Tuesday 20 December 2016

Gabo: Mtindo wa Maisha Yangu ni Tofauti na Wenzangu

Msanii Gabo Zigamba ameweka wazi kuwa hana tofauti na wasanii wenzake kama ambavyo imekuwa ikilalamikiwa na wengi kuwa msanii huyo haelewani na wenzake.

Akizungumza na East Africa Television, Gabo amesema kinachomfanya aonekane ana tofauti na wasanii wenzake ni utoafuti wa mtindo wa maisha alionao, lakini hana tatizo nao na anawapenda kwa dhati.
“Hakuna msanii ambaye sielewani naye, sema lifestyle yangu mimi ndiyo haifanani na wao, lakini naelewana na wasanii wote nawapenda wananipenda, mimi nawapenda kwa dhati ya moyo, sijui wao kama wananipenda kwa nafsi ya uso, ila sina kikwaruzo, sina ugomvi, ila utofauti unapoonekana unaweza mtu ukakunja kwa sababu ndiyo tatizo la watanzania, ila mimi niko sawa nao labda wao wasiwe sawa na mimi”, alisema Gabo.
Gabo aliendelea kusema kwamba tofauti kubwa iliyopo kwake na wasanii wenzake ni matarajio yake ya kufanya utofauti kwenye tasnia ya filamu hapa nchini.
“Unajua kila mmoja ana nafasi yake kwa mashabiki wake, siwezi nikasema najiona tofauti na wao, ila naweza kusema natarajia kufanya vitu tofauti na wao walivyovifanya”, alisema Gabo.

KUMBE MIMBA YA NISHA ILIKUWA KIKI TU

 Wiki kadhaa zimepita tangu muigizaji  Salma Jabu nisha kuweka picha mtandaoni akiwa mja mzito na kusema ujauzito huo umetokana na kubakwa na aliyekua mpenzi wake ambae ata hivyo hajamuweka wazi
 Akifunguka kiafrika bila hofu yoyote kwa kua Tanzania ni nchi huru amesema yeye sio mjamzito ila amesema hivyo ili kuona mtu mwenye ujauzito uliotokana na kubakwa jamii inampokeaje anapoweka wazi swala lake
 "mimi sina ujauzito ata ile picha yangu ya kwanza kuweka mtandaoni na kujitangaza ni mimi,sikua mimi ile ni picha ya mdada wa Nigeria nimeitumia tu"
Amesema kwa yupo kwenye maandalizi ya filamu yake mpya amabayo imelenga mambo ya mimba za utotoni na ataifanya vizuri kwakua ameshapitia kipindi cha ujauzito wa mtu aliyebakwa na kutelekezwa


kwa sasa Nisha anatamba na filamu ya Kiboko kabisa akiwa na mkongwe wa tasnia hii King Majuto,inasongezwa mtaani na kampuni ya steps entertainment.

Tuesday 13 December 2016

FILAMU YA SIRI YA MOYO SASA INAPATIKANA KWENYE AFROBOX

 Filamu kutoka kwa muigizaji anaekuja juu kwa kasi nchini Man Fizo imeanza kuoneshwa kwenye application ya Afrobox inayopatikana kwenye play store kwa wale wenye simu za android na app store kwa wenye simu za apple
 Wasanii wengine ambao wameonesha uwezo mkubwa kwenye filamu hiyo ni pamoja na Mwanaher,Kupa pamoja na Mzee majuto wakiwa sambamba na msanii chipukizi kabisa kwenye tasnia Careen Jonas
Mbali na kuoneshwa kwenye Afrobox filam hiyo inasambazwa na kampuni ya steps entertainment kwa mfumo wa DvD nchi nzima,usikose nakala yako halisi

Saturday 3 December 2016

UZINDUZI WA SIRI YA MOYO WATIKISA DAR ES SALAAM

wasanii wa filamu ya siri ya moyo wakiwa na waandaji wa uzinduzi wa filamu hiyo



Mcheza filamu Rammy Galis


Msanii fizo



Uzinduzi wa filamu ya Siri ya moyo umefanyika kwenye ukumbi wa sinema Suncrest ulipo ndani ya jumba la biashara,Quality centre na kuudhuriwa na mamia ya mashabiki wa filamu nchini

Akifunguka kiafrika bila hofu yoyote muandaaji na muhusika mkuu wa filamu hiyo Salum Salehe(man fizo) amesema filamu hiyo ameitengeneza visiwani Zanzibar na imeghalimu dora 13799.45 sawa na zaidi ya milioni 30 kwa madafu ya kibongo

Aidha amesema wahusika wote wameonesha uwezo mkubwa kwenye nafasi zao jambo lilifanyanya muongozaji asipate shida sana kuwaongoaza

"kwenye filamu hii wahusika ni mimi mwenyewe,Mwanaheri,Careen,Deus,Kupa pamoja na Mzee Majuto,ni hadithi ambayo kila mtu ataipenda itakapo kuwa madukani msikose"

Filamu ya siri ya moyo inatarajia kuingia sokoni tarehe 12 mwezi wa 12 mwaka 2016 na inasambazwa na kampuni ya Steps entertainment.

Friday 11 November 2016

MUNGU NISTILI YA AISHA BUI KUONESHWA LEO SIBUKA MAISHA

 Filamu ya Mungu Nistili kutoka kwa mcheza filamu Aisha Bui itaoneshwa leo kupitia Sibuka maisha channel 111 kwenye startimes
Filamu hiyo ambayo imesheni masta kibao aliwemo Baba Haji,Hemed, Aisha na wengine wengi itaingia sokoni Jumatatu ya wiki ijayo ikisambazwa na kampuni ya steps enyertainment

CHEKI PICHA ZA VIDEO QUEEN WA KWENYE COVER YA WIMBO WA NISAMEHE ILIYO FANYWA NA STAN BAKORA




Wednesday 2 November 2016

MUNGU NISTILI YA AISHA BUI KUTOKA MWEZI HUU







Filamu ya Mungu nistili kutoka kwa Aisha Bui inatarajia kutoka mwezi huu wa 11,usikose nakala yako

Tuesday 11 October 2016

HII NDIO MUNGU NISTILI YA AISHA BUI

 Diva wa filamu nchini Aisha Bui anatarajia kuachia filamu yake ya Mungu Nistili mapema mwezi ujao,filamu hiyo ambayo amewesharikisha wasanii mbali mbali akiwemo Hemed na wasanii wengine wengi,

Hizi ni picha za nyuma ya camera wakati wanaandaa filamu hiyo ya Mungu Nistili






KAJALA MASANJA: UKIWA NA SIFA HIZI NJOO TUZAE

 Malkia wa muziki wa kizazi kipya Kajala Masanja, amesema kwa sasa yupo tayari kuzaa na kuongeza mtoto wa pili wa kiume endapo mwanaume atakuwa na sifa


Mwigizaji huyo ambaye ana mtoto mmoja wa kike aitwaye Paula aliyezaa na prodyuza maarufu Bongo, Paul Matthysse ‘P Funk’, amesema anahitaji Paula apate kaka yake.

“Najua mtoto ni mtoto lakini kwa sasa natamani kuwa na mtoto wa kiume ili Paula naye ajivunie kuwa na kaka. Siku zote nilitamani nipate watoto wenye jinsia tofauti na sasa tayari ninaye wa kike ni zamu ya kumpata mwingine wa kiume,” Kajala aliliambia gazeti la Mtanzania.
Aliongeza, “Natamani kuzaa na mwanaume yeyote aliye tayari na anayejitambua na kuwa tayari kuitwa baba na kugharamia matumizi ya watoto wangu na kuipa familia matunzo bora.”

Kwa upande mwingine, Kajala ameweka wazi kuwa anatamani kuvuka nje ya nchi kimafanikio, jambo ambalo tayari kwa sasa limeanza kuonesha dalili kwa kiasi kikubwa.

Friday 7 October 2016

SIBUKA MAISHA KUIONESHA FILAMU YA KOVU LEO USIKU KABLA YA KUINGIA SOKONI

Filamu ya Kovu inayotarajia kuoneshwa leo saa 3 usiku kupitia Sibuka Maisha channel 111 kwenye king'amuzi cha startimes kabla ya kuingia sokoni

Filamu hiyo inayoingia sokoni mwanzoni mwa wiki ijayo kupitia kampuni ya Steps entertainment imechezwa na wasanii wenye uwezo mkubwa  akiwemo Mzee Majuto na Almasi itaptikana nchi nzima

Wednesday 28 September 2016


Leo tarehe 28 mwezi wa 9 mcheza filamu grade 1 kutoka bongo movie Wastara Juma amesaini mkataba wa miaka miwili kwenye kampuni ya simu KZG,kupitia ukurasa wake wa
 instagramamesemanimesain rasmi mkataba wa kuwa balozi wa company ya uuzaji wa sim ya china KZG

kuanzia leo mim wastara juma issa nimeanza rasmi kazi ya ubalozi wa KZG itakayoningizia milion 400 kwa mwake

kikubwa ni kunisupot kwa kila hatu naimani ndani ya mafanikio yangu nyuma yake kuna watanzania wenzangu wengi watakao nufaika na kujipatia vibarua kupitia wastara
asanteni kwa ushirikiano kwa wale woootw walihudhuria tukio hili.....

Wednesday 21 September 2016

KALAMBATI LOBO YA JB KUONESHWA SIBUKA MAISHA IJUMAA KABLA YA KUINGIA SOKONI

 Mcheza filamu maarufu Jacob stephen (JB) amefanya mkutano na waandishi wa habari kwa lengo la kutambulisha mfumo mpya wa kuonesha filamu kupitia media ya Sibuka Maisha channel 111 kwenye startimes kabla ya kuingia madukani.
Amesema filamu hiyo inaoneshwa kwa mara ya kwanza Ijumaa tarehe 23 mwezi huu saa 3 usiku na kurudiwa Jumamosi na Jumapili ili kuwapa muda mashabiki zake waweze kuona filamu hiyo
Aidha ameishukuru kampuni ya Steps entertainment kwa kuanzisha mfumo huu mpyaa wa kuonesha filamu kabla hazijaingia sokoni
Filamu hii inatarajia kuingia sokoni Jumatatu 26 mwezi wa 9 nchi nzima,kwa sasa hivi Jb anatamba sokoni na filamu ya chungu cha tatu akiwa na Wema Sepetu na wasanii wengine wengi.

FILAMU YA NANI ZAIDI IMEINGIA SOKONI

FILAMU YA NANI ZAIDI IMEINGIA SOKONI

KAMA UMEPITWA NA KIPINDI CHA STARS AND FANS KIKO HAPA







Mcheza filamu za kitanzania Sonnatah Nduka akiwa kwenye kipindi cha stars and fans kinachorushwa sibuka maisha channel 111 kila ijumaa saa 1 usiku

Friday 2 September 2016

SIBUKA MAISHA WAICHUKUA KESHO YANGU

Filamu ya Kesho yangu leo saa tatu usiku inaingia kwenye histori ya kuwa filamu ya kwanza kutoka kampuni ya usambazaji steps entertainment kuonekana kwenye Sibuka Maisha channel 111 ndani ya startimes kabla ya kuingia sokoni

Filamu hiyo iliyochezwa na waigizaji wenye uwezo mkubwa kutoka Dodoma Sonnatah Nduka,Gosbert Mvungi na wengine wengi itaingia sokoni jumatatu ya wiki ijayo

Thursday 11 August 2016

MAZIKO SAA SITA KUTOKA JUMATATU IJAYO





Filamu ya Maziko saa sita inaingia sokoni jumatatu 15.08.2016.filamu hiyo imechezwa na wasanii wengi wakali akiwemo Chuchu Ansi,Mzee Majuto na wengine wengi,inasambazwa na steps entertainment,usikose nakala yako

KESHO YANGU KUMTAMBULISHA SONNATA KWENYE TASNIA YA FILAMU BONGO







Filamu ya Kesho yangu kutoka kwa muongozaji mwenye uwezo mkubwa Tanzania Suleshi Marah inatoka tarehe 29 mwezi wa 8 inategemewa kufanya mapinduzi kwenye tasnia ya filamu bongo,kutokana na jinsi ilivyotengenezwa na wausika walivyo tendea haki stori hiyo



Kwenye filamu hiyo ambayo kuna msanii chipukizi Sonnata Nduka imechezewa mjini Dodoma na inasambazwa na Kampuni ya Steps entertainment