Saturday 22 November 2014

BATULI KUOLEWA SOON

GOOD news kwa mtoto mzuri Bongo Movies, Yobnesh Yusuf ‘Batuli’ ni kwamba anatarajia kuolewa hivi karibuni baada ya kuishi maisha ya upweke kwa muda mrefu, Risasi Jumamosi linakujuza.

Batuli ambaye ni mama wa watoto wawili, amesema kuwa kwa umri alionao, amejifunza vitu vingi katika maisha hivyo kwa kuwa ameshampata mtu sahihi kwake, ameona bora aolewe.
Amesema katika safari ya maisha, vikwazo ni vingi ikiwemo masuala ya skendo za wasanii lakini ameshavuka vikwazo hivyo na hahitaji tena kuyumbishwa na mtu kwani anaingia kwenye ndoa akiwa ameshajifunza mengi.
“Ndoa siyo kitu cha mchezo tena kwa sisi wasanii mambo ni mengi. Kazi yetu tunakutana katika mazingira mbalimbali hatarishi na wadau tofauti, vikwazo ni vingi na mtu akivuka salama basi ni jambo la kumshukuru Mungu,”  

No comments:

Post a Comment