Thursday 15 January 2015

SALMA NISHA:NAOMBA STEPS ISHUSHE BEI YA FILAMU ILI WANAOKODISHA WAACHE NA WAANZE KUUZA FILAMU NA KUPATA FAIDA BADALA YA KUKODISHA


Mcheza filamu za kitanzania Salma Jabu Nisha ameelezea hisia zake juu ya kampuni ya Steps Entertainment kwa atua yake ya kushusha bei za filamu nchini

Kupitia ukurasa wake wa facebook Nisha ameandika hivi


Kikao cha kuhusu maswala ya bei za filamu kinatarajiwa kuanza hivi punde chini ya wizara 3 ambazo ni wizara ya habari michezo na utamaduni, wizara ya viwanda na biashara na wizara ya fedha.
Kwa msimamo wangu kama mfanya biashara wa filamu na msanii Tanzania,napendekeza bei ishuke ili watu wote wawe na uwezo wa kununua,haiwezekani tuwauzie mashabiki filamu kwa elf 3 wakati elf 1500 pia tunapaa faida,kwanini mununue filamu kwa bei kubwa filamu iliyokatwa katwa ambayo 

unaweza ifanya iwe part 1? Huo ni wizi wa wazi wazi @stepsentertainment imeleta vifaa vya kuzalisha kazi hapa nchini faida inapatikana kwanini tuuze bei kubwa?ili kunufaisha pirates wanaouza 500 kwa kazi za kuiba,kila siku tunapigana na pirates (wizi wa kazi za wasanii)lkn bado wapo,leo kushusha bei kwa nia ya kuzuia kuibiwa msanii na mnunuzi kuna wanaopinga,Natamani bei ishuke ili hawa wanaokodisha waanze kuuza wapate faida na wao,na wanao zikodi waanze kununua.
Ni aibu kubwa kwa tasnia kama hii kuuza nakala elfu 20 tu wakati watanzania tupo zaidi ya ml.47,sio kwamba haiuziki inauzika sana ila wanaofaidika ni wale wanaoiba.

No comments:

Post a Comment