Monday 23 March 2015

Baba Haji: Kanumba Ameondoka Na Sanaa ya Bongo

Staa wa Bongo Movies, Haji Adamu Rajabu ‘Baba Haji’ amefunguka kuwa, soko la filamu  Bongo kwa sasa linashuka siku hadi siku  na sababu kubwa ni  wasanii kutopenda kwenda shule kujiendeleza kielimu na kujua ni jinsi gani filamu inatakiwa kutengenezwa.
 Baba Haji amesema anakubaliana na kila mtu anayesema soko limeshuka kwa sababu wasanii wanapenda kukopi,  pia hawapendi kuandika miswada ya filamu na kupendelea kuingiza mambo ya kizungu, ingawa wengi wanamtaja msanii Steven  Kanumba kuwa ameondoka na soko hilo.

Baba haji anafunguka kama hivi…
Mwandishi: Vipi, mbona kimya kingi? Soko la filamu limekwenda na Kanumba au unalionaje?
Baba Haji: Tunaweza kusema hivyo, kwa sababu yeye alikuwa anajitoa kwa hali na mali, anatoa pesa zake kwa ajili ya filamu, ni tofauti na wasanii wengine ingawa pia alikuwa akitumia sana ‘media’ kueleza kila anachokifanya.
Mwandishii: Unadhani ni kwa nini wasanii wengi wanapenda kufanya kazi na Wanaigeria?
Baba Haji: Kwa sababu wao wanalipwa tu ila nchi nyingine wana sheria kali, kufanya kwao filamu ni mpaka uwe na digrii ya sanaa.
Mwandishi:  Wewe umejipanga vipi kwa hilo?
Baba Haji: Mimi nimejipanga vizuri kwa sababu nilikwenda Shule Bagamoyo (Pwani) kwa muda wa miaka mitatu na nilifanikiwa kupata diploma ya sanaa, wakati nakwenda shule nakumbuka Kanumba aliniambia napoteza muda kwani soko ndiyo lilikuwa limechanganya ila namshukuru Mungu hata niliporudi sijapotea sana kwa mashabiki.
Swala hili sio mara ya kwanza kusema wasanii na mashabiki kulisema, kwako wewe mdau, unadhani kuna ukweli wowote hapa? mbona alivyokuwepo watu hawakusema kuwa yeye ndio amebeba soko?...

No comments:

Post a Comment