Friday 14 November 2014

AUNT, ODAMA WATIMULIWA BONGO MOVIE

UPEPO mbaya unaendelea kuvuma ndani ya Klabu ya Bongo Movie Unity! Safari hii umewakumba mastaa wakubwa klabuni hapo, Devotha Mbaga, Aunt Ezekiel na Jennifer Kyaka ‘Odama’ ambao wanadaiwa kutimuliwa kundini kwa sababu ya kujiweka karibu na mwenyekiti wa klabu hiyo aliyejiuzulu, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’.
 uongozi ambao ulibaki madarakani kundini baada ya Steve kujiuzulu, ulifanya tathmini upya ya memba waliobaki kisha kuwachuja hadi kubaki na wasanii 20 pekee wenye sifa

“Wamewaengua baadhi ya wasanii ambao wameona hawana sifa ya kubaki kundini, miongoni mwao ni Devotha, Aunt na Odama. Wamesema wanahitaji mastaa wenye msimamo siyo kujipendekeza upande wa Steve, siku si nyingi watayaanika majina ya wenye sifa za kubaki kundini,”  

Baada ya habari hiyo walivyotafutwa MASTAA wanadaiwa kutimuliwa  haya ndio wameyasema 

Odama: Hakuna kitu kama hicho, wanaoenguliwa ni viongozi siyo wanachama, watanienguaje bila kunipa taarifa? Kwanza ndiyo nasikia sijui chochote ndiyo napata taarifa kutoka kwako.
Kwa upande wa Aunt Ezekiel, simu yake iliita bila kupokelewa.

No comments:

Post a Comment