Monday 5 October 2015

ESTER KIAMA:MUHANGA INA MAFUNZO MAKUBWA KWENYE NDOA

Staa wa filamu za kibongo nchini Ester Kiama amesema filamu ya Muhanga ina mafunzo makubwa kwenye ndoa,kwa kua stori yake inalenga maisha halisi ya matatizo wanayokutana nayo wanandoa,wengi wanaotafuta mtoto
 Ester amesema filamu hiyo inahusu wanandoa waliokaa mda mrefu bila kupata mtoto,mpaka mama mkwe akawa anamsumbua mtoto wake wa kiume jambo lililopelekea mtoto huyo kujitoa Muhanga

Anasema kwenye filamu hiyo ambayo ameshiriki na Issa Mussa cloud,Suleiman Barafu,pamoja na Luckness Mokiwa yeye amacheza kama mwanamke ambae ameamua kuzaa na mume wa mtu kwa makubaliano maalum ili kuioka ndoa ya mwanaume huyo
"kwenye filamu hiyo mm ndio mwanamke ambae Cloud alinifata nimzalie mtoto baada ya mkewe kuonekana hawezi kuzaa kabisa,hivyo akajitoa muhanga kuja kwangu kwa makubaliano maalum zaid nunu filamu hii ujifunze mambo mengi "

filamu hiyo ipo madukani kote Tanzania inasmbazwa ns steps entertainment

No comments:

Post a Comment