Tuesday 6 January 2015

WASTARA ALIA MASTAA KUSUSIA KISOMO CHA SAJUKI

 DIVA wa filamu Bongo, Wastara Juma amelia na mastaa wenzake wa filamu kususia kisomo cha marehemu mumewe, Juma Kilowoko ‘Sajuki’.
Msanii huyo mwishoni mwa wiki iliyopita aliandaa kisomo cha kumuenzi marehemu Sajuki ambapo dua ilianzia kwenye makaburi ya Kisutu alipozikwa na kumalizika nyumbani kwake maeneo ya Tabata Barakuda jijini Dar.


mwanadada huyo ambaye alionekana akiangua kilio kizito kwenye kaburi la mumewe huyo alisema, kamwe kwenye maisha yake hataacha kumlilia Sajuki sababu ndiye mwanaume pekee aliyemuonesha upendo wa kweli na kujivunia thamani yake kama mwanamke anayeishi kwenye ndoa.
Kuhusu mastaa kususia kisomo hicho, Wastara alisema;
 “Hilo nililijua mapema sababu hawa wasanii wenzangu mambo ya maana hawapendi kabisa, hapa ungewaalika kwenye sherehe yenye pombe wangefika kwa wingi lakini suala la dua wameona tabu sana kuja, nimeshazoea siwezi kulipa kisasi kwa yeyote yule nitajumuika nao kama kawaida japo jambo hili limenikwaza mno.”
Baadhi ya mastaa waliofika katika kisomo hicho ni Davina, Sandra, Vanitha, Frank, Nisha na Mtitu.

No comments:

Post a Comment