Thursday, 29 January 2015

FILAMU YA MZEE WA SWAGGA YAINGIA SOKONI LEO

 Filamu ya Jacob Stephen inayokwenda kwa jina la Mzee wa swagga imeingia sokoni leo,filamu hiyo iliyochezwa Arusha,Zanzibar,Dodoma na hapa Dar es salaam imewajuisha wacheza filamuw enye majina makubwa Afrika mashariki akiwemo Wastara Juma,Welu Sengo,Cassie Kabwita pamoja na Ndumbagwe Misayo maarufu kama Thea
JB amesema filamu hiyo inaelezea kwamba kila mtu anamaisha amabayo anayapenda pengine yanaweza kuwakwaza wengine lakini hayo ndio yakawa maisha yake poleni wote niliowaumiza mzee wa swaga

filamu hii imetoka na inasambazwa na steps intertainment pata nakala yako sasa

Wastara Awa Balozi Wa Medo Katika Kuchangia Elimu


 Mwigizawa filamu Bongo, Wastara Juma,  jana amepata heshima baada ya kupata nafasi ya  kuwa balozi wa Morogoro Education Devolopment Organization (MEDO) kwa ajili ya kuchangia elimu kwa watoto wa kike.
Hafla hiyo fupi ilifanyika  katika ukumbi wa Hotel ya Tamal, jijini Dar, ambapo Wastara alisaini mkataba wa kazi hiyo rasmi inayohusu uchangishaji wa fedha kwa jukumu hilo ambapo kaulimbiu yake ni  ‘500/= Yatosha Kunipa Elimu’.  Namba ya  uchangiaji katika mfuko huo kwa wenye nia ya kufanikisha mradi huo ni 0713  834540, 0787 747327 na 0769 224726.
PICHA: Meneja wa mradi huo, Bertha Gama (kushoto) na mwenyekiti wake Silas Masui (katikati) wakiwa na Wastara Juma.
Hili ni jambo jema na la mfano, tuwaunge mkono.

Wednesday, 28 January 2015

JB:FILAMU YA MZEE WA SWAGGER NI ZAWADI KWA MASHABIKI WA WASTARA,CASSIE KABWITA,THEA NA WADAU WOTE WA FILAMU POPOTE DUNIANI


Mcheza filamu mwenye jina kubwa nchini Jacob Stephen amewakutanisha Wastara,Thea na Cassie kwenye filamu yake mpya ya Mzee wa Swagger baada ya mashabiki wa mastaa hao kumsumbua kwa muda mrefu wakitaka kuwaona kwenye filamu zake

Jacob amesema amekuwa akiwasikiliza sana mashabiki wake na kuwapa vitu wanavyovitaka ndio maana amewatendea haki kwa kukubali maombi yao,kupitia ukurasa wake wa instagram amesema


"WADAU WA JERUSALEM MNAKUMBUKA NILIOMBA MCHAGUE WAIGIZAJI WA MOVIE YANGU MPYA.TAYARI NIKO ARUSHA NA BAADHI YAO.KISHA TUTAENDA DODOMA,ZANZIBAR, NA TUTAMALIZIA DAR.ASANTENI"

Akiwa na maana ya Wastara,Thea na Cassie kabwita kutoka Zambia

Kwenye filamu hiyo inayotarajiwa kuingia sokoni kesho pia yumo mwana dada Welu Sengo amabae nae ameonesha uwezo ,mkubwa 

Filamu hiyo inasambazwa na kampuni kubwa ya steps entertainment na kwa mtu yoyote aaneitaka basi awasiliane kwa namba +255716 788 805 na +255713570 581  au atembelee kwenye duka kubwa la kampuni hiyo Kariakoo mtaa wa Msimbazi ana Masasi jijini Dar es salaam

Monday, 26 January 2015

JB:Baada kufanya kazi na Thea, Wastara na Wellu, pendekeza nani tufanyenae kazi tena?..soma vigezo

Muigizaji na muongozaji wa filamu, Jacob Stephen  “JB”aliweka bandiko hili mtandaoni, tumeona sio mbaya kulukuletea hapa na wewe uchangie. Nakuu;
“Wakati naanda mzee wa swaga niliomba mapendekezo mkachagua wengi hatimaye tukawapata Thea,Wastara na Wellu nakubali mapendekezo yenu sana.
Lakini sera ya kampuni ni kujaribu kuwapa nafasi wasanii ambao wana majina lakini sio makubwa ila wana vipaji ili tutengeneze mastaa wengi.
Swali safari hii tumpe nani nafasi ambae unaona anakipaji lakini hajapewa nafasi?. Jb anauliza..
Ni wakati wako sasa kupendekeza jina la masanii huyo.

MZURURAJI YAINGIA SOKONI LEO

Filamu mpya ya Mzururaji imeingia sokoni leo ikisambazwa na kampuni ya steps entertainment,filamu hiyo ambayo imeandikwa na Takura Maurayi inategemewa kufanya vizuri sokoni kutokana na story yake kuwa ya tofauti

akichezesha taya mmoja wawausika kwenye filamu hiyo Ayoub Kondo amesema kwenye filamu hiyo wamejaribu kuelezea kuwa sio kila mzururaji ukazani amepotea njia na sio kila kinga aacho ukajua nia dhahabu,miguu ndio silaha ya mwisho kabisa binadamu kaskazini,magharibi,kusini na mashariki ubinadamu wa damu

filamu hii inapatikana Tanzania nzima kwa bei poa kabisa pata nakala yako

NOMA SANAA,WAKATI WOLPER AKIKEMEA KITENDO CHA JINA LAKE KUANDIKWA KWENYE KOPO LA COCA COLA BILA RIDHAA YAKE,BONGO MOVIE WENGINE WAMEAMUA KUANDIKA MAJINA YAO WENYEWE BILA ATA KUPEWA ZAWADI HIZO

habari Followers pamoja na wa Tanzania wote ambao naamini huwa mnaingia katika page yangu ya insta.Nimepokea zawadi hii ya coca cola kwa siku 6 ,Na sio kwamba sikutaka kupiga picha kama wenzangu au ku post kama wenzangu ,nilikuwa natafakari Kweli Kampuni kubwa ya Kitaifa Na Kimataifa inaweza kutumia gharama kubwa kuandika majina Yetu bila kuchukuwa hata nafasi na heshima kubwa tuliyonayo kutushirikisha tu katika makubaliano ya kuandika majina Yetu Katika Makopo Yao.Maana Naamini maFan's wa woolper wangeweza kushare na coca cola kutokana Jina Langu kuwa label katika makopo yao.

Sasa Naamini tuna wanaharakati,wabunge,wanaSheria pamoja na serikali ambao huwa wanafwatilia wale wauza CD wa kariakoo basi Naomba Juhudi hizi mzihamishie huku katika kampuni hii kubwa ya Kimataifa coca cola ili kutetea haki za Wasanii na sio kudhalilishwa kwa kiasi hiki jamani.sijui kama wasanii wenzangu walilipwa siwezi kuwasemea lakini haya ni mawazo yangu binafsi. #shareaCokeTz

Wakati staa huyo wa filamu akijaribu kuelezea kitendo ambacho kampuni hiyo imekifanya hali imekua tofauti kwa mcheza filamu Niva Zubery baada ya kujiandika mwenyewe kwenye kopo la kinywaji hicho pendwa na badae kuiweka picha hiyo kwenye mitandao ya kijamii


Friday, 23 January 2015

NISHA NA GABO NDANI YA FILAMU MPYA INAITWA SHIDA CHEKI HAPA

WASTARA,ODAMA NA HEMEDY NDANI YA MOVIE MOJA CHEKI HAPA

WASTARA,THEA,WELU SENGO NA CASSIE KABWITA WAMFANYA KITU MBAYA JB CHEKI VIDEO HAPA

Ray – “Mwaka huu filamu za nje tu, ni mwendo wa Ghana na Nigeria”

Msanii mkongwe wa filamu nchini, Vicent Kigosi a.k.a Ray amejipanga kufanya filamu nyingi za kimataifa mwaka huu, huku akiweka bayana ataanza na Ghana pamoja na Nigeria.
Kwa mujibu wa tovuti Bongo5 , Ray amesema ndani ya mwaka huu ataweka pembeni kazi za ndani na kujikita kimataifa zaidi.
“Nimepanga kufanya mambo mengi mwaka huu, lakini mwaka huu movie zangu zote nitafanya International sitafanya movie yoyote ya hapa hapa kwa sababu kama hapa nishafanya sana, kwahiyo movie zangu zote nitakazocheza mwaka huu 90% nitacheza nje, kwahiyo kama kuna lolote ambalo litabadilisha nitawajulisha, ni mapema sana kusema lakini kitu ambacho ninaweza kuweka wazi ni nitaanza kazi na Nigeria na Ghana, ndani ya mwezi wa nne nadhani kazi zitakuwa zimeanza,” alisema Ray.
Mipango hii ya Ray inaonekana kja baada ya mwanadada Wema kwenda Ghana na kufanya filamu na Van Vicker.

Thursday, 22 January 2015

Dude akubaliana na bei ya Tshs. 1500 kwa filamu. Asema ndio njia pekee ya kupambana na uharamia.

Masanii wa filamu nchini Dude, amefunguka kwa kusema kuwa kwa kuwa serikali imeshindwa kupambana na wezi wa kazi za wasanii ni bora bei ya Steps Tsh 1500 iyendelee ili kuiyokoa tasinia hiyo.
Dude ameiambia tovuti ya Bongo5 kuwa hakuna njia kwa sasa ya kuweza kupambana na maharamia wa kazi za wasanii zaidi kushusha bei ya filamu.
“Tumeshindwa kuwathibiti pirates, watu wanasambaza kazi, wanauza kazi kwa bei rahisi, leo hii ukienda Buguruni unapata kazi kwa elfu mbili, elfu moja mia tano, filamu ambayo wewe unaiuza dukani elfu tano wenzako wanauza elfu mbili, kwakuwa watanzania wengi ni masikini hawawezi kwenda kununua kazi elfu tatu dukani wakati anaweza kupata kazi hiyo hiyo mtaani kwa elfu moja na mia tano. Kwahiyo hicho ndo kinachotuua sana sana, mimi kwa upande wangu kwakuwa serikali imeshindwa kutokomeza pirates, mimi naona steps kushusha bei ni sawa kwa sababu 

tunapambana na pirates, watanzania ambao wanaishi chini ya dola moja ndo wanunuzi wa kazi zetu, sisi kazi zetu hazinunuliwi na watu wa Masaki, watu wetu ni wa Mwananyamala, Magomeni, Gongolambo watu ambao wanakipato cha chini, sasa mtu kama huyo kweli atumie elfu tano yake anunue filamu? Ni wachache wanafanya hivyo ndiyo maana wanakimbilia kununu za bei ya chini, kwahiyo mimi steps naona wamechukua uwamuzi mzuri ambao una manufaa kwetu na kwao pia,” alisema Dude.

CHEKI PICHA ZA JB,WASTARA,THEA,WELU SENGO NA CASSIE KABWITA WAKIWA LOCATION FILAMU MPYA YA MZEE WA SWAGGA








Monday, 19 January 2015

Davina Ampigia Magoti Mama Kanumba

Mwigizaji mkongwe wa filamu Bongo, Halima Yahya ‘Davina’, amesema anamuomba radhi mama wa marehemu, Steven Kanumba, Flora Mtegoa kwa kutofika kwenye uzinduzi wa kitabu cha marehemu mwanaye kutokana na taarifa hiyo kutomfikia mapema.
Davina alikiri kuwa yeye ni mmoja kati ya wasanii ambao walikuwa karibu sana na marehemu enzi za uhai wake, akasema anaweza kuwa amekosea kwa namna moja au nyingine lakini kikubwa ni kwamba alipata taarifa muda ukiwa tayari umeenda.
“Ni kweli naweza kuchukua lawama kwa upande wangu, namuomba mama yangu anisamehe kwa sababu nilichelewa  kupata taarifa nilipompigia Maya kumbe ndiyo muda huo uzinduzi unafanyika,” alisema Davina.

Uzinduzi wa kitabu cha marehemu Kanumba kiitwacho The Great Fallen Tree ulifanyika  wikiendi iliyopita katika Ukumbi wa Landmark, Ubungo jijini Dar.
GPL

JB:Mwaka Huu Nitacheza Filamu Mbili Tu!!

Mwigizaji na mwongozaji wa filamu hapa bongo, Jacob stephen ‘JB’ ambae pia ni mkurugenzi na mliliki wa kampuni ya maswala ya filamu ya Jerusalem alitupia picha hiyo hapo juu na kuibandikia maelezo haya;
“Mzee huyo mwenye kofia anaitwa Chimbeni herry, hii ni moja kati ya scene utakazo ziona ndani ya mzee wa swaga.Hapo ni zanzibar,kati ya wasanii wazuri ambao hawajatumika vizuri ni pamoja na huyu.
Jamani anaweza,mwaka huu nitacheza filamu mbili (2) tu, lakini nitaanda nyingi ambazo nitawaachia watu wengine waonekane hasa Zanzibar,Mwanza,Arusha,Dodoma na Mbeya.
Hakika tutazalisha mastaa wengi kama tulivyofanya kwenye bado natafuta,wageni wangu na Chausiku,Jerusalem ni yenu vijana”. JB alimaliza

Thursday, 15 January 2015

SALMA NISHA:NAOMBA STEPS ISHUSHE BEI YA FILAMU ILI WANAOKODISHA WAACHE NA WAANZE KUUZA FILAMU NA KUPATA FAIDA BADALA YA KUKODISHA


Mcheza filamu za kitanzania Salma Jabu Nisha ameelezea hisia zake juu ya kampuni ya Steps Entertainment kwa atua yake ya kushusha bei za filamu nchini

Kupitia ukurasa wake wa facebook Nisha ameandika hivi


Kikao cha kuhusu maswala ya bei za filamu kinatarajiwa kuanza hivi punde chini ya wizara 3 ambazo ni wizara ya habari michezo na utamaduni, wizara ya viwanda na biashara na wizara ya fedha.
Kwa msimamo wangu kama mfanya biashara wa filamu na msanii Tanzania,napendekeza bei ishuke ili watu wote wawe na uwezo wa kununua,haiwezekani tuwauzie mashabiki filamu kwa elf 3 wakati elf 1500 pia tunapaa faida,kwanini mununue filamu kwa bei kubwa filamu iliyokatwa katwa ambayo 

unaweza ifanya iwe part 1? Huo ni wizi wa wazi wazi @stepsentertainment imeleta vifaa vya kuzalisha kazi hapa nchini faida inapatikana kwanini tuuze bei kubwa?ili kunufaisha pirates wanaouza 500 kwa kazi za kuiba,kila siku tunapigana na pirates (wizi wa kazi za wasanii)lkn bado wapo,leo kushusha bei kwa nia ya kuzuia kuibiwa msanii na mnunuzi kuna wanaopinga,Natamani bei ishuke ili hawa wanaokodisha waanze kuuza wapate faida na wao,na wanao zikodi waanze kununua.
Ni aibu kubwa kwa tasnia kama hii kuuza nakala elfu 20 tu wakati watanzania tupo zaidi ya ml.47,sio kwamba haiuziki inauzika sana ila wanaofaidika ni wale wanaoiba.

Wednesday, 14 January 2015

FILAMU YA MIKONO SALAMA NI HISTORIA KWA JB

 Filamu ya mikono salama ni historia kwa JB kwakua ndio filamu ya mwisho kushiriki na marehemu Adamu Kuambiana,filamu hiyo imewashirikisha mastaa wengine kama vile Joketi na RIchie



Inasambazwa na kampuni ya steps entertainment pata nakala yako sasa uone kitu alichokifanya Adamu kuambianai

THE BLOOD STORY OF A MURDERER YAKAMILIKA











AMANDA ACHAFUKA MTANDAONI

MSANII wa filamu Bongo, Tamrina Poshi maarufu kama Amanda, amechafuka baada ya mtu anayejitambulisha kwa jina lake, kujinadi kwa kujitongozesha katika mtandao wa kijamii wa Facebook.

Amanda huyo feki amekuwa akijiuza bila aibu katika mtandao huo kwa kujitongozesha kwa wanaume, kitu kinachomuumiza muigizaji huyo ambaye pia anawashangaza wasanii wenzake juu ya tabia hiyo ya kuchefua.

“Yaani nimekuwa nikiulizwa sana, lakini juzi ndipo nilishtuliwa na msanii mwenzangu, nikafanya uchunguzi na kugundua kwamba kuna mtu ananichafua kupitia mtandao, mashabiki wangu watambue kuwa mimi sijawahi kujiuza na ninajiheshimu,” alisema Amanda.

Monday, 12 January 2015

WILLIAMU MTITU NA BOND BIN SINAN WATIBUANA FACEBOOK KISA BONDI KUTETEA KAMPUNI YA STEPS KUSHA BEI YA FIALMU ZAKE

  • 0 hrs · Like
  • William Mtitu Kabuti nimeitika kaka plz mimi siongei na vibaraka wa diresh ambao ili waende chooni lazima diresh acheke ambao miaka mitatu nyuma awakuwepo katika hii tasnia leo wanaongea sana kutetea usenge wanaotaka kuuleta katika hii tasnia eti wana uchungu na tasnia na STEPS usenge huu kwanza plz BOND NAKUHESHIMU SANA SITAKI TENA ULITAJE JINA LANGU KOKOTE KULE MIMI SIO RAFIKI YANGU NA ATUNA MAHUSIANO YEYOTE NA WEWE WALA KAMPUNI YANGU ATA KIPINDI CHAKO BATTLE YANGU NA DIRESH AIKUHUSU HATA KIDOGO.


  • 20 hrs · Like · 2
  • Bond Bin Sinnan Huyo ndio William Mtitu anesema anauchungu na ananiheshimu ambae Kabuti Onyango amemuita aje aweke hoja yake kwann hataki bei ishushwe na ili tasnia ipate hadhi na wasanii wasiwe ma malaya na majambazi ananitukana na hataki jina lake nilitaje popote nadhani mwenye akili timamu na mwenye uchungu na tasnia hii kashazijua mbivu na mbichi. Nisamehe kaka Mtitu na hakuna sehemu nimekutukana au kukukashifu na pia sijakuita hapa ni sijakutag na post yangu. Pia wewe umelitaja jina langu basi tuwe na amani tu. Pigania mkate wako na mimi na ukibaraka na njaa yangu ntaendelea kuwa navyo. Ila mwisho wa siku ukweli utabaki palepale. Asantee
    20 hrs · Like · 1