Wednesday 18 February 2015

NISHA KUWAPA ELIMU YA MAISHA MASHABIKI

 MWIGIZAJI wa filamu nchini, Salma Jabu ‘Nisha’, amesema anatarajia kuachia kazi yake mpya aliyoipa jina la ‘Shida’, ambayo itatoa mafunzo kwa mashabiki kukabiliana na hali yoyote ya maisha.
Akizungumzia filamu hiyo hapo jana, Nisha alisema filamu hiyo inatarajia kuingia sokoni mwishoni mwa mwezi huu, ambapo ameweza kumshirikisha nguli mwingine, Gabo.
"Napenda sana kusikiliza maoni ya mashabiki zangu na kuyafanyia kazi,kwenye filamu ya SHIDA nimewakumbusha Matilda kwa wale walioniomba nitoe serious movie pia sio comedy peke yake.. mimi mwenyewe nililia Ukweli kwa matukio yake, ingawa pia SHIDA itakuburudisha,kukuelelimisha na kukupa ladha halisi ya maisha ya mtanzania ungana nasi Gabo,Nisha,Tunu na wasanii kibao kutoka Zanzibar house of talent,chini uongozi na wapiga picha mashuhuri Tanzania CLEAR PICTURES" .
Amesema mashabiki wategemee mambo mengi mazuri zaidi kutoka kwake, kwani mara nyingi amekuwa akifanya kazi kwa mpangilio ili kuhakikisha anatoa vitu vyenye ubora.
Filamu hii inasmbazwa na kampuni ya steps entertainment kuwa wakwanza kuiona kwa kupiga namba 0788233635 kupata filamu kwa bei poa kabisa

No comments:

Post a Comment