Alikuwa anajulikana
zaidi kama “The great” kama mwenyewe alivyopenda kujiita. Jina lake halisi ni
Steven Kanumba. Alikuwa mmoja wa waigizaji wakubwa sana ndani ya tasnia ya
bongomovies. Na Katika historia ya tasnia ya filamu nchini Tanzania, Kanumba
ndiye aliyekuwa msanii wa kwanza nchini kufanya kazi nje ya nchi na kuweza
kuwavuta wageni kutoka nchi mbalimbali kuja kuigiza Tanzania, hasa Wanigeria
kama vile Mercy Johnson, Emmanuel France, Nkiru Silvanus, Ramsey Nouah, na
wengine wengi. Kanumba pia ameweza kuwaleta waongozaji filamu kadhaa was
Kinigeria nchini. Moja ya filamu zilizompa umaarufu sana kimataifa ni pamoja na
Devil’s kingdom nyingine kama Dar 2 Lagos na Cross my sin. Alikuwa mmoja wa
sanii wenye uwezo mkubwa kifenda na utajiri wako ulikuwa unakadiriwa kuwa zaidi
ya shillingi milioni 300 za kitanzania.
Steven Kanumba
alizaliwa tarehe 8 mwezi wa Kwanza mwaka 1984 huko shinyanga. Kwa kabila
alikuwa ni msukuma. Alipata elimu yake ya awali katika shule ya msingi msingi
ya Bugoyi, na kuendela na masomo ya sekondari huko Mwadui huko huko
shinyanga na baadaye kuhamia katika shule ya sekondari ya Dar es salaam
Christian Seminary akiwa kidato cha pili ambako alisoma mpaka kidato cha nne na
akaendelea na masomo ya kidato cha tano na sita katika shule ya sekondari ya
jitegemee iliyopo Dar es salaam.
Kanumba alianza kuigiza toka alipokuwa shule ya msingi kabla ya
kujiunga na kikundi cha kaole sanaa group miaka ya tisini. Akiwa kaole kanumba
alikutana na walimu wa sanaa toka chuo cha sanaa bagamoyo na vyuo vingine
ambako alipata mafunzo zaidi ya uigizaji na baadae alikutana na Dr. Nyoni toka
Chuo kikuu cha Dar es Salaam ambako alweza pata mafunzo ya uigizaji kwa muda wa
miezi mitatu.
Baada ya hapo kanumba alianza rasmi kuigiza filamu na filamu
moja ya filamu zake za kwanza kuigiza zilikuwa sikitiko langu na Johari ambazo
zilimpa umaarufu zaidi na kumuwezesha kufanya kazi nyingine mbalimbali ndani na
nje ya nchi.
Steven kanumba alikuwa mmoja wa wasanii wa kwanza Tanzania
kuweza kutembelea studi za filamu za Universal Studio pamoja na Warner bros
zilizopo huko nchini Marekani. Pia kanumba alikuwa mtunzi wa nyimbo na alikuwa
na uwezo wa kupiga vifaa vya muziki kama kinanda na gitaa
Steven Kanumba alifariki dunia tarehe saba(7) mwezi wa nne (4)
mwaka 2012 baada ya kuanguka chmbani kwake kufuatia ugomvi baina yake na aliyekuwa
mpezi wake Elizabeth Michel (LULU). Alifariki muda mfupi baada ya kufikishwa
Hospitali ya taifa ya Muhimbili. Mazishi yake yalihudhuriwa na viongozi
mbalimbali wa nchi na umati unaokadiriwa kufikia watu elfu thelathini (30,000).