Friday 6 March 2015

KUWA STAR SIO MPAKA UKAE UCHI KAMA UWEZO HUNA AUNA TU JIPANGE

 Mwanzoni mwa miaka ya tisini ilikua kila nyumba kuna msanii wa kuimba,vipaji vilikua vingi ila kwa sasa waliofata mkumbo wanaonekana na wenye uwezo ndio wanamafanikio kwasasa,kuna baadhi ya watu waliacha shule wakiamini muziki utawalipa lakini zimebaki kuwa stori tu za mjini,sasa na kwenye tasnia ya filamu wamejazana sasa hivi kila nyumba kuna muigizaji kitu ambacho sio kweli kabisa bali wanafata mkumbo wakiamini ipo siku watafanikiwa.
 Dada zetu wengi wanauchu wakutoka na kuwa mastaa wakubwa nchini lakini wengi wao wanaishia kudhalilishwa na kutumiwa kingono bila faida yoyote wanayopata,mfano mzuri ni hizi picha nimekutana nazo facebook zimewekwa na moja ya wataarishaji wa filamu nchini akimnadi huyu dada kuwa ni msanii mzuri sasa hofu yangu ni je huyu mtaarishaji amesomea wapi?na kwanini anatuma picha hizi kwenye mitandao ya kijamii mi binafsi naona ni udahlilishaji na kutojitambua.
 Mwana muziki wa bongo fleva Nay wa mitego amewai kusema kwenye moja ya nyimbo zake kuwa "makahaba wenye viwango wapo bongo movie,bongo movie kama danguro poleni Ray na JB kuonesha ulijali nanyie mnawapitia" wasanii wengi walilalamikia kauli hii lakini je iki cha kupiga picha za uchi na alichokisema Nay kunatofauti gani?Je mastaa wakubwa ndio wanawapotosha chipukizi wanaokuja au chipukizi wanajipotosha wenyewe kwa kuamini kukaa uchi kutawafanya watambulike kwa halaka na kupata mashabiki wengi? ebu soma ujumbe huu wa Madebe Lidai na picha alizoweka kwenye mitandao ya kijamii


Ongea chochote juu ya msanii huyu....!
 — with Warda Salum.
 Tasnia itakufa kwa kudhalilishwa na wachache waliovamia fani kuja kuchafua wenzao,na kuwadhalilisha waonekane hawana maana kabisa kwenye kazi zao za sanaa kumbe ni ujinga wawa chache wasiojielewa ndio wanaalibu
Ushauri wangu kwa dada zangu mnaoingia kwenye filamu,msijidhalilishe kwakupiga picha za uchi ili mjulikane kujulikana sio lazima kupiga picha za uchi ni uwezo wako binafsi pamoja na kujituma tu na sio vinginevyo9

No comments:

Post a Comment