Wednesday 17 February 2016

MWANAHER YA MWANAHER YAKAMILIKA SOON ITAKUA MTAANI

 Baada ya kufanya vizuri kwenye filamu ya Pumu,mcheza filamu anaekuja juu kwa kasi Mwanaher amemaliza utengenezaji wa filamu ya Mwanaher aliyowashirikisha wa sanii nyota wa filamu nchini

 Akifunguka kiafrika bila hofu yoyote amesema amepania kuteka soko la filamu nchini kwa kufanya kazi nzuri zenye viwango vikubwa sana
amesema filamu hiyo amecheza na wasanii kama vile Stanley nsungu,Riyama Ally,Frola Mvungi na wengine wengi


Thursday 4 February 2016

RAY NA BATULI WATIBUANA CHANZO TAJIRI MFUPI

Mcheza filamu wenye jina kubwa Afrika Mashariki Vicent Kigosi ametupiana maneno kwenye mtandao wa kijamii wa instagram na muigizaji mwenzake Batuli baada ya kutofautina kwenye mkataba wa filamu ya Tajiri mfupi

Batuli anadai amedhrumiwa na Kigosi pesa zake alizocheza kwenye filamu hiyo inayotoka mwishoni mwa mwezi huu

kupitia akaunti yake ya instagram Batuli amepost picha na kuweka ujumbe huu kwa Ray na mashabiki wake

official_batuliactressHaki Ya Mtu Haizami 
Swali: Movie Yako Nimecheza Mwaka Juzi Wiki Moja Kabla Ya Mwezi Mtukufu Wa Ramadhani, Makubaliano Yetu Ya Kazi Kimkataba Ni Siku 10 Tu Lkn Ulienda Kinyume Na Matokeo Yake Nilifanya Kazi Yako Mwezi Mzima Wa Ramadhan Je Ulikuwa Sawa!? Swali: Pamoja Na Usumbufu Wako Wote Nilifanya Kazi Sikufanya!? Kumbuka Nilikuwa Kwenye Swaumu
Swali: Toka Mwaka Juzi Mpaka Mwaka Jana Ni Mm Ndie Niliekuwa Nafuatilia Malipo Yng Ofisini Sio Chini Ya 20 Times Na Umekuwa Ukinikimbia Matokeo Yake Nikachoka Kuja, Simu Zng Umekuwa Ukizipokea Unapotaka Na Sms Unanijibu Unavyotaka Je Mkataba Wetu Ulisema Hivyo!? Swali : Naimani Ww Una Mkataba Upo Ofisini Kwako Upige Picha Tuone Kama Upo Unavyodai, Binafsi Kila Mtu Anajua Nyumba Yng Iliteketea Moto Hivyo Sina Kitu Na Ndio Maana Umekuwa Ukinitendea Unyama Huu Je Kuna Anaeweza Kukaa Kimya Zaidi Ya Mwaka Mmoja Na Hatimae Unaona Kazi Inatoka Wakati Hujalipwa!?
Swali : Ni Movie Ngapi Nilizofanya Kwenye Kampuni Yako Chini Ya Johari!? Ni Zaidi Ya 3 Je Nililalamika!? Kwanini Hii Ambayo Johari Hakuwepo Nikaingia Mkataba Na Ww Iweje Nilalamike!? Dhulma Itakufikisha Pabaya Sana, Tambua Nilifanya Kazi Yako Ktk Mazingira Magumu, Nilikuwa Kwenye Swaumu Baba Nilifuturu Mabarabarani Chipsi Na Vingine Visivyo Rasmi Yote Ni Ktk Kutimiza Kazi Yako, Nionyeshe Mkataba Unaosema Nilipwe Baada Ya Mwaka 1 Na Kuendelea Hakika Umeonyesha Ulivyo Na Roho Ya Dhulma Sijawahi Kulalamika Popote Kuhusu Unachonifanyia Kwa Sbb Nilijua Ipo Siku Utanilipa Changu Matokeo Yake Umeona Ujivishe Ujemedari Lakini Haitokisaidia Chochote, Kama Haki Yng Basi Itanifuata Hata Nikiwa Kaburini....Be Blessed....Allah Bariq


Hata hivyo baada ya muigizaji huyo kufunguka bila hofu na kuonesha kusapotiwa na mashabiki wake muigizaji mwenzie nae amejibu mapigo kwa kuweka ujumbe huu


raythegreatestKATIKA MAISHA YANGU HUWA SIYUMBISHWI WALA SITIKISIKI KWENYE MISIMAMO YANGU NA SIKU ZOTE UKITAKA KUWA MTETEZI MZURI LAZIMA UWEZE KUSIKILIZA PANDE ZOTE MBILI ZA SHILINGI. NINA MIAKA 15 KWENYE TASNIA HII YA FILAMU UKUWAHI KUSIKIA NENO LINALOITWA DHURUMA KUTOKA KWANGU ILA WASWAHILI WANASEMA USILOLIJUA NI SAWA NA USIKU WA GIZA. NASEMA HIVI NIKIKUPA WALAU UTENGENEZE NUSU FILAMU TU NADHANI HAYA MATUSI YOTE MNAYOTUKANA MNGEGEUKA UPANDE WA PILI WA SHILINGI. JINSI WATU WANAVYOSHINDWA KUESHIMU KAZI ZA WATU COZ WAO WANA NJIA NYINGI ZA KUPATA KIPATO AMBAZO HIZO NJIA SISI HATUWEZI ZIFANYA LAZIMA TUFANYE KAZI ILI MKONO UENDE KINYWANI. MTU YOYOTE ANAYECHEZEA MAISHA YAKO MUOGOPE KAMA UKOMA. ISHU YA BATULI IKO KIMKATABA ZAIDI YA YEYE KAMA UPANDE MMOJAWAPO WA KUTEKELEZA MKATABA ANAJUA ILO. UPANDE MMOJA WA MKATABA UNAPOSHINDWA KUTEKELEZA WAJIBU WAKE NJIA ZA KUPITA ZIKO WAZI NA ZINAJULIKANA....INAPOFIKIA MTU BADALA YA KUFUATA NJIA SAHIHI NA AKAAMUA KULETA MJADALA KWENYE SOCIAL MEDIA HAPO KUNA ULAKINI AU AMEAMUA KUJIPA UPOFU WA SHERIA YA MIKATABA NINGEPENDA MUHUSIKA AJIKUMBUSHE ILO NA AFUATE NJIA SAHIHI. KUTUMIA SOCIAL MEDIA HAZITAMSAIDIA ZAIDI YA KULIKUZA JAMBO KWA WATU WASIOJUA UNDANI WAKE.


Filamu hii inatoka mwezi huu mwishoni ikiwa imewashirikisha wasanii kama vile muhogo mchungu,kupa,batuli na ray mwenyewe 

Wednesday 3 February 2016

Erick Omondi Amsapoti Nishabebee Kuuza Filamu ya Kiboko Kabisa

 UNAPOTAJA jina la Erick Omondi ni jina kubwa kwa sasa barani Afrika kijana mdogo mahiri katika uchekeshaji mwenye sifa kubwa Afrika ya Mashariki, msanii huyu ni bingwa wa kutawala jukwaa, alikuja Dar es salaam kwa show maalum na kuamua kumsapoti Nishabebee kuuza filamu ya Kiboko Kabisa.
“Mimi natamba sana na stage but Nisha ni Kiboko kabisa katika kuact filamu na anafuns wengi hata kwa Kenya so naungana naye katika kuhakikisha anauza filamu ya Kiboko kabisa na kuwa Plutnamu mauzo ya juu kabisa,”anasema Eric


Wiki hii msanii huyo katika kumsapoti msanii mwenzake kutoka Swahilihood Nishabebee aliipigia debe filamu hiyo kwa kuwashawishi wapenzi wa filamu wainunue kwa sababu anamjua vizuri Nisha kwa kazi bora na watafurahi bila kujutia pesa zao.
Filamu ya Kiboko kabisa ipo madukani nchi nzima na inapatika katika maduka yote ya filamu Bongo , ni sinema ya kipekee kufanyika Bongo ikiwashirikisha wasanii kama King Majuto, Mzee Jengua, Ben Blanko, Nishabebee na wasanii wengine wakali katika tasnia ya filamu Bongo.