyenye ubora.
Filamu hii inasmbazwa na kampuni ya steps entertainment kuwa wakwanza kuiona kwa kupiga namba 0788233635 kupata filamu kwa bei poa kabisa

Monday 16 February 2015

NISHA:GABO AMENITELEKEZA KWENYE SHIDA


 Mcheza filamu za kitanzania anaefanya vizuri kila kukicha Salma Jabu Nisha ametelekezwa na msanii mwenzake kwenye filamu ya shida inayotoka mwezi huu mwishoni




Kwenye filamu hiyo Gabo amemtelekeza Nisha akiwa mjamzito,na hii ni mara ya kwanza kwa wawili hao kukutana kwenye filamu hivyo tegemeo kuona kitu kikubwa kutoka kwao inasambazwa na steps entertainment

Saturday 14 February 2015

FILAMU YA KITAZANI KUTOKA JUMATATU

STEVEN KANUMBA PENGO LAKO BADO LIPO

 Alikuwa anajulikana zaidi kama “The great” kama mwenyewe alivyopenda kujiita. Jina lake halisi ni Steven Kanumba. Alikuwa mmoja wa waigizaji wakubwa sana ndani ya tasnia ya bongomovies. Na Katika historia ya tasnia ya filamu nchini Tanzania, Kanumba ndiye aliyekuwa msanii wa kwanza nchini kufanya kazi nje ya nchi na kuweza kuwavuta wageni kutoka nchi mbalimbali kuja kuigiza Tanzania, hasa Wanigeria kama vile Mercy Johnson, Emmanuel France, Nkiru Silvanus, Ramsey Nouah, na wengine wengi. Kanumba pia ameweza kuwaleta waongozaji filamu kadhaa was Kinigeria nchini. Moja ya filamu zilizompa umaarufu sana kimataifa ni pamoja na Devil’s kingdom nyingine kama Dar 2 Lagos na Cross my sin. Alikuwa mmoja wa sanii wenye uwezo mkubwa kifenda na utajiri wako ulikuwa unakadiriwa kuwa zaidi ya shillingi milioni 300 za kitanzania.
Steven Kanumba alizaliwa tarehe 8 mwezi wa Kwanza mwaka 1984 huko shinyanga. Kwa kabila alikuwa ni msukuma. Alipata elimu yake ya awali katika shule ya msingi msingi ya Bugoyi,  na kuendela na masomo ya sekondari huko Mwadui huko huko shinyanga na baadaye kuhamia katika shule ya sekondari ya Dar es salaam Christian Seminary akiwa kidato cha pili ambako alisoma mpaka kidato cha nne na akaendelea na masomo ya kidato cha tano na sita katika shule ya sekondari ya jitegemee iliyopo Dar es salaam.
Kanumba alianza kuigiza toka alipokuwa shule ya msingi kabla ya kujiunga na kikundi cha kaole sanaa group miaka ya tisini. Akiwa kaole kanumba alikutana na walimu wa sanaa toka chuo cha sanaa bagamoyo na vyuo vingine ambako alipata mafunzo zaidi ya uigizaji na baadae alikutana na Dr. Nyoni toka Chuo kikuu cha Dar es Salaam ambako alweza pata mafunzo ya uigizaji kwa muda wa miezi mitatu.

Baada ya hapo kanumba alianza rasmi kuigiza filamu na filamu moja ya filamu zake za kwanza kuigiza zilikuwa sikitiko langu na Johari ambazo zilimpa umaarufu zaidi na kumuwezesha kufanya kazi nyingine mbalimbali ndani na nje ya nchi.
Steven kanumba alikuwa mmoja wa wasanii wa kwanza Tanzania kuweza kutembelea studi za filamu za Universal Studio pamoja na Warner bros zilizopo huko nchini Marekani. Pia kanumba alikuwa mtunzi wa nyimbo na alikuwa na uwezo wa kupiga vifaa vya muziki kama kinanda na gitaa


Steven Kanumba alifariki dunia tarehe saba(7) mwezi wa nne (4) mwaka 2012 baada ya kuanguka chmbani kwake kufuatia ugomvi baina yake na aliyekuwa mpezi wake Elizabeth Michel (LULU). Alifariki muda mfupi baada ya kufikishwa Hospitali ya taifa ya Muhimbili. Mazishi yake yalihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa nchi na umati unaokadiriwa kufikia watu elfu thelathini (30,000).