Tuesday 11 November 2014

RAMY GALIS;MASIKINI HANA THAMANI KWENYE ULIMWENGU WA KIFALME

 Mcheza filamu Ramy Galis anaekuja juu kwa hivi sasa hapa nchini anatarajia kuachia filamu yake mpya ya Vocha mapema jumatatu ijayo,kwenye filamu hiyo amecheza na Hemedy Suleimani pamoja na Hamisa Mobeto na wasanii wengine wengi wenye uwezo mkubwa
Akipiga stori na blog hii Ramy amesema filamu hiyo ni tofauti na filamu zote zinazoandaliwa na wacheza filamu waliowengi kwani mpangilio wa matukio upo tofauti sana

'mimi nimepanga matukio tofauti sana ukiangalia sehemu ya kwanza ya filamu hii na sehemu ya pili kunautofauti sana japo stori ni moja'

Filamu ya Vocha inatarajia kuingia sokoni tarehe 17 mwezi huu na inasambazwa na kampuni kubwa kabisa ya filamu Tanzania Steps Entertainment.

No comments:

Post a Comment