Monday 17 August 2015

KAJALA:HII NI LAANA NILIANDIKA GEREZANI


Mcheza filamu mwenye jina kubwa Tanzania Kajala Masanja amesema story ya hii ni Laana ameiandika akiwa Gerezani na alipotoka akaona asichelewe kuwapa mashabiki wake utamu wa filamu hiyo ya kusisimua

Amesema mambo yaliyomo kwenye filamu hiyo ni mambo ambayo vijana wengi wamekua wakitamani kuwa nayo,tena kwa njia ambazo hazimpendezi mwenyezi mungu

"Hii na Laana ni story amabayo nimeandika nikiwa Gerezani na inahusu kijana mmoja ambae alimaliza chuo,na akubahatika kupata kazi,akawa na maisha ya chini sana,lakini alikua anasaidiwa na mpenzi wake,mwisho wa siku anakuja kukutana na rafiki yake waliosoma nae lakini yeye ana maisha mazuri

Ndio anaamua kufata njia alizopita rafiki yake kupata utajili,anaenda kwa mganga na mganga anampa masharti ya kutembea na mama yake,sasa kilichoendelea hapo itafute ikitoka 20.08.2014 ujue zaidi

Kwenye filamu hii Kajala amecheza na Gabo zigamba pamoja na pasta miyamba na wengine wengi inasmbazwa na stepsentertainment









No comments:

Post a Comment