Friday 23 January 2015

Ray – “Mwaka huu filamu za nje tu, ni mwendo wa Ghana na Nigeria”

Msanii mkongwe wa filamu nchini, Vicent Kigosi a.k.a Ray amejipanga kufanya filamu nyingi za kimataifa mwaka huu, huku akiweka bayana ataanza na Ghana pamoja na Nigeria.
Kwa mujibu wa tovuti Bongo5 , Ray amesema ndani ya mwaka huu ataweka pembeni kazi za ndani na kujikita kimataifa zaidi.
“Nimepanga kufanya mambo mengi mwaka huu, lakini mwaka huu movie zangu zote nitafanya International sitafanya movie yoyote ya hapa hapa kwa sababu kama hapa nishafanya sana, kwahiyo movie zangu zote nitakazocheza mwaka huu 90% nitacheza nje, kwahiyo kama kuna lolote ambalo litabadilisha nitawajulisha, ni mapema sana kusema lakini kitu ambacho ninaweza kuweka wazi ni nitaanza kazi na Nigeria na Ghana, ndani ya mwezi wa nne nadhani kazi zitakuwa zimeanza,” alisema Ray.
Mipango hii ya Ray inaonekana kja baada ya mwanadada Wema kwenda Ghana na kufanya filamu na Van Vicker.

No comments:

Post a Comment