Monday 12 January 2015

SOMA ALICHOKISEMA FACEBOOK MTANGAZAJI BOND BI SINAN KUHUSIANA NA KAMPUNI YA KUSAMBAZA FILAMU YA STEPS ENTERTAINMENT

Mtangazaji wa kipindi cha Action and cut Bond Bin Sinan ameweka wazi msimamo wake juu ya wasanii kuonesha hawakubaliana na steps kwa kushusa bei za filamu zake kupitia ukurasa wake wa facebook amesema hivi

 Kwakweli mi nawashangaaa saana wasanii wa Tanzania hivi ugomvi na Steps huwa unatoka wapi? Steps hana anaemlazimisha kufanya nae kazi kila mtu anakwenda kwake kwa ajili ya kufanya nae biashara na sio lazima ufuate anavyotaka yeye kwa sababu masuala ya mikataba no baina mtu na mtu kama ukiona huridhiki basi unaangalia sehem nyingine.
Nashindwa kuelewa ugomvi unatoka wapi kwa sababu.
Wasanii wenye hali nzuri kipesa wanafanya kazi na Steps
Msambazaji anaesambaza sehem kubwa ya Tanzania na nje ni Steps
Msambazaji anaeongoza kulipa kodi kubwa kupita biashara zote K.koo ni steps na ni kupitia Filamu
Msambazaji anarngoza kulipa vizuri akinunua filamu ni Steps
Msambazaji anaefanya promotion na matangazo ya kazi za filamu ni Steps
Msambazaji pekee mwenye kiwanda chenye muundo wa usambazaji ni Steps
Msambazaji aliechukua tuzo ya msambazaji bora afrika na mwenye kukuza tasnia ya filamu afrika ni Steps
 Msambazaji anaetoa filamu nyingi kwa mwezi kuliko wengine ni Steps anatoa filamu 10 kwa mwezi.
Sasa ubaya wa huyu mtu uko wapi?
Hebu tizameni wasambazaji wengine kama PapaZii, Gmc, Firs Quality, Bajomba, BekNet, B4U, Femous Video mpaka nw Proin Na PiliPili wamefanya nini na wako wapi? Msambazaji kama pilipili ananunua filamu za watu mpaka kwa Milioni moja na nusu kweli. Sasa tukimuondoa Steps ndio nani aiokoe Tasnia hii?
Tunapaswa kupamban na serikali ndio inatusababishia wasambazaji wanakufa kila kukicha kwa sababu ya uharamia. Huwezi niambia nchi kubwa kama hii ya tanzania yenye watu Milioni 47 eti unauza nakala elfu 50 tu
 Hakuna Sera ya filamu
Hakuna sheria za kulinda
Hakuna mahakama ya kushitaki
Wala hakuna chuo cha kujifunza mambo ya filamu
Hayo ndio matatizo yanayotusumbua na sio Steps Tubadilikeni maana watoto wetu wameanza kukua na wanasoma sasa watakuja kuona umbumbumbu wetu.
Kuhusu suala la bei kabla sijakujibu nikuulize maswali kumi hivi
1. Je Mtanzania wa kima cha chini yaani dola moja kwa siku ambayo ni elfu moja namia saba anaweza kununua filam kwa shilingi elfu sita?
2. Je ni halali katika nchi zenye watu milioni 170 nazungumzia (Est and Central Afrika) kuuza nakata elfu 50?y
4. Je unaweza kushindana na filamu za nje zinazouzwa shilingi 1500 na hazina stika wala hazikaguliwi wala hazina kodi huku zikiwa na kiwango cha juu na mastaa wa dunia na zimetafsiriw na Lufufu?
5. Je filamu hizi haziuzwi na wezi kwa shilingi 1000 huko buguruni. Tandika na Tanzania nzima?
6. Je ni halali kwa mtu anaekuibia akauza kwa shilingi elfu moja na akapata faida na wewe mwenye mali usiuze kwamba utapata hasara?
7. Je nisawa kuendelea kuwa na wasambazaji wanaopigania kuuza copy elfu 20 na kukataza njia na akili za wale wanaotaka tuuze copy laki 5?
8. Je wasambazaji wadogo wadogo wanauwezo wa kununua filamu kwa mil.50?
9. Na kama wanaweza kuproduce hizi za cover kwanini washindwe kuproduce za box ili kupunguza gharama za uzalishaji?
10. Wewe na familia yako umewahi kununua filamu ngapi?
11, je kuna library ngapi tanzania zinazokodisha filamu ambao bei ikishuka zitaanza kuuza
12. Na hao wasambazaji wadogo wananunua filamu au wanatengeza wao?

Na nyongeza hii
Je faida ya shilingi 600 kwa cd na kuuza nakala elfu 20 na ulinganishe faida ya shilingi 200 kuuza nakala laki 250 tu ipi nyingi?
Wasambazaji wadogo wanataka Tasnia hii Idumae kila kukicha waendelee kuwatumia wasanii kuwalipa kucheza filamu zao wanaogopa kuwa zikishuka watatakiwa kuwa na uwezo wa kuzalisha nakala kuanzia laki mbili na hawana hela maana kama nakala moja itakuwa na gharama ya shilingi 600 × 200,000= 120, 000,000/= sasa hofu yao ni watakufa
Kwa mtazamo wangu kama hawana mitaji hatakiwi kuwepo kabisa kwa sababu kama leo tasnia hailipi na tunaona makampuni yanakuja je ikianza kulipa? Tunahitaji watu watakao saidia tasnia ihakikishe tunauza nakala zaidi ya milioni kwa sababu ndio sehemu pekee tunapoingizia pesa tofauti na Holywood na Bolywood wanaingiza pesa kwenye majumba cinema kwanza.
Wapo watu wengi tu na wanapesa na wanatafuta pa kuzifanyia kazi faida ikionekana wawekezaji wa viwanda kama cha Steps au zaidi yake watakuja.

Kitu kingingine kama wauzaji wa filamu za nje wanaleta makontena ya filamu kutoka China na kisha wanauza kwa jumla shilingi 750 na faida wakaipata je kwanini sisi tushindwe kupeleka master zetu China tukaja kuuza kwa bei ya 1000 kwa jumla?
Tatizo lililopo hata hao wasambazaji wadogo wadogo ukiwauliza tudanye nini ili tuuze zaidi ya hapa hawana jibu la msingi zaidi ya kuitukana Steps na watu wanaofanya kazi nao na ni Kwa sababu
Steps anaugomvi na Mtitu watu wote wanajua.
Kwa sababu Bongo movie wanabiff na TAF na Bongo movie wanafanya kazi na steps walio wengi.
Hapa kuna bif za kimaslahi tu na uoga wa biashara.
Lakini ukiangalia kwa ufupi tu utakuta
Wanatumia kivuli cha Tasnia kuwadanganya Watu.
Mfano mdogo tu.. Iwapo wasambazaji wanauza shilingi 1600 kwa jumla na cd moja wanatengeza kwa shilingi 850 hivyo wanafaida ya shilingi 750
Na muonekano wa cd ya shilingi 1000 gharama za utengenezaji ni shilingi 700
Sasa basi cd ambazo wanauza shilingi 1600 wanasambaza nakala elfu 30 maxmum
Lakini hizi za 1000 watauza nakala mpaka laki 5.
Hivyo faida ya shilingi 750 mara Cd elfu 30 milioni kama 25
Na huku kwenye faida ya 350 mara laki 5 ni karibu miliono 150
Sasa iko wapi faida kubwa?
Ukipata faida ndogo lakini ukauza kwa wingi ni bora kuliko kupata faida kubwa na ukauza kidogo.
Nadhani kwa waliosomea biashara wanaelewa hili.
By Bond Bin Sinnan

No comments:

Post a Comment