Wednesday 28 January 2015

JB:FILAMU YA MZEE WA SWAGGER NI ZAWADI KWA MASHABIKI WA WASTARA,CASSIE KABWITA,THEA NA WADAU WOTE WA FILAMU POPOTE DUNIANI


Mcheza filamu mwenye jina kubwa nchini Jacob Stephen amewakutanisha Wastara,Thea na Cassie kwenye filamu yake mpya ya Mzee wa Swagger baada ya mashabiki wa mastaa hao kumsumbua kwa muda mrefu wakitaka kuwaona kwenye filamu zake

Jacob amesema amekuwa akiwasikiliza sana mashabiki wake na kuwapa vitu wanavyovitaka ndio maana amewatendea haki kwa kukubali maombi yao,kupitia ukurasa wake wa instagram amesema


"WADAU WA JERUSALEM MNAKUMBUKA NILIOMBA MCHAGUE WAIGIZAJI WA MOVIE YANGU MPYA.TAYARI NIKO ARUSHA NA BAADHI YAO.KISHA TUTAENDA DODOMA,ZANZIBAR, NA TUTAMALIZIA DAR.ASANTENI"

Akiwa na maana ya Wastara,Thea na Cassie kabwita kutoka Zambia

Kwenye filamu hiyo inayotarajiwa kuingia sokoni kesho pia yumo mwana dada Welu Sengo amabae nae ameonesha uwezo ,mkubwa 

Filamu hiyo inasambazwa na kampuni kubwa ya steps entertainment na kwa mtu yoyote aaneitaka basi awasiliane kwa namba +255716 788 805 na +255713570 581  au atembelee kwenye duka kubwa la kampuni hiyo Kariakoo mtaa wa Msimbazi ana Masasi jijini Dar es salaam

No comments:

Post a Comment