Tuesday 11 November 2014

WEMA NA PENNY WAPATANA

WEMA, PENNY WAPATANA
HATIMAYE mastaa wawili wakubwa Bongo, Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu na Mtangazaji wa Redio EFM, Peniel Mungilwa ‘Penny’ wamepatana baada ya kuwa katika bifu kwa kipindi kirefu, chanzo kikiwa ni penzi la Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’.

Habari za ndani zinaeleza kuwa wawili hao walipatanishwa na mdau mkubwa wa burudani, Jennifer Pemba kwenye sherehe ya siku yake ya kuzaliwa iliyofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita katika Ukumbi wa East 24 Bar and Grill uliopo ndani ya Hoteli ya Sea Cliff, Masaki jijini Dar es Salaam ambapo wawili hao walialikwa.

No comments:

Post a Comment