Wednesday 25 March 2015

RAY KUWAPA ZAWADI YA PASAKA MASHABIKI WAKE

.Mcheza filamu anaemiliki kampuni ya RJ COMPANY Vicent Kigosi (Ray) anatarajia kuachia filamu yake ya Kichwa cha Kuku tarehe 01.04.2015 kama zawadi ya pasaka kwa mashabiki wake

Ray amesema kwenye filamu hiyo amecheza na waigizaji wengi nyota akiwemo Skyner Ally na Rayuu na filamu hiyo inamafundisho makubwa sana kwa wanawake wanaoishi kwenye ndoa zao akifafanua filmu hiyo anasema "Unajua katika maisha siku zote mwanamke anatakiwa kujiamini na anachokokifanya usidhani kama unafanya ushujaa bali unaonyesha udhaifu ,inawezekanaje ukamuachia mtu aendelee kufaidi raha za mumeo"

Filamu hii inasmbazawa na kampuni ya steps entertainment hivyo naomba mashabiki wangu wanunue DVD original ili kukuza kipato cha wasanii wao watanzania

SKYNER

RAYUU

No comments:

Post a Comment