Friday 7 November 2014

TIKO WA BONGO MOVIE ABONDWA

 STAA wa filamu za Kibongo, Tiko Hassan, hivi karibuni alionja joto ya jiwe baada ya kushushiwa kipigo kizito na hawara wake aliyetajwa kwa jina moja la Ally.
Kwa mujibu wa chanzo makini, siku ya tukio Tiko alikuwa na Ally nyumbani kwake, Mwananyamala ndipo ghafla hali ya hewa ikachafuka baada ya pedeshee mmoja kumpigia simu mwigizaji huyo.
“Mzozo ulianzia kwenye simu na huwezi amini amemvunjia simu yake kwani alimpiga kwa sababu alikuwa akiongea na mwanaume mmoja kimahaba na hapo ndipo timbwili lilipoanza,” kilidai chanzo hicho.
Kikazidi kumwaga ubuyu kwamba, wakati kipigo cha ngumi kikiendelea, mwanaume huyo alimrushia chupa Tiko ambayo ilimpasua usoni na kumuacha na jeraha kubwa lakini hakwenda kumshtaki polisi kwa kuwa anampenda sana.

No comments:

Post a Comment