Tuesday 28 October 2014

KABUTI ONYANGO;WASTARA,NISHA NA SHAMSA FORD NDIO WASANII WAKIKE WANAOLETA CHANGAMOTO KWENYE TASNIA YA FILAMU

 Camera man mwenye jina kubwa kwenye tasnia ya filamu kwa hivi sasa Kabuti Onyango ameshindwa kuficha hisia zake na kuamua kutoa yamoyoni kuhusiana na wacheza filamu wakike wanaosumbua kwenye soko la filamu kwa hivi sasa hapa nchini
 Akifunguka kiafrika bila hofu yoyote amesema kwa hivi sasa kwenye tasnia ya filamu hakuna kama Wastara,Nisha na Shamsha ford na kwamba hao ndio vinala wake.
Amesema Wastara ni msanii anaebadilika kuendana na jamii yake na ukiangalia kwenye filamu ya Gumzo aliyocheza na Nisha ni tofauti kabisa na filamu ya Uaminifu Dhaifu inayosumbua kwa hivi sasa sokoni kwani ameonesha uwezo mkubwa sana
Kabuti pia amesema Salma Nisha ni msanii ambae amaejinyakulia tuzo ya uchekeshaji bora kuoitia tuzo za action and cut na kwamba filamu zake za Gumzo,Tikisa na zena na betina zimemuweka kwenye orodha ya wacheza filamu wakike wanaokubalika kwa hivi sasa hapa bongo.

Kwa upande wa Shamsa Ford yeye ajawai kushuka tangu alipocheza filamu ya Saturday morning ya marehemu Kanumba na nyota yake inazidi kuwa juu siku adi siku,na amekua kivutio kikubwa kwa watu mara baada ya kucheza filamu mpya ya chausiku amabayo amevaa uhusika wa tofauti sanaa

filamu zote hizo zinazowaweka juu wasanii hawa zinasambazwa na kampuni kubwa ya usambazaji nchini stepsentertainment ambayo kwa kiasi kikbwa inasaidia sanaa ya Tanzania kwenda mbali zaidi

No comments:

Post a Comment