Saturday 14 February 2015

STEVEN KANUMBA PENGO LAKO BADO LIPO

 Alikuwa anajulikana zaidi kama “The great” kama mwenyewe alivyopenda kujiita. Jina lake halisi ni Steven Kanumba. Alikuwa mmoja wa waigizaji wakubwa sana ndani ya tasnia ya bongomovies. Na Katika historia ya tasnia ya filamu nchini Tanzania, Kanumba ndiye aliyekuwa msanii wa kwanza nchini kufanya kazi nje ya nchi na kuweza kuwavuta wageni kutoka nchi mbalimbali kuja kuigiza Tanzania, hasa Wanigeria kama vile Mercy Johnson, Emmanuel France, Nkiru Silvanus, Ramsey Nouah, na wengine wengi. Kanumba pia ameweza kuwaleta waongozaji filamu kadhaa was Kinigeria nchini. Moja ya filamu zilizompa umaarufu sana kimataifa ni pamoja na Devil’s kingdom nyingine kama Dar 2 Lagos na Cross my sin. Alikuwa mmoja wa sanii wenye uwezo mkubwa kifenda na utajiri wako ulikuwa unakadiriwa kuwa zaidi ya shillingi milioni 300 za kitanzania.
Steven Kanumba alizaliwa tarehe 8 mwezi wa Kwanza mwaka 1984 huko shinyanga. Kwa kabila alikuwa ni msukuma. Alipata elimu yake ya awali katika shule ya msingi msingi ya Bugoyi,  na kuendela na masomo ya sekondari huko Mwadui huko huko shinyanga na baadaye kuhamia katika shule ya sekondari ya Dar es salaam Christian Seminary akiwa kidato cha pili ambako alisoma mpaka kidato cha nne na akaendelea na masomo ya kidato cha tano na sita katika shule ya sekondari ya jitegemee iliyopo Dar es salaam.
Kanumba alianza kuigiza toka alipokuwa shule ya msingi kabla ya kujiunga na kikundi cha kaole sanaa group miaka ya tisini. Akiwa kaole kanumba alikutana na walimu wa sanaa toka chuo cha sanaa bagamoyo na vyuo vingine ambako alipata mafunzo zaidi ya uigizaji na baadae alikutana na Dr. Nyoni toka Chuo kikuu cha Dar es Salaam ambako alweza pata mafunzo ya uigizaji kwa muda wa miezi mitatu.

Baada ya hapo kanumba alianza rasmi kuigiza filamu na filamu moja ya filamu zake za kwanza kuigiza zilikuwa sikitiko langu na Johari ambazo zilimpa umaarufu zaidi na kumuwezesha kufanya kazi nyingine mbalimbali ndani na nje ya nchi.
Steven kanumba alikuwa mmoja wa wasanii wa kwanza Tanzania kuweza kutembelea studi za filamu za Universal Studio pamoja na Warner bros zilizopo huko nchini Marekani. Pia kanumba alikuwa mtunzi wa nyimbo na alikuwa na uwezo wa kupiga vifaa vya muziki kama kinanda na gitaa


Steven Kanumba alifariki dunia tarehe saba(7) mwezi wa nne (4) mwaka 2012 baada ya kuanguka chmbani kwake kufuatia ugomvi baina yake na aliyekuwa mpezi wake Elizabeth Michel (LULU). Alifariki muda mfupi baada ya kufikishwa Hospitali ya taifa ya Muhimbili. Mazishi yake yalihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa nchi na umati unaokadiriwa kufikia watu elfu thelathini (30,000).

No comments:

Post a Comment