MSANII wa filamu Bongo, Wastara Juma amemuumbua msanii mwenzake Deogratius Shija baada ya kutoa taarifa zinazoonekana ni za uongo.
Awali Wastara ambaye hivi karibuni alinyakua tuzo ya Muigizaji Bora wa
Kike wa mwaka kwenye tuzo za Action and Cuts, alimshukuru Mzee Majuto
kwamba ndiye aliyemtoa kisanaa jambo ambalo limemhuzunisha Shija na
kusema anashangaa kwa kuwa yeye ndiye aliyemtoa.
Kufuatia maelezo hayo, Wastara amesema, taarifa aliyoitoa Shija ni ya
uongo kwani filamu ya kwanza kabisa alicheza na Mzee Majuto ndiyo maana
alimshukuru, ya pili alicheza na Frank Mwikongi na ya tatu ndiyo ya
Shija.
“Nimemshukuru Mzee Majuto kwa kuwa ndiye wa kwanza kunitoa, huyo Shija
nimecheza naye filamu ya tatu, sasa anacholaumu nini? Mimi huwa sipendi
lawama za kijinga,” alisema Wastara.
No comments:
Post a Comment