Saturday 14 March 2015

RAY: “VIP haijaigwa popote duniani” Ni baada ya Kashfa iliyompata JB kwenye ‘Mzeee wa Swagga’.

MWIGIZAJI na Muongozaji mahiri wa filamu tokea bongo movie  Vincent Kigosi AKA ‘Ray’ ametangaza dau nono kwa mtu yoyote anayethibitisha kuwa filamu yake ya V.I.P kuwa imeigwa kutoka katika filamu yoyote kutoka nje ya nchi au ndani ya nchi and thet person atayefanya hivyo atampatia milioni moja taslimu.

Ameamua kufanyahivyo baada ya mdau mmoja kuwashutumu wasanii wakubwa kuwa wamekuwa (VILAZA) mabingwa wa kuiga filamu kutoka nje yaani (Copy and paste) wakati wakijadili filamu ya Mzee wa Swaga ya JB iliyoigwa kutoka katika moja ya filamu ya kihindi na kuzua mjadala.

“Hakuna wazo jipya mtu unaweza kufanya na likawa la kipekee, hadithi zinaweza kufanana lakini si hadi dialogue, kuna mtu anadai filamu yangu ya V.I.P nimeiga kutoka sinema ya Ghana, sasa mimi nasema mtu ambaye ana filamu niliyoiga aje nayo ofisini nitampatia milioni moja,”anasema Ray.

No comments:

Post a Comment