Wednesday, 31 December 2014

DIAMOND AMEWAI KUMUOMBA ALIKIBA WAPIGE PICHA,USHAHIDI HUU HAPA

 Kwenye picha hii Alikiba na Marlow walikua ndio mastaa wa kubwa kwa wakati huo na ukiangalia picha ni wazi Diamond ameomba kupiga hiyo picha na mastaa hao wakubwa kwenye muziki
 Pia picha hii Diamond yuko mbali na wenzake hivyo yeye ndio ameomba kupiga hiyo picha
 Pia picha hii inajieleza kabisa kua bwana mdogo Diamond ndio ameomba kupiga picha na Ali kiba
Hapa Diamond ameomba kukaa karibu na Ali kiba ili wapige picha na Alikiba anaonekana kabisa anaendelea na stori lakini bwana mdogo Diamond amemtolea macho mpiga picha hivyo yeye ndio ameomba kupiga hiyo picha

MASTAA SABA WAKIKE WALIOFANYA VIZURI KWENYE FILAMU KWA MWAKA HUU 2014

WASTARA JUMA
 Namba moja inakwenda kwa Wastara Juma,kwa mwaka huu amecheza filmau sita mbili zikiwa za kwake filamu hizo ni Gumzo,Dr Max,Last Decision,Uaminifu Dhaifu,Njia Panda na Mama kijacho ,pia amepata tuzo kama msanii bora wa kike kwa mwaka huu kupitia tuzo za action and cut na tuzo ya heshima aliyopewa na team wastara,pia amefanikiwa kucheza filamu nchini London chini ya kampuni ya didas entertainment

SALMA JABU NISHA
 Namba mbili inakwenda kwa Salma Jabu Nisha ambae kwa mwaka huu ameweza kufanya filamu zake tatu na zote zimefanya vizuri na kumuongezea mashabiki zaidi,filamu hizo ni Gumzo,Zena na Betina pamoja na Hakuna Matata aliyofunga nayo mwaka,pia amepata tuzo ya mchekeshaji bora kwenye tuzo za action and cut kwa mwaka huu


SHAMSA FORD
 Namba tatu inakwenda kwa Shamsha Ford kwa mwaka huu ameweza kujizolea umaharufu mkubwa kupitia filamu ya Chausiku na kufanya filamu hiyo kuvunja rekodi ya mauzo ambayo aliwai kuifikia marehemu Kanumba,pia ameshiriki filamu ya Hukumu ya ndoa Yangu


RIYAMA ALLY
Namba nne inakwenda kwa Riyama Ally,kwa mwaka huu amecheza filamu nyingi sana na amejizolea umahaarufu mkubwa kwa mashabiki,filamu kama kigodoro kantangaze,Msuto Daily,Likwata,pamoja na Najua kua zimemuweka nafasi ya juu sana,pia ameweza kushiriki filamu ya kimataifa ya Mateso yangu Ughaibuni ambayo imefanyika nchini London


ODAMA
Namba tano imeshikiliwa na mwana mama Odama kwa mwaka huu amecheza filamu kama Jicho langu na Inside ambazo zote zimefanya vizuri sokoni,pia kwa mwaka huu hakupata skendo yoyote mbaya


ESHA BUHETI
Namba sita inakwenda kwa Esha buheti ambapo kwa mwaka huu amefanya vizuri kwenye filamu kama taliq swalaa na tugawane maumivu pia amechukua tuzo mbili za filamu


WELU SENGO
Welu Sengo amefanya vizuri kwa mwaka huu kupitia filamu ya Hukumu ya Ndoa yangu pia amepata tuzo ya action and cut kama msanii anaesapoti muhusika mkuu kwenye filamu kupitia filamu ya Matrida

Tuesday, 30 December 2014

R.I.P WASANII WETU! KINACHOWAUA KWA KASI CHAJULIKANA

MWAKA 2014 unakatika, matukio ya kukumbukwa ni pamoja na wasanii Bongo kupoteza maisha katika mazingira yasiyotarajiwa, Ijumaa linakupa hatua kwa hatua.Kumbukumbu za haraka zinabainisha kuwa, tangu mwaka 2011 mpaka 2014, wasanii  wenye majina makubwa na madogo wasiopungua 32 wamefariki dunia kwa sababu mbalimbali.

Inauma sana! Katika kipindi cha miaka mitatu kuwapoteza wasanii kwa kiasi hicho ni pigo kubwa kwa tasnia, hasa filamu na muziki, ukiwemo wa muziki wa Injili.
Leo katika toleo hili maalum, Ijumaa linawakumbusha wasanii hao walioaga dunia na namna vifo vyao vilivyotokea.

ALBERT MANGWEHA ‘NGEA’
Alikuwa msanii wa Bongo Fleva. Akiwa na miaka 31 alifariki dunia Mei 28, 2013 nchini Afrika Kusini. Chanzo cha kifo chake inadaiwa ni matumizi yaliyopitiliza  ya madawa ya kulevya. Alizikwa Morogoro, Tanzania, Juni 6, 2013.
LANGA KILEO ‘RAIS WA GHETO’
Alikuwa msanii wa Bongo Fleva. Alifariki dunia Juni 13, 2013 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar akiwa na miaka 28. Kifo chake kilithibitishwa kuwa, kilitokana na kuzidiwa na Ugonjwa wa Malaria. Alizikwa  Juni 17, kwenye Makaburi ya Kinondoni, Dar.
MUHIDIN GURUMO ‘MAALIM’
Alikuwa mkongwe wa muziki wa dansi Bongo. Mpaka kifo chake kilichotokea Aprili 13, mwaka huu kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili akiwa na miaka 74, alikuwa mwanamuziki wa Msondo Music Band. Kifo chake kilisababishwa na kusumbuliwa na matatizo ya moyo. Alizikwa Aprili 15 kwenye Makaburi ya Kijiji cha Masaki, Kisarawe, Pwani.
FATUMA BINTI BARAKA ‘BI KIDUDE’
Alikuwa mwanamuziki wa taarab. Alifariki dunia Aprili 17 2013 Bububu mjini Zanzibar akiwa na miaka inayodaiwa haipungui mia moja. Alizikwa siku iliyofuata, kwenye Makaburi ya Bububu, Zanzibar.
SHEM IBRAHIM KALENGA
Alikuwa mwanamuziki wa dansi. Alifariki dunia Desemba 15, mwaka huu kwenye Hospitali ya Amana jijini Dar es Salaam akiwa na miaka 64. Haijathibitishwa ugonjwa uliomuua. Alizikwa Desemba 16 kwenye Makaburi ya Kisutu, Dar.
MWANAISHA MOHAMED MBEGU ‘AISHA MADINDA’
Alitikisa kwenye eneo la unenguaji kwenye bendi ya muziki wa dansi. Alifariki dunia Desemba 17, mwaka huu Mwananyamala, Dar es Salaam akidaiwa kuchomwa sindano yenye madawa ya kulevya kiasi cha kuwa sumu kali mwilini. Alizikwa Desemba 19 kwenye Makaburi ya Kigamboni jijini Dar. Mpaka kifo chake alikuwa na miaka 35.
SUDI MOHAMED ‘MCD’
Alikuwa mpiga tumba kwenye Bendi ya The Afrcan Stars ‘Twanga Pepeta’. Alifariki dunia Januari 27, mwaka huu mjini Moshi akisumbuliwa na matatizo ya kifua. Alizikwa Januari 28, mwaka huu kwenye Makaburi ya Njoro, Mjini Moshi.
HAMIS KAYUMBU ‘AMIGOLAS’
Alikuwa mwimbaji wa zamani wa Bendi ya The African Stars ‘Twanga Pepeta’. Alifariki dunia Novemba 9, 2014 kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa siku kadhaa akisumbuliwa na matatizo ya moyo. Alizikwa Novemba 10, kwenye Makaburi ya Kisutu jijini Dar.
STEVEN KANUMBA
Alikuwa msanii nyota wa filamu za Bongo. Alifariki dunia Aprili 7, 2012, Sinza jijini Dar baada ya kuangukia sehemu ya nyuma ya kisogo. Mpaka anaaga dunia, Kanumba alikuwa na miaka 28. Alizikwa Aprili 10, kwenye Makaburi ya Kinondoni, Dar akiwa na miaka 28.
MARIAM KHAMIS ‘PAKA MAPEPE’
Alikuwa mwanamuziki wa taarab wa Bendi ya Tanzania One Theatre ‘TOT’. Alifariki dunia Novemba 13, 2012 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar kwa matatizo ya uzazi wakati akijifungua. Alizikwa Novemba 14 kwenye makaburi ya Magomeni, Dar.
GEORGE OTIENO ‘TYSON’
Alikuwa msanii na mwongozaji wa filamu za Bongo. Alifariki dunia Mei 31, mwaka huu kwa ajali ya gari mkoani Morogoro akiwa na miaka 31. Alizikwa Juni 14, Kijiji cha Siaya, Kenya.
AMINA NGALUMA ‘JAPANESE’
Anaitwa Amina Ngaluma. Alikuwa mwimbaji wa bendi mbalimbali nchini ikiwamo Double M Sound na African Revolution. Alifariki dunia Mei 15, mwaka huu nchini Thailand baada ya kupatwa na uvimbe kichwani. Alizikwa jijini Dar, Mei 24, 2014 kwenye Makaburi ya Tabata, Dar.
ADAM KUAMBIANA
Alikuwa msanii wa sinema za Bongo. Alifariki dunia Mei 17, mwaka huu, Sinza jijini Dar baada ya kuugua ghafla. Alizikwa Mei 20, kwenye Makaburi ya Kinondoni, Dar akiwa na miaka 38.
RECHO HAULE
Alikuwa msanii wa filamu Bongo. Alifariki dunia Mei 27, mwaka huu kwenye Hospitali ya Lugalo jijini Dar kwa matatizo ya uzazi wakati wa kujifungua akiwa na miaka 26. Alizikwa Mei 30 kwenye Makaburi ya Kisutu, Dar.
ZUHURA MAFTAH ‘MELISA’
Zuhura Maftah ‘Melisa’ (39) alikuwa chipukizi wa Bongo Muvi. Alifariki dunia Septemba 8, 2013 katika Hospitali ya Hindu Mandal jijini Dar baada ya kusumbuliwa na uvimbe kichwani. Alizikwa kwenye Makaburi ya Kinondoni, Dar.
MZEE MANENTO
Mzee Manento (73) alikuwa msanii wa Bongo Movies. Alifariki dunia Oktoba 29, 2014 katika Hospitali ya TMJ iliyopo Mikocheni, Dar baada ya kusumbuliwa na maradhi ya moyo kwa muda mrefu. Alizikwa kijijini kwake, Mamba-Miamba wilayani Same, Kilimanjaro.
JUMA KILOWOKO ‘SAJUKI’
Sajuki (26) alikuwa staa mkubwa wa sinema za Kibongo. Alifariki dunia Januari 1, 2013 katika Hospitali ya Muhimbili, Dar baada ya kusumbuliwa na maradhi ya uvimbe na kansa ya ini. Alizikwa kwenye Makaburi ya Kisutu, Dar.
SAID NGAMBA ‘MZEE SMALL’
Mzee Small (59) alikuwa mkongwe wa vichekesho Bongo. Alifariki dunia Juni 8, 2014 katika Hospitali ya Muhimbili, Dar baada ya kusumbuliwa na kiharusi kwa muda mrefu. Alizikwa kwenye makaburi ya Tabata-Segerea, Dar.
YESAYA AMBIKILE ‘YP’
YP (26) alikuwa msanii wa Bongo Fleva kutoka Kundi la TMK Wanaume Family. Alifariki dunia Oktoba 20, 2014 kwenye Hospitali ya Temeke, Dar baada ya kusumbuliwa na ugonjwa wa kifua kwa muda mrefu. Alizikwa kwenye makaburi ya Chang’ombe, Dar.
AHMED ALLY UPETE ‘GEEZE MABOVU’
Geeze Mabovu alikuwa msanii wa Bongo Fleva. Alifariki dunia Novemba 12, 2014 baada ya kuumwa kwa zaidi ya mwaka mmoja. Alizikwa huko Iringa katika makaburi ya Makanyagio.
JOHN STEFANO MAGANGA
Alikuwa mwigizaji wa sinema za Kibongo. Alifariki dunia Novemba 24, 2012 katika Hospitali ya Muhimbili, Dar baada ya kuugua ghafla. Alizikwa kwenye makaburi ya Kinondoni, Dar.
JAJI KHAMIS ‘KASHI’
Mwigizaji Kashi alifariki dunia Juni 10, 2013 katika Hospitali ya Muhimbili, Dar alikokimbizwa baada ya kuzidiwa ghafla. Alizikwa kwenye makaburi ya Kinondoni, Dar.
RAMADHAN MKIETY ‘SHARO MILIONEA’
Sharo alikuwa ni staa wa vichekesho na Bongo Fleva. Alifariki dunia Novemba 26, 2012 baada ya kupata ajali mbaya huko Muheza, Tanga. Alizikwa kijijini kwao, Lusanga, Muheza mkoani Tanga.
SHERRY MAGALI
Sherry alikuwa mchekeshaji na mwigizaji wa sinema za Kibongo. Alifariki dunia Oktoba 21, 2014 kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro baada ya kuugua kifua kwa muda mrefu. Alizikwa kwenye Makaburi ya Mji Mpya, Morogoro.
Wakati huohuo, taarifa zilizotufikia zinasema kuwa, yule mchungaji aliyewahi kutabiri vifo vya wasanii wawili wa filamu na Bongo Fleva ameibuka tena na kutabiri kuwa, jinamizi la vifo vya wasanii bado lipo ambapo amesema:
“Natabiri tena vifo vya wasanii nchini. Kwamba, hadi kufikia Februari mwakani (2015), wasanii wawili watapoteza maisha.
“Lakini ili kukwepa mauti wasimame katika roho wakimwomba sana Mungu na kutoa sadaka bila kusahau kuwasaidia yatima na wazee.”
Naye mtabiri maafuru nchini, Maalim Hassan Hussein Yahya amesema roho ya mauti kwa wasanii ipo inazunguka, itafanya kazi hiyo kufikia Aprili mwakani. 

BONDI, WASTARA PENZI LAO KIZUNGU MKUTI


Akizungumza na Uwazi, mpenzi wa Wastara anayetambulika kwa jina la Bondi Bin Salim alidai kuwa yupo kwenye mchakato wa mwisho wa kutoa mahari kwa ndugu wa msanii huyo kiasi cha shilingi milioni 5 pamoja na pete za dhahabu ili aweze kuwa na Wastara.
Alisema kuwa maamuzi ya kutoa posa yamekuja baada ya kuona kila mmoja anaweza kuishi na mwingine kwani wameshasomana kwa muda mrefu.
“Najua si jambo la watu kuhoji sana kwa sababu ndoa ipo na kila mtu atafanya hivyo, nina hela ya mahari tayari na siku ikipangwa ya kutoa tutafanya hivyo lakini ninachowaza sasa ni kuona nafanya vipi ili harusi yangu iwe ya kipekee na zoezi hili tutalifanya mwakani,”
Bond na Wastara wamecheza filamu ya uaminifu dhaifu ambayo inasambazwa na kampuni ya steps intertainment jipatie nakala yako sasa uone walichokifanya

WASTARA NA BONDI NDANI YA UAMINIFU DHAIFU CHEKI HAPA

JOKETI,RICH,JB NA MAREHEMU ADAMU KUAMBIANA WAMEKUTANA MIKONO SALAMA CHEKI HAPA

MCHEKI GABO NDANI YA HIMAYA YA MACHOZI

KAMA BADO UJAIONA HAKUNA MATATA YA NISHA CHKI HAPA KIDOGO

Wednesday, 24 December 2014

NIVA AMEWAFATA SHILOLE NA SNURA KWENYE MUZIKI,CHEKI PICHA HAPA



Mcheza filamu za kitanzania Niva Zuber ameamua kuingia kwenye muziki na kuonekana kama amewafata wenzake Shilole na Snura ambao wanafanya vizuri kwenye muziki uku wakiachia nafasi kwa wengine kwenye filamu

STEPS KUTAMBULISHA FILAMU KATIKA MUONEKANO MPYA KWA MWAKA 2015



Kampuni ya usambazaji wa filamu bora Tanzania ya Steps Entertainment Ltd inatarajia kutoa bidhaa mpya za filamu kwa mwaka ujao wa 2015 filamu zenye ubora muonekano mzuri huku pia kuwaletea walaji bei rafiki kutoka kampuni bor a ya usambazaji wa filamu Tanzania StepsEntertainment Ltd.
Steps Entertaiment Ltd ni ilioanzishwa mwaka 2007 nchini Tanzania na makao yake makuu yako jijini Dar salaam, Kampuni ya Steps Entertainment inajishughulisha na usambazaji wa filamu za Kitanzania maarufu kwa jina la

 BONGO MOVIES
Tangu kuanzishwa kwake Kampuni ya Steps Entertainment imekuwa mdau mkubwa katika kukuza tasnia ya filamu nchini Tanzania na mpaka sasa ndiyo kampuni kubwa ya usambazaji wa filamu nchini Tanzania. 
Kampuni ya Steps Entertainment kupitia mikakati yake ya kuinua tasnia ya filamu nchini Tanzaania imefanikiwa kutoa ajira nyingi kwa wadau mbalimbali wa tasnia ya filamu, wakiwemo waandaaji wa filamu, Waigizaji, Wasambazaji wakubwa kwa wadogo, Wauzaji wa rejareja na wanaoonyesha na au kukodisha katika vibanda. 

Akiongea na wanahabari Carlos Johns Silondwa mtendaji mkuu ameielezea Steps Entertainment imefanikiwa pia kuvuka mipaka na kufikisha sinema za kitanzania katika mataifa mbalimbali ya nje na katika luninga za kimataifa na televisheni za ndani kuonyesha kazi za nyumbani.

“Kwa sasa mataifa mengi Ulaya na nchi za Scandinavia wanajifunza Lugha yetu ya Kiswahili kupitia filamu zetu, moja kwa moja utaona njia nyingine katika kukuza Kiswahili nje ya nchi kwa njia ya filamu tu ambazo zinasambazwa na kampuni hii, na kutengeneza ajira kwa vijana wengi,”

Pia kampuni imekuja na bei rafiki kwa mlaji baada ya kilio chake kuumiza kwa muda mrefu, kampuni kwa kutumia wataalamu pamoja na wadau wa filamu kutoka sehemu mbalimbali wamefanya utafiti ili kupata Mwarobaini wa Maharamia wa kazi za nyumbani kampuni imeshusha bei.
Hiyo inatokana na hali halisi filamu inatakiwa imfikie mtumia kwa 6,000/ lakini utafiti umebaini kuwa mtanzania anatumia zaidi kiasi cha 34,000/ na zaidi bila kuimiliki Dvd hiyo, baada ya Vibanda au Library kuanzimisha, badala ya kumuuzia. 

Filamu ambayo itauzwa ikiwa katika ubora na muonekano mzuri, inakuja baada ya filamu kutoka nje, kuuzwa kwa bei ya chini kabisa na kuleta ushindani pamoja na kuwa sinema hizo hazilipiwi kodi tofauti sana, nakuzifanya zinunulike sana kuliko filamu za ndani kutokana na bei yake kuwa ndogo.

 Kampuni ya Steps Entertainment ilifanya utafiti ili kujua ni jinsi gani filamu zinatoka mbali na bado zinawafikia walaji kwa bei ya chini ni baada ya utafiti huo ndipo Kampuni ya Steps Entertainment iliamua kujibana na kufanikiwa kuingiza na kufunga mtambo mkubwa wakisasa kuzalisha cd/dvd, kuzirekodi na kuziprinti hapa hapa nchini.

Tofauti  na siku za nyuma ambapo ilikuwa inaagiza cd/dvd kutoka nje ya nchi na kuja kuzirekodi tu, sambamba na mtambo huo pia kampuni hii imeamua kubuni kifungashio kipya yaani kasha za cd/dvd, ambayo ni za bei nafuu, zinamuonekano mzuri zaidi, ni rahisi kuhifadhi, nirahisi kusafiriha na nirafiki wa mazingira.

Mtambo mkubwa na wakisasa pamoja na kifungashio kipya vimepunguza sana gharama za kuzalishia nakala za dvd na cd na hivyo Steps imeona ni vyema kuonyesha moyo wa uzalendo kwa wateja wake  kwa kuwapunguzia bei ya kununua filamu kwa kuwauzia kwa nusu ya bei ya awali.

Kampuni ya Steps Entertainment inaamini kuwa kitendo cha kupunguza bei za filamu zake, kitawanyima Maharamia ulafi na wizi wa wazi kabisa, kama kampuni inakaribisha wadau wote wanaosambaza filamu kwa kuja kwetu kuzalishiwa filamu zao kwa bei rahisi sana ili huyu Gaidi mkubwa anayenyonya kazi zetu aache. 

·                     Kinaonyesha moyo wa uzalendo lakini pia kitapandisha mauzo ya filamu za kitanzania ambapo kwa ujumla wake itaongeza kipato kwa wasanii na kuchangia pato la Taifa.

·                     Kitapunguza uharamia wa filamu kwa kuwa bei itakuwa chini hivyo kila mtu atakuwa na uwezo wa kununua nakala halisi.
·                     Kitaziwezesha library zinazokodisha filamu kuacha kukodisha na badala yake kuanza kuuza moja kwa moja

 Hivyo basi Kampuni ya Steps Entertainment inamaliza mwaka 2014 na kuingia mwaka 2015 kwa kubororesha bidhaa zake, zikiwa katika ubora na muonekano wa kuvutia kwenye kasha la bahasha ngumu, bidhaa hizi zitamfikia mlaji kwa bei ya  1,500/= tu bei hii kwa filmu zitakazo kuwa katika kifungashio kipya pekee filamu zitakazo kuwa katika kifungashio cha zamani yaani kasha la plastiki zitaendelea kuuzwa kwa bei ile ile na wateja watakuwa huru kuchagua aina ya kifungashio pale wanaponunua nakala za filamu za Steps

Hivyo basi Steps Entertaiment imeanzisha kampeni maalum ya “Faidika na Steps kwa bidhaa bora, Wasanii nyota, na Filamu Bora”.
Kampuni ya Steps Entertainment  inawaomba wadau wote kuendelea kuzienzi filamu za kitanzania ili kukuza kipato cha wasanii na taifa kwa ujumla , kutangaza lugha ya Kiswahili na utamaduni wa kitazania.

Bei zetu zitakuwa wazi kwa maan za steps tofauti ya bei iliyoandikwa kwenye kasha ya kuonekana zikiwazimeandikwa katika kasha na mwananchi asikulaghai mtu wa Library eti usinunue hadi hakukodishe sema No.

Mwisho, Tunaiomba Serikali Chini ya Rais wetu Mpendwa Mheshimiwa Dr. Jakaya Mrisho Kikwete wawasaidie wadau wa filamu kupambana na uharamia wa filamu ambao kwa sasa umevuka mipaka wezi wanafanikiwa wasanii wanabaki Maskini.
MUNGU IBARIKI TANZANIA Mungu bariki Afrika 
Carlos Johns Silondwa 
Mtendaji Mkuu.


Monday, 22 December 2014

FILAMU YA HAKUNA MATATA IMETOKA LEO

Filamu ya Salma Jabu Nisha,inayokwenda kwa jina la Hakuna Matata imetoka leo chini ya kampuni kubwa ya usambazaji nchini Steps entertainment,

Filamu hiyo ambayo imeongozwa na muongozaji bora wa kike nchini Lamata na kupigwa picha na Kabuti Onyango imewashirikisha mastaa wengine kama vile Mau,Hemed,Tausi na Gwiji wa vichekesho nchini King Majuto

sio ya kukosa yani Hakuna Matata

Thursday, 18 December 2014

FILAMU YA SOZI NDOTO YA AJABU YAINGIA SOKONI

Kampuni ya usambazaji wa filamu nchini Steps Entertainment imeingizasokoni  filamu mpya ya Tino Muya inayokwenda kwa jina la Sozi Ndoto,

Filamu hiyo yenye stori nzuri ya kusisimua inapatikana kwenye maduka yote ya filamu nchini pata nakala yako halisi sasa

Saturday, 13 December 2014

SOMA ALICHOKISEMA Timoth Conrad Kachumia BAADA YA KUPATA TUZO UKO U.S.A

Nina masikitiko kidogo, nilitegemea wanasanaa wenzangu wangenipa sapoti kwa mafanikio haya ya kuipeperusha bendera ya nchi yetu nchini marekani, lakini imekuwa tofauti.
Ila Mama na Baba yangu walinambia "MWIKO KUKATA TAMAA" nitaipigania nchi yangu mpaka kieleweke, nafurahi marafiki zangu wa facebook, instagram, twitter mnanipa sapoti na kunitia moyo lakini huko mtaani kwa baadhi ya wenzangu du utasikia "aah anajifanya mjuaaaji eti limuvi lake limeshinda tuzo marekani basi ndio linajidaaai"
Anyway tungoje Diamond Apate tuzo nyingine ndio tukampokee tena airpot kwa shangwe na vigere gere.
Kwa wale watu wangu wanguvu napenda niwape taarifa kuwa ndugu yenu naingia tarehe 16 siku ya jumanne saa saba kamili mchana. Mkipata nafasi msisite kuja kunipokea na LITUZO LANGU MKONONI.
Asante sana.
We Make We Believe.

MTUNISY: Siku Hizi Mtu Akikuumiza Nawe Muumize Tu Mradi Mugawane Maumivu

Tugawane Maumivu ndio jina la filamu mpya iliyotoka hivi karibuni kutoka kwa muigizaji na muongozaji wa filamu, Nice Mohammed  maarufu kama Mtunisy. Akizungumzia maendeleo ya kazi hii sokoni, Mtunisy aliwashukuru mashabiki na wapenzi wote waliomuunga mkono kwa kununua kazi yake na kuwaomba waendelee kumuunga mkono.

 “Ahasanteni wapendwa kwa sapoti yenu kubwa mlioionyesha kwa kununua film yangu mpya hakika nimeamini huwezi kuchukiwa na wote hii imedhihilisha ktk kz yangu hii ya TUGAWANE MAUMIVU na kuifanya iwe ndio habari ya mjini kwa sasa nawaomba endeleeni kuniunga mkono wapendwa mungu awabariki sana amen”.
Mashabiki wengi waneonyesha kuipenda na kuikubali kazi yake hii  kwani ina dhana mpya ambayo imewagusa wengi, akizungumzia mrejesho huu Mtunisy alisema
“Nashukuru ndugu zangu siku hizi mtu akikuumiza nawe muumize tu mradi mugawane maumivu iweje yeye akuumize na asiumie bwana!tuumizane tu habari ndio hiyo”.
Hiyo ndio dhana nzima ya filamu hiyo ya Munisy, TUGAWANE MAUMIVU ambayo imejumuisha wakali kama, Chuchu Hans, Rammy Galis, Mukly Ismail na Nice Mohammed mwenyewe. imefanyika chini ya STEPS ENTERTAINMENT.
Jipatie nakala yako halisi kumsapoti wasanii wetu wa Tanzania.

Tuesday, 9 December 2014

Kuwa wa kwanza kuona filamu ya Jina Langu hapa inasambazwa na steps entertainment

FILAMU YA JINA LANGU KUFUNIKA SOKO LA FILAMU NCHINI

 Filamu ya Jina Langu iliyochezwa na wasanii chipukizi kutoka mkoani Dodoma inasubiliwa kwa hamu kubwa na wadau wa filamu nchini kwani imechezwa kwa kiwango kikubwa sana
 Akifunguka kiafrika bila hofu yoyote muandaaji wa filamu hiyo Sulesh Mara amesema filamu hiyo imechezwa na wasanii kutoka kanda ya kati ambao wanauwezo mkubwa sana kisanaa
Filamu hiyo inatoka hivi karibuni na inasambazwa na kampuni ya steps entertainment usikose nakala yako sasa

ZAMARADI NA JB WAJIBISHANA INSTAGRAM CHANZO KIKIWA NI FILAMU ZA BONGO


leo asubuhi kupitia mtandao wa Instagram mtangazaji wa kipindi cha take one na movie leo ndani ya Clouds media ameshindwa kuficha hisia zake kwenye tasnia ya filamu na kuandika haya
"
Natamani sana siku moja atokee mtu kwenye hii sekta atutambulishe hata kama sio kimataifa basi africa tu... R.I.P KANUMBA alianza kuonesha mwangaza na juhudi binafsi zilionekana na kila mtu aliona huenda angefika mbali.. lakini baada ya hapo sioni tena!!!!
Mbona hapa nyumbani ni wakubwa tu..? Nini kinawakwamisha..?  Kwanini wasanii wetu wa filamu ukubwa wao unaishia nyumbani tu....!!? Tatizo ni nini!!!????? kiukweli ni kama inakatisha tamaa na inaonekana kabisa watu wamerelax na ustar wa bongo wakati wana nafasi ya kufanya vizuri zaidi... wana bongo movie tukifika kwa wenzetu unaona kabisa tunapwaya kiasi gani.. Ujanja wetu ni nyumbani tu!!?? why!!!?? tukianza utanzania wa kufichaficha tutasifiana uongo lakini tukiwa wakweli na nafsi zetu tutaliona hilo na kuchukulia kama challenge..!!! ukweli ni kwamba hii tasnia inasikitisha!!! tena sana.. nahisi sasahivi tunafanya filamu kwa ajili ya nyumbani tu na tukiingia kwenye mabendi tukisharushwa tumeridhika!! kweli!! hapa ndio mnapotaka mfike!!? ukifika sehemu ukiwa juu nchini kwako tunachotegemea ni wewe kupasua mawimbi uende mbali zaidi nje ya mipaka!! lakini ukiamua kurelax hapo ulipo inamana unasubiri kushuka sababu kiukweli huwezi kukaa juu milele!!! kwanini mmeridhika hivi!!! kaka JB tatizo ni nini!!!??
Mi nakuangalia wewe kama mfano wa msanii mkubwa sana kwenye tasnia kwa sasa... mbona umerelax!!!??? umeridhika na ustar wa tanzania!!!? una kila kitu cha kukufikisha mbali... kinachohitajika ni juhudi binafsi tu ili kesho na sisi tufike mahala pazuri!! hebu tuongee wapenzi.. mnahisi huku kwenye bongo movie TATIZO LIKO WAPIII…!!???

Baada ya maelezo hayo ya Zamaradi JB na yeye aliamua kumjibu mtangazaji huyo kupia ukurasa wake wa instagram

“Kwako Zamaradi na wengine wote.

Kwanza napenda niwashukuru wote kwa jinsi mnavyotuwazia mema. Naomba nichukue nafasi hii kuwapongeza waigizaji wote wa Tz na waandaaji wa filamuU kwa kuthubutu kutengeneza filamu hizi katiks mazingira magumu. Najua watanzania wengi wangependa kuona tukipeperusha bendera nje,lakini naomba muwape wasanii muda.
Tasnia hii ni changa na ina changamoto ambazo zinakatisha tamaa. Hebu tujiulize kwa nini wasomi wengi waliosomea filamuu UDSM na BAGAMOYO hawafanyi filamu hizi? Wasambazaji wengi wakubwa mamu,wananchi na hata hans pop walijaribu wakakimbia, kuna producer mkubwa hapa nchini JOHN RIBER ambaye ametengeneza filamuu kama NERIA na YELLOW CARD lakini naye ukimwambia njoo kwenye hizi filamu atakupa jibu.
Nakubali tuna makosa mengi kama ubora wa filamu zetu na stori lakini nataka niwaambie mazingira ya kufanya filamu bongo yanakatisha tamaa wizi wa kazi zetu umezidi na wasambazaji wengi wamekimbia. Binafsi najipanga kuwa mtayarishaji zaidi kuliko mwigizaji kwa sasa kupitia JERUSALEM FILMS na ndio maana filamu nyingi natoa nafasi kwa vijana ambao kama mabadiliko ya sera ya filamu yatafanywa watatuwakilisha nje.
Kiswahili kisichukuliwe poa kwani kina nafasi kibwa sana. Tukumbuke SHARUK KHAN ni ‘actor’ tajiri2 dunian lakini filamu zake ni za kihindi. Hebu sote tusaidiane kupambana na changamoto hizi na tuanze na EAST AFRICA kwanza huku tukiboresha, wasomi wa filamu msikimbie njooni tuanze wote na tuwape moyo wasanii wetu waliojaribu kusimamisha tasnia hii kwa vimtaji toka mifukoni mwao na vipaji walivyopewa na mungu bila msaada kutoka popote. Asanteni kwa kutuunga mkono kwemye filamu zetu.”

Monday, 8 December 2014

FILAMU MTUNIS,TUGAWANE MAUMIVU YAINGIA SOKONI LEO

 Filamu ya mtunis inayokwenda kwa jina la Tugawane maumivu imeingia sokoni leo ikisambazwa na kampuni ya steps entertainment.
Filamu hiyo imechezwa na wasanii wenye majina makubwa nchini kama vile Rammy Galis,Chuchu Hansi na Esha Buheti
Filamu hii yenye kisa cha kimapenzi ambacho kimechezwa kwa kwa umakini mkubwa inapatikana kwenye maduka yote Tanzania wai nakala yako sasa

Saturday, 6 December 2014

WATANZANIA WALILIA ADAMU KUAMBIANA KWENYE FILAMU YA LIKWATA

 Filamu ya Likwata iliyoingia mtaani ijumaa hii imewapa wakati mgumu mashabiki wa filamu Tanzania baada ya kuona jinsi marehemu Adamu kuambiana alivyoitendea haki filamu hiyo na wengine wamefika mbali na kusema mungu amemchukua mapema sana msanii huyo aliekuwa kivutiao kwa wengi kutokana na busara zake.
Kwenye filamu hiyo yumo pia mcheza filamu mwenye jina kubwa uswahilini wakiamini kuwa ndio anaongoza kwa kuchamba kwenye filamu Riyama Ally uku pembeni akiwepo kaka mtanashati Niva na wasnii wengine wengi

Kama kweli we ni mpenzi wa filamu za kitanzania nunu nakala halisi uone jinsi marehemu Adamu Kuambiana alivyowaliza watu kwenye filamu hii ambayo ni moja kati ya filamu za mwisho kabisa kwa mkongwe huyo kucheza

Thursday, 4 December 2014

Happy birthday kwa kaka yetu JB. Swahili filamu tunakuombea uishi maisha marefuuuuu...!

Mwakani panapo majaliwa ya mwenyezi mungu mwezi wa kwanza anatarajia kuachia filamu mpa inayokwenda kwa jina la mzee wa swagga akiwa na wasnii nyota kama Wastara,Tea,Welu sengo na Grace kabitwa kutoka nchini Zambia