Tuesday 20 December 2016

KUMBE MIMBA YA NISHA ILIKUWA KIKI TU

 Wiki kadhaa zimepita tangu muigizaji  Salma Jabu nisha kuweka picha mtandaoni akiwa mja mzito na kusema ujauzito huo umetokana na kubakwa na aliyekua mpenzi wake ambae ata hivyo hajamuweka wazi
 Akifunguka kiafrika bila hofu yoyote kwa kua Tanzania ni nchi huru amesema yeye sio mjamzito ila amesema hivyo ili kuona mtu mwenye ujauzito uliotokana na kubakwa jamii inampokeaje anapoweka wazi swala lake
 "mimi sina ujauzito ata ile picha yangu ya kwanza kuweka mtandaoni na kujitangaza ni mimi,sikua mimi ile ni picha ya mdada wa Nigeria nimeitumia tu"
Amesema kwa yupo kwenye maandalizi ya filamu yake mpya amabayo imelenga mambo ya mimba za utotoni na ataifanya vizuri kwakua ameshapitia kipindi cha ujauzito wa mtu aliyebakwa na kutelekezwa


kwa sasa Nisha anatamba na filamu ya Kiboko kabisa akiwa na mkongwe wa tasnia hii King Majuto,inasongezwa mtaani na kampuni ya steps entertainment.

No comments:

Post a Comment