Tuesday 9 December 2014

ZAMARADI NA JB WAJIBISHANA INSTAGRAM CHANZO KIKIWA NI FILAMU ZA BONGO


leo asubuhi kupitia mtandao wa Instagram mtangazaji wa kipindi cha take one na movie leo ndani ya Clouds media ameshindwa kuficha hisia zake kwenye tasnia ya filamu na kuandika haya
"
Natamani sana siku moja atokee mtu kwenye hii sekta atutambulishe hata kama sio kimataifa basi africa tu... R.I.P KANUMBA alianza kuonesha mwangaza na juhudi binafsi zilionekana na kila mtu aliona huenda angefika mbali.. lakini baada ya hapo sioni tena!!!!
Mbona hapa nyumbani ni wakubwa tu..? Nini kinawakwamisha..?  Kwanini wasanii wetu wa filamu ukubwa wao unaishia nyumbani tu....!!? Tatizo ni nini!!!????? kiukweli ni kama inakatisha tamaa na inaonekana kabisa watu wamerelax na ustar wa bongo wakati wana nafasi ya kufanya vizuri zaidi... wana bongo movie tukifika kwa wenzetu unaona kabisa tunapwaya kiasi gani.. Ujanja wetu ni nyumbani tu!!?? why!!!?? tukianza utanzania wa kufichaficha tutasifiana uongo lakini tukiwa wakweli na nafsi zetu tutaliona hilo na kuchukulia kama challenge..!!! ukweli ni kwamba hii tasnia inasikitisha!!! tena sana.. nahisi sasahivi tunafanya filamu kwa ajili ya nyumbani tu na tukiingia kwenye mabendi tukisharushwa tumeridhika!! kweli!! hapa ndio mnapotaka mfike!!? ukifika sehemu ukiwa juu nchini kwako tunachotegemea ni wewe kupasua mawimbi uende mbali zaidi nje ya mipaka!! lakini ukiamua kurelax hapo ulipo inamana unasubiri kushuka sababu kiukweli huwezi kukaa juu milele!!! kwanini mmeridhika hivi!!! kaka JB tatizo ni nini!!!??
Mi nakuangalia wewe kama mfano wa msanii mkubwa sana kwenye tasnia kwa sasa... mbona umerelax!!!??? umeridhika na ustar wa tanzania!!!? una kila kitu cha kukufikisha mbali... kinachohitajika ni juhudi binafsi tu ili kesho na sisi tufike mahala pazuri!! hebu tuongee wapenzi.. mnahisi huku kwenye bongo movie TATIZO LIKO WAPIII…!!???

Baada ya maelezo hayo ya Zamaradi JB na yeye aliamua kumjibu mtangazaji huyo kupia ukurasa wake wa instagram

“Kwako Zamaradi na wengine wote.

Kwanza napenda niwashukuru wote kwa jinsi mnavyotuwazia mema. Naomba nichukue nafasi hii kuwapongeza waigizaji wote wa Tz na waandaaji wa filamuU kwa kuthubutu kutengeneza filamu hizi katiks mazingira magumu. Najua watanzania wengi wangependa kuona tukipeperusha bendera nje,lakini naomba muwape wasanii muda.
Tasnia hii ni changa na ina changamoto ambazo zinakatisha tamaa. Hebu tujiulize kwa nini wasomi wengi waliosomea filamuu UDSM na BAGAMOYO hawafanyi filamu hizi? Wasambazaji wengi wakubwa mamu,wananchi na hata hans pop walijaribu wakakimbia, kuna producer mkubwa hapa nchini JOHN RIBER ambaye ametengeneza filamuu kama NERIA na YELLOW CARD lakini naye ukimwambia njoo kwenye hizi filamu atakupa jibu.
Nakubali tuna makosa mengi kama ubora wa filamu zetu na stori lakini nataka niwaambie mazingira ya kufanya filamu bongo yanakatisha tamaa wizi wa kazi zetu umezidi na wasambazaji wengi wamekimbia. Binafsi najipanga kuwa mtayarishaji zaidi kuliko mwigizaji kwa sasa kupitia JERUSALEM FILMS na ndio maana filamu nyingi natoa nafasi kwa vijana ambao kama mabadiliko ya sera ya filamu yatafanywa watatuwakilisha nje.
Kiswahili kisichukuliwe poa kwani kina nafasi kibwa sana. Tukumbuke SHARUK KHAN ni ‘actor’ tajiri2 dunian lakini filamu zake ni za kihindi. Hebu sote tusaidiane kupambana na changamoto hizi na tuanze na EAST AFRICA kwanza huku tukiboresha, wasomi wa filamu msikimbie njooni tuanze wote na tuwape moyo wasanii wetu waliojaribu kusimamisha tasnia hii kwa vimtaji toka mifukoni mwao na vipaji walivyopewa na mungu bila msaada kutoka popote. Asanteni kwa kutuunga mkono kwemye filamu zetu.”

No comments:

Post a Comment