Tuesday 4 November 2014

NIVA AMEANZA KUFATA NYAYO ZA MAREHEMU KANUMBA KWENYE FILAMU

 Mcheza filamu za kitanzania Niva Zubery ameonesha kuwavutia mashabiki wake kwa kile anachofanya kwenye filamu zake kwa kuwatumia wasanii wenzake wa kikundi cha Jumba la Dhahabu na kupelekea mashabiki kuvutiwa na kazi zake na kumtabili uenda akariziba pengo la marehemu Kanumba kwani ameonesha nia ya kufata nyayo zake

 Kanumba mara kwa mara kwenye filamu zake alikua anatumia wasanii wenzake kutoka kikundi cha Kaole kitu amabacho anakifanya Niva kwa hivi sasa kwenye filamu zake.

Pia Niva amekua akibadilika kila mara kama alivyokua anafanya Kanumba kwa kucheza uhusika wa sehemu yoyote jambo ambalo linamfanya ajiongezee mashabiki wengi

Ukiangalia filamu yake ambayo inasumbua kwa hivi sasa nchini ya Najuta Mie ambayo amecheza na  Nikita na Mam tei ambao ni zao la tamthilia ya Jumba la Dhahabu utagundua msanii huyu ni miongoni mwa wasanii watakaofika mbali sana endapo akizidi kujituma zaidi na kuwa na heshima kwa mashabiki

Filamu ya Najuta Mie ip madukani Tanzania nzima itafute uone utofauti na uwezo mkubwa alionao mcheza filamu Niva Zubery

No comments:

Post a Comment