Thursday 22 January 2015

Dude akubaliana na bei ya Tshs. 1500 kwa filamu. Asema ndio njia pekee ya kupambana na uharamia.

Masanii wa filamu nchini Dude, amefunguka kwa kusema kuwa kwa kuwa serikali imeshindwa kupambana na wezi wa kazi za wasanii ni bora bei ya Steps Tsh 1500 iyendelee ili kuiyokoa tasinia hiyo.
Dude ameiambia tovuti ya Bongo5 kuwa hakuna njia kwa sasa ya kuweza kupambana na maharamia wa kazi za wasanii zaidi kushusha bei ya filamu.
“Tumeshindwa kuwathibiti pirates, watu wanasambaza kazi, wanauza kazi kwa bei rahisi, leo hii ukienda Buguruni unapata kazi kwa elfu mbili, elfu moja mia tano, filamu ambayo wewe unaiuza dukani elfu tano wenzako wanauza elfu mbili, kwakuwa watanzania wengi ni masikini hawawezi kwenda kununua kazi elfu tatu dukani wakati anaweza kupata kazi hiyo hiyo mtaani kwa elfu moja na mia tano. Kwahiyo hicho ndo kinachotuua sana sana, mimi kwa upande wangu kwakuwa serikali imeshindwa kutokomeza pirates, mimi naona steps kushusha bei ni sawa kwa sababu 

tunapambana na pirates, watanzania ambao wanaishi chini ya dola moja ndo wanunuzi wa kazi zetu, sisi kazi zetu hazinunuliwi na watu wa Masaki, watu wetu ni wa Mwananyamala, Magomeni, Gongolambo watu ambao wanakipato cha chini, sasa mtu kama huyo kweli atumie elfu tano yake anunue filamu? Ni wachache wanafanya hivyo ndiyo maana wanakimbilia kununu za bei ya chini, kwahiyo mimi steps naona wamechukua uwamuzi mzuri ambao una manufaa kwetu na kwao pia,” alisema Dude.

No comments:

Post a Comment