Tuesday 5 May 2015

FILAMU YA KIMENUKA YA MAFUFU YAIBIWA


Kupitia ukurasa wake wa instagram Jimmy Mafufu amendika 

Ndugu zangu mashabiki na wadau wa film zangu nasikitika kuwaambia kuwa Film yangu mpya iko jirani sana kutoka lakini Mtu mmoja mjinga asiyependa mafanikio yangu kana kwamba alihusika kunitoa baada ya kujua ninatoa film niliyowaahidi hivi karibuni na yeye amechukua jina la film yangu huku akijua nimelitumia jina hilo na film nimeshauza Steps na iko mbioni kutoka nilimsihi kabla hajatoa

 akakaidi na kuruhusu kifilm chake kibovu kitoke nimehuzunika sana maana nimekula hasara na kubwa niliwalipa wasanii wakubwa wa bongofreva wakafanya sound track na vitu vingi vimekula pesa lakini mjinga huyu ameona yote hayo ni upuuzi kubwa zaidi muandaaji wa film hiyo ndiye aliyeweka sauti (voice over) katika film Yangu na amekiri kuwa amemuuzia huyo aliyenitenda hayo na film yake iliitwa 

(SIKU MOJA)anasema baada ya kuuza film.hiyo mnunuzi alishawishi iitwe KIMENUKA jina ambalo ni la kwangu na film tayari lakini Muhafidhina huyo aligoma na kudai mafufu ni Mtu mdogo akatumia nguvu kujitwalia jina la film yangu kwa hiyo film nitaitoa na kuanzia sasa Sintatumia jina la KIMENUKA ukiiona film yenye jina hilo sio langu na film hiyo siyo yangu jina nitalitangaza hivi karibuni yaliyotokea 
nimemwachia Mungu na kama walidhani wameniwin wamechemsha na kikazi nimejipanga Pumbavu sana.

No comments:

Post a Comment