Monday 23 November 2015

KAJALA MASANJA"NAPENDA SANA KUCHEZA FILAMU,NDIO MAISHA YANGU

 Mcheza filamu mwenye jina kubwa Tanzania kwa uwezo wake wa kuigiza Kajala Masanja amesema anapenda sana kucheza filamu kwani ni moja ya vitu anavyovipenda sana kwenye maisha yake,

amesema tangu akiwa na umri mdogo amekua akipenda nakutamani kucheza filamu mara nyingi sana jambo ambalo akilifanya anajisikia faraja zaidi.
 "mimi napenda sana kucheza filamu yani sana natamani ata kwa mwaka nicheze filamu tano,yani filamu ni sehemu ya maisha yangu"
 Kajala Masanja amecheza filamu nyingi za zimependwa na watu wa lika zote,na kwa sasa anatamba sokoni na filamu ya hii ni laana aliyocheza na Gabo Zigamba
Mbali na filamu hiyo pia Kajala amecheza filamu kama vile Pishu na wake up ambazo pia zinafanya vizuri sokoni

JB NA WEMA WAKUTANA TENA KWENYE FILAMU YA CHUNGU CHA TATU

Mcheza filamu mwenye jina kubwa Tanzania Wema Sepetu anatarajia kukutana tena na mkongwe wa fani hiyo Jacob Steven kwenye filamu ya chungu cha tatu

Filamu hiyo ambayo ina husu mwanadada Doreen (wema sepetu) an aingia kwenye mahusiano na wanaume wa tatu tofauti kwa kile anachoamini kuwa atapata mtoto na badala yake kupambana na visa na mikasa ya kusisimua

Kwenye filamu hiyo inayotoka mwezi ujao wamo pia Patcho,Mwamba,Mau na wengine wengi inatarajiwa kuasmbazwa na steps entertainment kwa jumla na reja reja wasiliana nao kwa namba 0713 570 581 au 0716 788 805

FILAMU YA FIGISU FIGISU INATOKA MWISHONI MWA MWEZI HUU

KUTANA NA MUANDISHI ALIETEKWA NA KUTOROKA NDANI YA WHO"S BACK

Monday 12 October 2015

LUCY KOMA AMERUDI NA "TANZANIA TO DENMARK AKIWA NA SLIM OMARY

 Muigizaji mkongwe kwenye tasnia ya filamu Lucy Komba amabae anapiga mziko nchini Denmark amerudi na filamu ya 'From Tanzania to Denmark akiwa na Slim Omary  na wenginie wengi kutoka nchini humo


Filamu hiyo inayomuhusu binti ambae alikenda Denmark na kukutana na misuko suko mingi kabla ajakutana na mpenzi wake na kuanza kuishi pamoja inasambazwa na kampuni ya steps entertainment pata nakala yako sasa

AUNT EKIEL:NAFANYA CHOCHOTE KUKIDHI MAITAJI YANGU,NITAWAFURAISHA

 Filamu ya Mwajuma nipe ya Aunt Ezekiel imeingia mtaani leo ikisambazwa na steps entertainment,filamu hiyo ambayo amewashirikisha Mzee majuto,Stanley Nsungu na wengine wengi inaelezea jinsi msichana Mwajuma anavyoweza kujutolea chochote alicho nacho kukidhi mahitaji yake

Aint Ezekiel anasema 'Nafanya chochote ili  kukidhi mahitaji yangu,ni mazoea ya jamii yetu kudharau na kutowathamin wanawake,lakin si mimi Mwajuma nipe ni zaidi ya mwanamke chungu na tamu naifahamu lazima nitawafuraaisha kwa gharama yoyote ile"




Saturday 10 October 2015

Ester Kiama avamiwa, apewa kichapo ajeruhiwa!

Staa wa Filamu za Kibongo, Ester Kiama juzikati alijikuta kwenye wakati mgumu baada ya kuvamiwa na vibaka na kuchezea kichapo kisha kuibiwa pesa na simu mbili.

Sosi aliye karibu na staa huyo aliyeomba hifadhi ya jina lake alidai kuwa, siku ya tukio Ester alitoka viwanja na wenzake, walipofika Kijitonyama jijini Dar yeye akiwa anaendesha gari, aliwashusha wenzake lakini wakati anarudi kwenye gari ili aondoke, wakatokea vijana wawili na pikipiki wakamfanyizia.


Ijumaa lilipopata taarifa hizo lilitinga nyumbani kwa Ester na kumkuta akiwa hoi sambamba na majeraha, alipotakiwa kueleza kilichompata alikiri kufanyiwa unyama huo ambapo alisema anajuta kutembea usiku bila kuwa na mwanaume.


Monday 5 October 2015

IVONY BIRINGWA STAA WA FILAMU YA HEART ATTACK AKIWA KWENYE UBORA WAKE




ESTER KIAMA:MUHANGA INA MAFUNZO MAKUBWA KWENYE NDOA

Staa wa filamu za kibongo nchini Ester Kiama amesema filamu ya Muhanga ina mafunzo makubwa kwenye ndoa,kwa kua stori yake inalenga maisha halisi ya matatizo wanayokutana nayo wanandoa,wengi wanaotafuta mtoto
 Ester amesema filamu hiyo inahusu wanandoa waliokaa mda mrefu bila kupata mtoto,mpaka mama mkwe akawa anamsumbua mtoto wake wa kiume jambo lililopelekea mtoto huyo kujitoa Muhanga

Anasema kwenye filamu hiyo ambayo ameshiriki na Issa Mussa cloud,Suleiman Barafu,pamoja na Luckness Mokiwa yeye amacheza kama mwanamke ambae ameamua kuzaa na mume wa mtu kwa makubaliano maalum ili kuioka ndoa ya mwanaume huyo
"kwenye filamu hiyo mm ndio mwanamke ambae Cloud alinifata nimzalie mtoto baada ya mkewe kuonekana hawezi kuzaa kabisa,hivyo akajitoa muhanga kuja kwangu kwa makubaliano maalum zaid nunu filamu hii ujifunze mambo mengi "

filamu hiyo ipo madukani kote Tanzania inasmbazwa ns steps entertainment

Friday 2 October 2015

THE SCAR YA MKUTANISHA RIYAMA NA RADO

Filamu ya the scar imetoka leo ikiwa imechezwa na mastaa kama Rado na Riyama,na wengine wengi,filamu hii inasmbazwa na steps entertainment sio ya kukosa,pata nakala yako sasa

Monday 28 September 2015

FILAMU YA MAMA LISHE YAINGIA MTAANI LEO

Filamu ya Mama Lishe imeingia mtaani leo ikisambazwa na steps entertainment,filamu hiyo imechezwa na Halima Yahaya maarufu kama Davina akiwa na Issa Mussa Clouds,Swebe na wasanii wengine wengi.

Akifunguka kiafrika bila hofu yoyote kwakua Tanzania ni nchi huru Davina amesema filamu hiyo inamafundisho makubwa sana kwenye ndoa ikiwa ni pamoja na kutomuamini rafiki yako wa karibu na madhara ya kufanya ngono zembe yanavyoalibu kizazi cha sasa na familia kwa ujumla

Davina anasema kwenye filamu hii amecheza kama mama lishe mwenye familia,nakuonesha changamoto wanazopata kina mama lishe kwa waume zao

filamu hii ipo madukani kuanzia sasa pata nakala yako halisi sasa

Wednesday 23 September 2015

HEMED AMPOKEA WASTARA KWA MIKONO MIWILI

Mcheza filamu wenye jina kubwa nchini Hemed Suleiman  ameonesha uhodari wa ali ya juu kwa kumpokea muigizaji mwenzie Wastara Juma kwa mikono miwili

Hemed ameya fanya hayo kwenye filamu ya Mama na Mwana baada ya kuamua kubeba shida zote za Wastara na mtoto wake na kumuacha Yusuph Mlela akiwa njia panda asijue pakwenda

Filamu ya Mama na mwana iliyoandikwa na kuongozwa na Leah Mwenda Mseke inatoa mafunzo kwenye ndoa jinsi ya kuishi na mtoto mlemavu,na kuonesha yeye ana haki

Akiongea na muandishi wa habari hii Wastara amesema kumekua na kawaida ya familia kuwatenga watoto wenye ulemavu na kuona kwamba hawana thamani ya kuishi kitu ambacho sio sawa,ndio maana alipambiwa acheze filamu hiyo hakusita

"niliongea na Lmata akaniambai kuna story anacheza Mlela,lakini stoey hiyo inakutaka wewe hivyo naomba ushiriki kwenye kucheza tutao kitu kizuri sana"

filamu hiyo ipo mtaani na inasambazwa na kampuni ya steps entertainment kwa mawsiliano zaidi jinsi ya kupata filamu hii na filamu zote za steps wasiliana nao kwa namba 0764 547 381,0713 570 581 au 0716 78 88 05

Tuesday 22 September 2015

CLOUD 112 AMERUDI NA MUHANGA

Baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu atimae mcheza filamu mkongwe Tanzania Issa Mussa maarufu kama Cloud 112 amerudi kwa kasi na filamu ya Muhanga akiwa na Barafu pamoja na Luckess Mokiwa

Filamu hiyo inayosukumwa mtaani na kampuni ya Steps entertainment inamuelezea mwanamke ambae ameolewa lakini ndoa yake inaingia dosari baada ya kukaa muda mrefu bila kubeba ujauzito

Atimae anashauriana na rafiki yake watafute mwanamke ambae ata beba ujauzito na mwisho wa siku mtoto akizaliwa amchukue kisili bila mama yake kujua

Tuesday 25 August 2015

TAIYA ODERA:FILAMU YA KICHECHE NI HISTORIA MPYA

 Mcheza filamu za kitanzania anaekuja juu kwa kasi Taiya Odera amesema filamu ya kicheche ni historia mpya kwake kwani ajawai kucheza filamu ya aina hii tangu ameanza kuigiza
 Akiongea na mwandishi wa habari hii amesema filamu hii imempa jina la kicheche kwakua inazungumzia mwanamke ambaye ameolewa,alafu anaishi na shemeji zake lakini mwisho wa siku anatembea na shemeji zake wote wawili,bila kujijua mpaka badae ambapo inakuja kugundulika
 "kicheche ni filamu ambayo nimecheza kama binti ambae sijatulia kwenye ndoa yangu,nilikua nafanya ukicheche,badae mpaka nikaingia kwa wadogo wa mume wangu nikatembea nao wote kwa kuwadanganya vitu kila mmoja kwa nafasi yake bila kujijua na mwisho yanatokea madhala makubwa kwenye familia"
 fFilamu ya kicheche imechezwa na wasanii wengine kama vile Mlela,Isike,Luckey na wengine wengi,imeandikwa na kuongozwa na Leah Mwenda Mseke na inasambazwa na steps intertainment jinsi ya kuipata filamu hii wasiliana kwa namba  0713 570 581 na 0716 788805






Monday 17 August 2015

KAJALA:HII NI LAANA NILIANDIKA GEREZANI


Mcheza filamu mwenye jina kubwa Tanzania Kajala Masanja amesema story ya hii ni Laana ameiandika akiwa Gerezani na alipotoka akaona asichelewe kuwapa mashabiki wake utamu wa filamu hiyo ya kusisimua

Amesema mambo yaliyomo kwenye filamu hiyo ni mambo ambayo vijana wengi wamekua wakitamani kuwa nayo,tena kwa njia ambazo hazimpendezi mwenyezi mungu

"Hii na Laana ni story amabayo nimeandika nikiwa Gerezani na inahusu kijana mmoja ambae alimaliza chuo,na akubahatika kupata kazi,akawa na maisha ya chini sana,lakini alikua anasaidiwa na mpenzi wake,mwisho wa siku anakuja kukutana na rafiki yake waliosoma nae lakini yeye ana maisha mazuri

Ndio anaamua kufata njia alizopita rafiki yake kupata utajili,anaenda kwa mganga na mganga anampa masharti ya kutembea na mama yake,sasa kilichoendelea hapo itafute ikitoka 20.08.2014 ujue zaidi

Kwenye filamu hii Kajala amecheza na Gabo zigamba pamoja na pasta miyamba na wengine wengi inasmbazwa na stepsentertainment









Monday 27 July 2015

KAJALA,WOLPER NA IRENE UWOYA WAKUTANA KWENYE FILAMU YA WAKE UP

 Kwa mara ya kwanza tangu Tanzania imeanza,muandaaji wa filamu Manaiki Sanga anawakutanisha mastaa wa filamu na muziki zaidi ya 30 na kucheza filamu kubwa Africa Mashariki "WAKE UP"
 Filamu hiyo ambayo imeandikwa na kuongozwa na muandishi mwenye jina kubwa bongo Leah Mwenda Mseke ni miongoni mwa filamu bora zitakazowaacha watu vinywa wazi kwa namna ilivyochezwa kwa kiwango cha juu sanaaa
 Amesema ikitoka watu wanunue waone jinsi ili mastaa hao walivyocheza kwa kiwango kikubwa watoto wa mjini wanasema wakiwa kwenye ubora wao
 Filamu hiyo inatoka mwisho wa mwezi huu na itafanyiwa uzinduzi wa kihistoria hivyo mashabiki mnaombwa mkae tayari



Saturday 4 July 2015

MLELA:MAMA NA MWANA NI FUNZO KWA JAMII INYOWATENGA WATOTO WENYE UTINDIO WA UBONGO

 Zikiwa zimebaki siku chache filamu mpya ya mcheza filamu Yusuph Mlela inayokwenda kwa jina la Mama na Mwana kuingia sokoni,Mlela amesema filamu hiyo ni funzo kwa jamii ya kitanzania inayowatenga watoto wenye utindio wa ubongo.
Mlela amesema filamu hiyo inatoa picha halisi ya mateso na maumivu yanayompata mama anaezaa mtoto mwenye utindio wa ubongo

"filamu ya mama na mwana inahusu mama aliezaa mtoto mwenye utindioa wa ubongo anavyopata shida kwenye ndoa yake baada mume kumguka na kumpa maneno makali<
kwenye filamu hiyo ambayo inasambazwa na steps entertainment Mlela amewashirikisha wasanii wengi akiwemo Wastara na Hemed,sio ya kukosa ikitoka

Thursday 11 June 2015

SHAMSA FORD NA RAMMY GALIS WATIBUANA KISA KIKO HAPA

 Wacheza filamu wanaofanya vizuri kwenye tasnia ya filamu kwa hivi sasa Shamsa Ford na Rammy Galis wametibuana baada ya Rammy Galis kuonesha mapenzi ya dhati kwa mwanamke mwingine bila kujali kuwa Shamsa anamsaidia kwa kiasi gani
 Kitendo hicho kimefanya mpaka mdogo wake Rammy anaeitwa Kareem kujisikia vibaya kutokana na kaka yake kumsaliti Shamsa Ford
Baada ya Rammy kutafutwa kwenye simu yake kujibu mashitaka haya simu yake haikupokelewa na shamsa hakupatikana kabisa hewani

Tuesday 26 May 2015

SALMA JABU NISHA KUJA NA MTAA KWA MTAA MWISHO WA NWEZI HUU

 Mcheza filamu anejizolea umaarufu kwenye uchekeshaji Salma Nisha nakuja na filamu ya mtaa kwa mtaa mwisho wa mwezi huu
Kwenye filamu hiyo wamo pia Hemedy,Tausi,Diana Kimaro pamoja na Asha Boko na wengine wengi
 Filamu hiyo anazungumzia  maisha ya traffick feki ambae anatumia nguo za jeshi la polisi vibaya na mwisho wa siku anajikuta kwenye matatizo makubwa
 Filamu hiyo inasambazwa na steps entertainment limited itaingia mtaani mwisho wa mwezi huu


ODAMA KUJA NA BIG SUPRISE MWEZI UJAO

 Mcheza filamu anaesumbua sana bongo kwa hivi sasa Jennifer Kyaka jina la kumuingizia kipato Odama anakuja na filamu ya Big suprise akiwa na na Salim Ahmed jina maarufu Gabo pamoja na mastaa wengine wengi
 Filamu hiyo inayosambazwa na kampuni ya steps entertainment imewashirikisha pia wasanii wengine kama vile Kupa,Pastor Miyamba,Jengua pamoja na Mutrah itakuwa sokoni mwezi ujao
 Filamu hiyo inaelezea kisa cha mwanamke aliekuwa kwenye ndoa lakini akawa anachepuka na vijana wadogo mwisho wa siku mume wake anamfumania na kuamua kumpa adhabu inayompa wakati mgumu sana
Mutraha na Odama


Gabo

Odama na Gabo

Kupa na Gabo

Odama