Kampuni ya
usambazaji wa filamu bora Tanzania ya Steps Entertainment
Ltd inatarajia kutoa bidhaa mpya za filamu kwa mwaka ujao wa 2015 filamu
zenye ubora muonekano mzuri huku pia kuwaletea walaji bei rafiki kutoka kampuni
bor a ya usambazaji wa filamu Tanzania StepsEntertainment Ltd.
Steps
Entertaiment Ltd ni ilioanzishwa mwaka 2007 nchini Tanzania na makao yake makuu
yako jijini Dar salaam, Kampuni ya Steps Entertainment inajishughulisha na
usambazaji wa filamu za Kitanzania maarufu kwa jina la
BONGO MOVIES
Tangu kuanzishwa
kwake Kampuni ya Steps Entertainment imekuwa mdau mkubwa katika kukuza tasnia
ya filamu nchini Tanzania na mpaka sasa ndiyo kampuni kubwa ya usambazaji wa
filamu nchini Tanzania.
Kampuni ya
Steps Entertainment kupitia mikakati yake ya kuinua tasnia ya filamu nchini
Tanzaania imefanikiwa kutoa ajira nyingi kwa wadau mbalimbali wa tasnia ya
filamu, wakiwemo waandaaji wa filamu, Waigizaji, Wasambazaji wakubwa kwa
wadogo, Wauzaji wa rejareja na wanaoonyesha na au kukodisha katika
vibanda.
Akiongea
na wanahabari Carlos Johns Silondwa mtendaji mkuu ameielezea Steps
Entertainment imefanikiwa pia kuvuka mipaka na kufikisha sinema za kitanzania
katika mataifa mbalimbali ya nje na katika luninga za kimataifa na televisheni
za ndani kuonyesha kazi za nyumbani.
“Kwa sasa
mataifa mengi Ulaya na nchi za Scandinavia wanajifunza Lugha yetu ya Kiswahili
kupitia filamu zetu, moja kwa moja utaona njia nyingine katika kukuza Kiswahili
nje ya nchi kwa njia ya filamu tu ambazo zinasambazwa na kampuni hii, na
kutengeneza ajira kwa vijana wengi,”
Pia
kampuni imekuja na bei rafiki kwa mlaji baada ya kilio chake kuumiza kwa muda
mrefu, kampuni kwa kutumia wataalamu pamoja na wadau wa filamu kutoka sehemu
mbalimbali wamefanya utafiti ili kupata Mwarobaini wa Maharamia wa kazi za
nyumbani kampuni imeshusha bei.
Hiyo
inatokana na hali halisi filamu inatakiwa imfikie mtumia kwa 6,000/ lakini
utafiti umebaini kuwa mtanzania anatumia zaidi kiasi cha 34,000/ na zaidi bila
kuimiliki Dvd hiyo, baada ya Vibanda au Library kuanzimisha, badala ya
kumuuzia.
Filamu
ambayo itauzwa ikiwa katika ubora na muonekano mzuri, inakuja baada ya filamu
kutoka nje, kuuzwa kwa bei ya chini kabisa na kuleta ushindani pamoja na kuwa
sinema hizo hazilipiwi kodi tofauti sana, nakuzifanya zinunulike sana kuliko
filamu za ndani kutokana na bei yake kuwa ndogo.
Kampuni
ya Steps Entertainment ilifanya utafiti ili kujua ni jinsi gani filamu zinatoka
mbali na bado zinawafikia walaji kwa bei ya chini ni baada ya utafiti huo ndipo
Kampuni ya Steps Entertainment iliamua kujibana na kufanikiwa kuingiza na
kufunga mtambo mkubwa wakisasa kuzalisha cd/dvd, kuzirekodi na kuziprinti hapa
hapa nchini.
Tofauti
na siku za nyuma ambapo ilikuwa inaagiza cd/dvd kutoka nje ya nchi na kuja
kuzirekodi tu, sambamba na mtambo huo pia kampuni hii imeamua kubuni
kifungashio kipya yaani kasha za cd/dvd, ambayo ni za bei nafuu, zinamuonekano
mzuri zaidi, ni rahisi kuhifadhi, nirahisi kusafiriha na nirafiki wa mazingira.
Mtambo
mkubwa na wakisasa pamoja na kifungashio kipya vimepunguza sana gharama za
kuzalishia nakala za dvd na cd na hivyo Steps imeona ni vyema kuonyesha moyo wa
uzalendo kwa wateja wake kwa kuwapunguzia bei ya kununua filamu kwa
kuwauzia kwa nusu ya bei ya awali.
Kampuni ya
Steps Entertainment inaamini kuwa kitendo cha kupunguza bei za filamu zake,
kitawanyima Maharamia ulafi na wizi wa wazi kabisa, kama kampuni inakaribisha
wadau wote wanaosambaza filamu kwa kuja kwetu kuzalishiwa filamu zao kwa bei
rahisi sana ili huyu Gaidi mkubwa anayenyonya kazi zetu aache.
·
Kinaonyesha moyo wa uzalendo lakini pia
kitapandisha mauzo ya filamu za kitanzania ambapo kwa ujumla wake itaongeza
kipato kwa wasanii na kuchangia pato la Taifa.
·
Kitapunguza uharamia wa filamu kwa kuwa bei
itakuwa chini hivyo kila mtu atakuwa na uwezo wa kununua nakala halisi.
·
Kitaziwezesha library zinazokodisha filamu kuacha
kukodisha na badala yake kuanza kuuza moja kwa moja
Hivyo
basi Kampuni ya Steps Entertainment inamaliza mwaka 2014 na kuingia mwaka 2015
kwa kubororesha bidhaa zake, zikiwa katika ubora na muonekano wa kuvutia kwenye
kasha la bahasha ngumu, bidhaa hizi zitamfikia mlaji kwa bei ya 1,500/=
tu bei hii kwa filmu zitakazo kuwa katika kifungashio kipya pekee filamu
zitakazo kuwa katika kifungashio cha zamani yaani kasha la plastiki zitaendelea
kuuzwa kwa bei ile ile na wateja watakuwa huru kuchagua aina ya kifungashio
pale wanaponunua nakala za filamu za Steps
Hivyo basi
Steps Entertaiment imeanzisha kampeni maalum ya “Faidika na Steps kwa
bidhaa bora, Wasanii nyota, na Filamu Bora”.
Kampuni ya
Steps Entertainment inawaomba wadau wote kuendelea kuzienzi filamu za
kitanzania ili kukuza kipato cha wasanii na taifa kwa ujumla , kutangaza lugha
ya Kiswahili na utamaduni wa kitazania.
Bei zetu
zitakuwa wazi kwa maan za steps tofauti ya bei iliyoandikwa kwenye kasha ya
kuonekana zikiwazimeandikwa katika kasha na mwananchi asikulaghai mtu wa
Library eti usinunue hadi hakukodishe sema No.
Mwisho,
Tunaiomba Serikali Chini ya Rais wetu Mpendwa Mheshimiwa Dr. Jakaya Mrisho
Kikwete wawasaidie wadau wa filamu kupambana na uharamia wa filamu ambao kwa
sasa umevuka mipaka wezi wanafanikiwa wasanii wanabaki Maskini.
MUNGU
IBARIKI TANZANIA Mungu bariki Afrika
Carlos
Johns Silondwa
Mtendaji
Mkuu.
No comments:
Post a Comment