Wednesday 1 June 2016

ODAMA:NAJIKUBALI NA SIFANANI NA MTU LABDA HUYO MTU AFANANE NA MIMI

 Mcheza filamu za kitanzania Jennifer Kyaka(Odama)kupia ukurasa wake wa instagram ametoa hizi zake juu ya watu wanaopenda kujifananisha na na watu flani na kuacha kujikubali wenyewe

Odama amesema

Kitu Kinachofanya Usijikubali Na Kujiona Wewe Ni Mrembo Na Wakipekee Kuliko Warembo Wote Ni Kujaribu Kujifananisha Na Flani Ama Kuwa Kama Flani Unatoka Kwenye Uhalisia Wako Na Unaacha Kuitambua Nguvu Iliyo Ndani Yako Na Kuanza Kuitamani Na Kuivaa Nguvu Na Uhusika uliyo Ndani Ya Mwingine


Jikubali Ulivyo Kuwa Wewe Ni Wakipekee Na Kwavile Ulivyo Waeza Tengeneza Upekee Wako Bila Hata Ya Kujibadilisha Kuwa Kama Flani Ama Kundi La Watu Wengi.....


Kujiamini Huleta Kujitambua Na Kujitambua Humfanya Mtu Afanikiwe Na Kuimarika Ktk Uhalisia Wa Vitu Vyake Vyote Vinavyomzunguka..... Kujikubali Sio Rahisi Kama Hujitambui Wewe Ni Nani, Ila Wote Wanao Jitambua Hujiamini Na Huifurahia Nguvu Yao Ya Kuwa Wakipekee Hufurahia Kuutengeneza Upekee Wao Na Kusimamia Kweli Yao .... Morning guys👋


No comments:

Post a Comment